Jeshi la Polisi kutoa msimamo wake leo kuhusu kauli za 'Mzee wa upako' kwamba waliomchafua watakufa

huyu mchungaji mlevi hadi kufika march mwakani atakufa kwa njaa Kwa kukosa sadaka au nusu ya waumini wake watamkimbia
huu ni utabiri wangu kwake,hiyo mikwala yake akawatishe watoto wake na misukule(waumini)wake yeye nani mpaka awatabirie kifo waandishi?
Kwani wewe ulimuandika vibaya??
 
Police imekuwa ya kutoa matamko na kuongea na waandishi wa habari...hizi ndio actions
 
Huu unabii wa mzee wa upako si unafanana na ndoto ya mbunge wa Arusha Godbless Lema. Ngoja tuone hatua zitakazochukuliwa na vyombo vya usalama.
Je, Lema kwao ni mungu mpaka wamshtaki?

Ni wazi dola ipo zaidi kwa ajili ya kuwashuhulikia upinzani
 
Huu unabii wa mzee wa upako si unafanana na ndoto ya mbunge wa Arusha Godbless Lema. Ngoja tuone hatua zitakazochukuliwa na vyombo vya usalama.
Lema anafananishwaje hapa?unafikiri kutumia ubongo kweli au sehemu tofauti?
 
Nimesikia ''mchungaji'' katoa 'kiapo' kuwa wale wote walio mnanga kwenye maadishi yao basi wajitayarishe ku resti ini pisi.. sasa kwa heshima na taadhima najitokeza kuwaombea msamaha hawa waandishi wetu maana mmoja wapo ni mdogo wangu, ndugu mchungaji wasamehe BURE tu walipitiwa na shetani.

Asante sana ..
 
Siku moja baada ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako kusema waandishi waliomuandika vibaya watakufa kabla ya Machi 2017, Jeshi la Polisi linatarajia kutoa msimamo wake dhidi ya kauli hiyo leo.

Kauli hiyo ya Mzee wa Upako aliyoitoa juzi kanisani kwake, ilikuwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu madai ya kulewa na kumfanyia fujo jirani.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro jana alisema ni mapema kuzungumzia sakata hilo kwa sababu jana ilikuwa sikukuu na atatolea ufafanuzi leo.

“Anasema hao waandishi watakufa kabla ya Machi 2017 kwani yeye Mungu? Hilo ni suala zito, tumeandaa mkutano na waandishi wa habari tutalizungumzia suala hilo kesho (leo),” alisema Kamanda Sirro.

Katika kauli hiyo, Mzee wa Upako alisema kila mwandishi aliyemuandika vibaya ikifika Machi mwakani hatakuwa hai na kama wataendelea kuishi, ataacha kazi ya kuhubiri injili na kwenda kuuza gongo.
Sirro mwenyewe anaogopa kufa unadhani atatoa kauli
 
kwani polisi hawajaangalia video yake vizuri mbona alitishia kupiga watu risasi...watuondolee unafiki
 
Siku moja baada ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako kusema waandishi waliomuandika vibaya watakufa kabla ya Machi 2017, Jeshi la Polisi linatarajia kutoa msimamo wake dhidi ya kauli hiyo leo.

Kauli hiyo ya Mzee wa Upako aliyoitoa juzi kanisani kwake, ilikuwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu madai ya kulewa na kumfanyia fujo jirani.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro jana alisema ni mapema kuzungumzia sakata hilo kwa sababu jana ilikuwa sikukuu na atatolea ufafanuzi leo.

“Anasema hao waandishi watakufa kabla ya Machi 2017 kwani yeye Mungu? Hilo ni suala zito, tumeandaa mkutano na waandishi wa habari tutalizungumzia suala hilo kesho (leo),” alisema Kamanda Sirro.

Katika kauli hiyo, Mzee wa Upako alisema kila mwandishi aliyemuandika vibaya ikifika Machi mwakani hatakuwa hai na kama wataendelea kuishi, ataacha kazi ya kuhubiri injili na kwenda kuuza gongo.
Nasubiria Polisi wamuweke ndani Bila dhamana kama walivyo fanya kwa Lema.
 
List tunayo tunasubiri machi 2017 ifike tuone wangapi watakuwa wamekufa, jamaa ajiandae kuuza Gongo.
 
Nna mashaka sana na akili za waumini wa huyu mzee...!
Mambo ya kishetani au giza yana mwisho mbaya. Makucha yameanza kujitokeza. Matusi, vitisho, sijui ulevi.... vyote tunaviona na kusikia kwa masikio yetu hata uki google kwenye google videos utapata na kuchambua mbichi na mbivu. Anayezungumza kwenye video kwa kutukana na vitisho ni yeye. Kwanini alaumu wengine?

Eti kuuza gongo....????? Huyu mtu sio Mkristo wala sio Msilamu. Hana chembe za upendo wa MUNGU, Bali ni upande mwingine kabisa.Wakristo na Waislamu hawamkubali. Nadhani anaweza akaua kwa wazi au kwa siri. Kwa kufuatia matamshi yake ni mtu hatari. Anaonekana ana hasira na sijui kama anamiliki silaha au la.

Labda wajaribu kumsaidia kisaikolojia ili apone. Labda ni kiburi cha pesa au sifa?????

Je hakuna chombo cha wachungaji, mashehe au dini ya kumsaidia mtu aliyeingilia shughuli zao ili mtu huyu asiharibu imani za watu?
 
Mbona ata mkulu alitabiri kua JK,LOWASSA n.a. yeye atakufa lkn hamna walio uliza kwanini alisema hivyo
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom