Jeshi la Polisi laonya walevi watakaoenda katika maeneo ya starehe na vyombo vya usafiri

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,047
2,000
Jeshi la Polisi limesema litafuatilia watumiaji vyombo vya usafiri watakaotoka katika sehemu za starehe katika sikukuu hizi kwa lengo la kuwapima viwango vya ulevi.

Wale watakaopatikana viwango vya juu vya ulevi na huku wakiendesha vyombo hivyo, watakamatwa na kufikishwa vituoni kwa hatua mbalimbali za kisheria.

Akiongea Kupitia TBC 1, Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani Afande Mpinga amewataka watumiaji wote wa vileo wenye vyombo vya usafiri kuwa na madereva au wakodi taxi.
 
bullbar

Senior Member
Oct 21, 2014
133
225
ningeshangaaa wapite bila tamko..hapo bia mbili utaambiwa umekunywa kreti zima!! PRA mtuache kidogo basii khaah
 
silasc

JF-Expert Member
Feb 10, 2013
3,356
2,000
Jeshi la Polisi limesema litafuatilia watumiaji vyombo vya usafiri watakaotoka katika sehemu za starehe katika sikukuu hizi kwa lengo la kuwapima viwango vya ulevi.

Wale watakaopatikana viwango vya juu vya ulevi na huku wakiendesha vyombo hivyo, watakamatwa na kufikishwa vituoni kwa hatua mbalimbali za kisheria.

Akiongea Kupitia TBC 1, Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani Afande Mpinga amewataka watumiaji wote wa vileo wenye vyombo vya usafiri kuwa na madereva au wakodi taxi.
Kuna mbinu mpya wanatumia madereva wa mikoani nimeisikia baadhi wakitoa ushuhuda Shinyanga stendi. Ilitulazimu kulala pale kulingana na utaratibu wa wa sasa wa jeshi la polisi kuhusu safari ya Dar-Mwanza.
Madereva wawili walikiri kuwa kwa sasa baada ya kutumia kilevi hulazimika kusukutua mdomo na mafuta aina ya disel. Hii hufanya kile kipimo kuonyesha kuwa hajatumia kilevi hata kama anaonekana amelewa.
Sidhani kama jeshi la polisi wameshtukia hili.
 
adden

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
5,134
2,000
ingekuwa vizuri kama wangepaki difenda zao kwenye mabaa wakamate ataepanda gari amelewa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom