Jeshi la polisi kuondolewa kodi kwenye bidhaa za ujenzi wakati raia wanateseka ni ubaguzi

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
SERIKALI imeondoa kodi kwenye baadhi ya bidhaa za ujenzi kwa askari polisi ili kuwawezesha kujenga nyumba kwa gharama nafuu kulingana na vipato vyao.Hatua hiyo imechukuliwa
siku chache baada ya Kambi ya Upinzani Bungeni kulia na serikali kuhusu huduma duni inazotoa kwa askari polisi, hatua iliyotafsiriwa kuwa kambi hiyo ilikuwa inawachochea askari hao kugoma.

Hayo yalibainishwa jana na Kamishna ya Idara ya Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Patrick Kassera wakati akifungua mafunzo ya usimamizi wa udhibiti na uendeshaji wa maduka ya bidhaa zenye msamaha wa kodi kwa Jeshi la Polisi iliyofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi(CCP).

Bw. Kassera alisema msamaha huo wa kodi kwa maduka ya jeshi ni mwendelezo wa msamaha ambao ulikuwepo kwa muda mrefu wa vinywaji vya bia na soda ambao ulikuwa kwa lengo la kuwapa askari motisha ya kufanya kazi.

Alisema msamaha wa sasa unalengo la kumnufaisha askari zaidi na kumuongezea uwezo wa kununua bidhaa muhimu zinazohitajika.

“Kwa kuzingatia hali halisi ya kazi za askari, ambapo muda mwingi anakuwa kazini na hivyo hana muda wa kufanya kazi nyingine ya kumuongezea kipato, ili kujiendeleza ikilinganishwa na watumishi wengine wa umma," alisema na kuongeza;

"Serikali imeondoa kodi kwenye baadhi ya bidhaa za ujenzi vinavyouzwa kwenye maduka hayo ya polisi ili askari waweze kujenga nyumba kwa gharama nafuu.”

Kamishna alitumia nafasi hiyo kuwataka askari kuhakikisha wanatumia fursa hiyo vizuri.

Alisema hatarajii kusikia ofisa yeyote amechukua bidhaa na kupeleka nje au kwa ndugu yake, kwani kufanya hivyo ni kukiuka matakwa na kusudio la serikali.

Kwa mujibu wa kamishana huyo misamaha ya kodi imekuwa ikipunguzia serikali mapato yake na kupunguza uwezo wake wa kuwahudumia wananchi.

Msamaha wa kodi uliotolewa safari hii ni kwa askari wote bila kubagua kwa kuangalia cheo, hivyo ni wajibu wa wasimamizi wakuu kuhakikisha kila askari anafaidika na msamaha huo.
 
Ni ubaguzi na ujinga kwa serikali. Kuna wakulima na wafanyabiashara ndogondogo kibao ambao nao wanahitaji makazi bora na hawana hata kipato cha kufikia cha hao mapolisi. Na hilo pengo la mapato litakalotokana na msamaha huo wanaongezewa hao wakulima na wafanyabiashara maskini. Kwanini wasijifunze kwa CDM waliopanga kupunguza kodi za vifaa vya ujenzi ili wananchi wote waweze kujenga? Shwaini kabisa.
 
Na hata wakipewa huo msamaha hivyo vifaa vya ujenzi vitabaki madukani kwa wahindi na wao kupewa pesa kidogo

Ni ubaguzi na ujinga kwa serikali. Kuna wakulima na wafanyabiashara ndogondogo kibao ambao nao wanahitaji makazi bora na hawana hata kipato cha kufikia cha hao mapolisi. Na hilo pengo la mapato litakalotokana na msamaha huo wanaongezewa hao wakulima na wafanyabiashara maskini. Kwanini wasijifunze kwa CDM waliopanga kupunguza kodi za vifaa vya ujenzi ili wananchi wote waweze kujenga? Shwaini kabisa.
 
Ubaguzi huo mbona wakulima na wafugaji hawana msamaha wowote,na kutoa VAT kwenye migodi pamoja na wanaohudumia pia na mafuta ya diesel na petrol wanasaidia matajiri wa Barrick au GGM au ndio ufisadi wenyewe
 
Mbona kodi zimeondolewa kwa bidhaa za kanisa ..ni sawa wacha polisi wafaidi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom