Jeshi la polisi lakamata watuhumiwa 711 kwenye operesheni kubwa ndani ya siku 5 Dar

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Kamanda wa polisi jijini Dar Simon Sirro amesema wamekamata wahalifu 711 kwenye operesheni kubwa walioifanya ndani ya siku 5.

Watuhumiwa hao wamekamatwa kwa makosa mbalimbali, pia wamekamatwa na vitu kama silaha za kisasa za moto na silaha za kienyeji, vifaa mbalimbali vya kufanyia uhalifu, mifuko ya sukari isiyolipiwa ushuru, gari zilizoibwa. Pia kwenye operesheni hiyo wamekamata panya road 8

 
Source Azam Tv News

Polisi kanda maalum ya Dar inawashikilia watuhumiwa 700 wa makosa mbali mbali ndani ya siku Nne....

Swali kwa idadi hiyo je tuko salama? Napongeza jitahada za Polisi wetu chini ya Kamanda Sirro ila napatwa na mashaka na idadi hiyo maana inatisha na kuogofya...
 
Source Azam Tv News
Polisi kanda maalum ya Dar inawashikilia watuhumiwa 700 wa makosa mbali mbali ndani ya siku Nne....
Swali kwa idadi hiyo je tuko salama? Napongeza jitahada za Polisi wetu chini ya Kamanda Sirro ila napatwa na mashaka na idadi hiyo maana inatisha na kuogofya...

Unapongeza nini sasa, kama amewaonea, ni kweli wote hao ni wahalifu? Screening ilikuwaje. Nani asiyejua mambo ya polisi! Kama wanaweza kufanya yaliyofanyika kahama, why not here
 
UNAPONGEZA NINI SASA, KAMA AMEWAONEA, NI KWELI WOTE HAO NI WAHALIFU? SCREENING ILIKUWAJE. Nani asiyejua mambo ya polisi! kAMA WANAWEZA KUFANYA YALIYOFANYIKA KAHAMA, WHY NOT HERE
Ngoja tuwapongeze mkuu, usiwe negative sana
 
Watu 711 ni watu wengi sana kwa siku 5 tu, tena kwa dar peke yake.

Mwezi mtukufu wa Ramadhan kama huu tumuabudu Allah na tuache vitendo viovu, kuuheshimu mwezi pamoja na kuwa na tabia njema na kujiepusha na matukio ya uvunjifu wa amani kwa kutii na kufuata sheria za nchi na dini.
 
serikali ijenge magereza mengne maana waharifu wanaongezeka na sheria kali znaendelea kutungwa.

kazi nzuri kwa jeshi la polisi
 
ni vema piaka ma tukiwa tunaambiwa ni wangapi wamefikishwa mahakamani.

Walishakamatwaga panya road 500 lakini hakukuwa na mrejesho.
 
Police wetu mnafanya kazi nzuri sana. Hongereni na Mungu awatie nguvu katika Utendaji wenu. Kazi yenu ni ngumu sana Mh. Rais watazame hawa jamaa kwa jicho la tatu na uwaboreshee maslahi yao.
 
Back
Top Bottom