Jeshi la Polisi kuwafikisha mahakamani madereva waliosababisha ajali ya Singida

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani limesema litawafikisha mahakamani madereva waliosababisha ajali ya vifo vya watu 30 pamoja na majeruhi 48 huko Manyoni mkoani Singida kwa kosa la kuuwa bila kukusudia huku likitoa onyo na kuhaidi kutoa adhabu kali kwa madereva watakao bainika kufanya mzaa wakati wa kupishana.

Chanzo: ITV
 
Watafikishwa mahakani kumbe jamaa walikuwa wanatimiza hesabu ya boss(Kafara) ili boss aongeze mabasi mengine.
 
Sumatra pia wameyafungia kutoa huduma mabas mengine ya kampuni hiyo ya city boy,nadhan hii si sahihi maana ni kuwanyima huduma wananchi wanaotegemea usafiri wa kampuni hii.wao wangeshugulika na hao hao waliosababiasha ajali hiyo,samaki mmoja akioza huwezi tupa tenga zima!
 
hope watapewa mvua za kutosha
siku zote ukisafiri kaa upande wa dereva...,
dereva ikitokea ajali anakwepeshea upande wake
 
Dereva mmoja alisepa hawajamuona so watakaempeleka ni yule aliyekua upande wake hakuama njia.......wanasheria wabobezi saidieni hapa huyu dereva akikomaa kuwa hakuama njia alifatwa kwenye njia yake je ?
Na yule dereva aliyehama njia hajapatikana mpaka muda huu maana alikimbia
 
Ajari hii ni uzembe uliopitiliza, na kwanini kila wakikutana wanasalimiana kwa kupishana? Na story hii nimeshawahi kuisikia tangu kitambo, na yawezekana yakawa maagizo kutoka kwa mmiliki maana wamiliki wengi sana wa mabasi ushirikina na makafara ni mengi muno, hawaoni uchungu wa kumwaga damu ya watu
 
1. Ikitokea ajali mbaya na ya kizembe halafu DEREVA akawa bado yupo hai huyo dereva anyongwe hapo hapo ndani ya saa 24 .
2. Ikitokea ajali mbaya na ya kizembe ambayo kuna ABIRIA wengine wamepona na wakitoa ushuhuda wao wanasema dereva alikuwa mwendokasi basi hao abiria wote waliobaki wapigwe viboko vikali sana sita ( 6 ) au watembee kwa miguu kutoka hapo eneo la ajali hadi huko waendako . Kwani nilichokigundua katika moja ya watu muhimu wanaosababisha hizi ajali ni sisi abiria yaani mimi na wewe na wengi wetu hufurahia mno spidi zile huko njiani kiasi kwamba tukiona gari halikimbii " tunamnunia " na kuanza " kumdharau " dereva.
3. Kama ajali ikitokea kutokana na ubovu wa barabara husika ambayo pengine imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu basi wahusika kuanzia WAZIRI wa WIZARA husika, SUMATRA na TANROADS Mkoa wote wahukumiwe kifungo cha maisha jela .
4. Kama ajali ikitokea eneo ambalo kuna Matrafiki au Matrafiki muda mfupi tu uliopita walilikagua hilo basi ambalo pengine lilikuwa na
matatizo ya kiufundi lakini kwa
tabia yao ya kupenda rushwa wakaliruhusu basi kuanzia Kiongozi wa Trafiki wa Mkoa husika na wale Matrafiki wote wa zamu wanyongwe ndani ya saa 24 .
5. Kama ajali ya kizembe ikitokea na ikajulikana kuwa lile basi lilikuwa na matatizo ya kiufundi ya
muda mrefu na Mmiliki wake anafahamu ila kwa kudharau tu na
kutudharau sisi abiria akatupuuza basi Mmiliki wake apelekwe kati ya Mto Ruaha au Kagera au Mara ambapo kuna Mamba wengi na wenye hasira kisha " arushwe " tu hapo awe kitoweo chao " murua " cha siku.
Nina uhakika hizi hatua zikichukuliwa tutazuia ajali hizi za kizembe kwa 100% labda tu zile ambazo haziepukiki na kiukweli unaona kuwa haikuwezekana kuepukika japo hata hizi nazo pia tunaweza kumtupia lawama
MALAIKA kwanini hakuziepusha.
Mamlaka husika ichukueni hii na ipo siku mtakuja kunikumbuka kwa wazo langu hili kwani tumechoka na Ndugu, Marafiki na Watanzania wenzetu kupoteza maisha kwa uzembe tu wa Watu wachache wasiojitambua na kujali maisha ya Watu.
Ajali ya Singida imenipandisha sana na mno hasira!
 
Hawa madreka waliponaje,mgongano wa uso kwa uso?

Mkuu, hawa watu hupishania kulia kila wakikutana, yan basi linahama site yake na kwenda upande wa kulia
Mpaka hapa ebu vuta taswira kichwani halafu ukiwa bado hujapata picha I will back kuelezea
 
hope watapewa mvua za kutosha
siku zote ukisafiri kaa upande wa dereva...,
dereva ikitokea ajali anakwepeshea upande wake

Ni kumwomba Mungu tu ajali isitokee kabisa ndo sahihi zaidi kwa sababu no one have idea ajali itatokeaje mtakufa tu wote na dereva. Ajali ngapi madereva wamekufa.

Au ile ajali ya iringa ambayo dereva aliruka akaliacha gari linaserereka lenyewe, what could one have done
 
Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani limesema litawafikisha mahakamani madereva waliosababisha ajali ya vifo vya watu 30 pamoja na majeruhi 48 huko Manyoni mkoani Singida kwa kosa la kuuwa bila kukusudia huku likitoa onyo na kuhaidi kutoa adhabu kali kwa madereva watakao bainika kufanya mzaa wakati wa kupishana.

Chanzo: ITV
Anayetoa adhabu kali kwa mkosaji ni jeshi la polisi au mahakama??
 
Back
Top Bottom