Jeshi la Polisi kutoa msimamo wake leo kuhusu kauli za 'Mzee wa upako' kwamba waliomchafua watakufa

DOFFA

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
425
233
Siku moja baada ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako kusema waandishi waliomuandika vibaya watakufa kabla ya Machi 2017, Jeshi la Polisi linatarajia kutoa msimamo wake dhidi ya kauli hiyo leo.

Kauli hiyo ya Mzee wa Upako aliyoitoa juzi kanisani kwake, ilikuwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu madai ya kulewa na kumfanyia fujo jirani.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro jana alisema ni mapema kuzungumzia sakata hilo kwa sababu jana ilikuwa sikukuu na atatolea ufafanuzi leo.

“Anasema hao waandishi watakufa kabla ya Machi 2017 kwani yeye Mungu? Hilo ni suala zito, tumeandaa mkutano na waandishi wa habari tutalizungumzia suala hilo kesho (leo),” alisema Kamanda Sirro.

Katika kauli hiyo, Mzee wa Upako alisema kila mwandishi aliyemuandika vibaya ikifika Machi mwakani hatakuwa hai na kama wataendelea kuishi, ataacha kazi ya kuhubiri injili na kwenda kuuza gongo.
 
Huu utabiri wa MZEE wa upako na Lema uko wapi? Tunataka kuona huyu MZEE anatiwa Lupango mpaka march 2017 ili kama watakufa hao waandishi basi anyee ndoo maisha yake yote
 
Sasa mnamsumbua Lema kwanini wakati matamko Yao yako sawa,Kama Polisi unasema watakufa yeye ni Mungu,kwanini Lema mmem'gan'gania wakati matamshi yake Hayana utofauti na Mzee wa Upako au kwakuwa yeye ni mpinzani wa kisiasa kwenye maslahi?
 
Hii tabia ya kutabiria watu kifo siyo nzuri. Mara hii tumeshasau wale watabiri maarufu waliomtabiria kifo yule mwanasiasa mkongwe halafu wakaishia kufa wao? Ni Mungu pekee Ajuaye juu ya kifo cha mtu. Mengine haya mbwembwe tu na kukufuru!
 
Huu unabii wa mzee wa upako si unafanana na ndoto ya mbunge wa Arusha Godbless Lema. Ngoja tuone hatua zitakazochukuliwa na vyombo vya usalama.
bora ya kaota kifi cha MTU.. huyu yy anahakikisha kabisa vifo vya watu..
hapa ndipo tutakapoona double standards
.... BT the way Mimi naona wangemuacha tu usikute wakati anatoa tamko hilo alikuwa amemka Nazo.
 
Kama kweli wataongelea jambo hilo ni dhahiri nafsi zimawasuta kuhusu Mh. Lema na Mzee wa upako katoa nafasi ya wao kupumua
Geshi na mbwembe zake
 
Pombe haina adabu....sasa hapo itamkosesha bahati....
-Hakumbuki kama aliahidiwa kujengewa barabara ya lami kuelekea kanisani kwake...nadhani imeota mbawa....
Pole yake.....
"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"....by Our almight God.
 
Huu unabii wa mzee wa upako si unafanana na ndoto ya mbunge wa Arusha Godbless Lema. Ngoja tuone hatua zitakazochukuliwa na vyombo vya usalama.

Vipi ile ndoto ya Babu Wassira kuwa CHADEMA itakufa 2015? Badala yake zikafa ndoto zake za Urais na hata za Ubunge tena mkonoini mwa mwana CHADEMA!
 
Inashangaza kuona huyu mlevi bado anapewa hela za sadaka na waumini wake.
 
Siku moja baada ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako kusema waandishi waliomuandika vibaya watakufa kabla ya Machi 2017, Jeshi la Polisi linatarajia kutoa msimamo wake dhidi ya kauli hiyo leo.

Kauli hiyo ya Mzee wa Upako aliyoitoa juzi kanisani kwake, ilikuwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu madai ya kulewa na kumfanyia fujo jirani.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro jana alisema ni mapema kuzungumzia sakata hilo kwa sababu jana ilikuwa sikukuu na atatolea ufafanuzi leo.

“Anasema hao waandishi watakufa kabla ya Machi 2017 kwani yeye Mungu? Hilo ni suala zito, tumeandaa mkutano na waandishi wa habari tutalizungumzia suala hilo kesho (leo),” alisema Kamanda Sirro.

Katika kauli hiyo, Mzee wa Upako alisema kila mwandishi aliyemuandika vibaya ikifika Machi mwakani hatakuwa hai na kama wataendelea kuishi, ataacha kazi ya kuhubiri injili na kwenda kuuza gongo.
Umeandaa mkutano wa waandishi wa habari wakati maisha ya watu wako hatarini? Mimi nilitarajia kuwa huyo alitabiri vifo yupo ndani kama mh. Lema Ndio uje kuongea na waandishi
 
Back
Top Bottom