Jeshi la Polisi kujipa jukumu la kuchunguza mauaji ya askari, ni sawaswa na kesi ya nyani kumpa ngedere

Jeshi la Polisi nchini limejipa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyotokea kwenye daraja la selander, ambapo mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Hamza, aliwafyatulia risasi askari wawili na mlinzi mmoja wa kampuni ya SGA na kuwaua wote na askari wengine kadhaa kujeruhiwa na hatimaye yeye mwenyewe kuuawa na askari waliokuwa wakilinda doria eneo hilo

Kuna hadithi nyingi zinazosemwa semwa kuhusu nia ya huyo kijana aliyewafyatulia risasi askari hao.

Kuna wengine wanadai kuwa huyo kijana alikuwa analipiza kisasi kwa askari hao, baada ya kumdhulumu dhahabu zake ambazo alikuwa akiziuza.

Hebu tujiulize hivi hawa hawa Polisi watatoa ripoti bila kuuficha ukweli, hata kama ripoti hiyo itasema chanzo cha mauaji hayo ni wao Polisi kufanya dhuluma hiyo ya kumpora dhahabu zake huyo kijana??

Hata ukiangalia mazingira ya mauaji hayo, kwa huyo kijana kuwa-target maaskari watupu na kuwaacha raia, inadhibitisha tetesi hizo.

Ni kwanini basi isiundwe Tume huru ya kuchunguza chanzo cha mauaji hayo, Tume hiyo ihusishe na wataalam wengine kwa mfano majaji wastaafu, wanasiasa maarufu toka kwenye vyama vya siasa, na kadhalika na kadhalika.

Ninavyoona Mimi, kuunda Tume ya uchunguzi, ya maaskari watupu, ni sawaswa na kesi ya nyani kumpa ngedere!

Ni dhahiri hapo hata hayo matokeo ya uchunguzi wa Tume hiyo unaweza kuyabashiri

Sirro anajua watanzania wote ni wajinga tu. Ipo siku atajua kwamba hajui ni suala la muda tu.

Mwaka jana alijipa kazi ya kama hii ya kijichunguza kuhusiana na tuhuma za ocd wa Hai kufanya siasa kinyume cha maadili ya jeshi. Kajichunguza na kujipa report mwenyewe na kisha kumpa promotion mtuhumiwa kuwa rpc. Mzee sirro ninakukumbusha kwamba hii nchi ni ya Watanzania wote na wala si ya ccm kama unavyodhani wewe.
 
Hamza analituhumu Jeshi la Polisi iweje Polisi ndio wafanye Uchunguzi

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Inawezekana wewe ndio kituko. Jeshi la Polisi lazima lichunguze jinai au uhalifu kama huu maana ndio kazi yake ya msingi.
Kama ukisema hilo jeshi lisiwepo kabisa kwa sababu zako nitakuelewa.
Lakini kama lipo lazima lichunguze.
Je unaweza ku-share uzoefu wako, sehemu zingine Mapolisi wakishambuliwa specifically kama hivi, huwa anachunguza nani?!
Kunapokuwa na tetesi kutoka kwa wananchi kwamba jeshi la Polisi limehusika kwa namna moja ama nyingine katika uhalifu fulani,jeshi hilo haliwezi na halipaswi kujichunguza lenyewe.

Kwa kawaida inapaswa kuundwa tume huru ili kuchunguza tukio kama hilo.

Enzi za JK kamanda Zombe alituhumiwa na wananchi katika kuhusika na mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro.

Alichofanya kikwete ni kuunda tume huru ya kuchunguza tukio hilo badala ya Polisi(akina Zombe) kujichunguza wenyewe na mwisho wa siku walichokuwa wanahisi wananchi ilikuja kujulikana kuwa walikuwa sahihi.

Siku zote katika matukio ya kihalifu wananchi hawapaswi kupuuzwa na Serikali katika kile wanachokihisi unless hiyo Serikali iwe ni serikali fake kwa sababu wananchi ndiyo mashuhuda wa kwanza wa matukio ya kihalifu kwa sababu wanaishi na wahalifu huku mitaani.
 
Watajijua wenyewe,sisi tunasimama na report halisi ya kitaa,majirani,wauza madini wenzie,marafiki,class mate wenzie,,full stop.
 
Chadema kiukweli mmechachamaa kwelikweli... Uweledi wa kitaasisi zote nchini mnao nyie...... Badala ya kujiimarisha kisiasa mmejikita kuielekeza serikali nini cha kufanya...
Kama mmechanganyikiwa...??
 
Unechanganyikiwa wewe unayei-support serikali hii ya kionevu. Full stop
 
Mwaka jana alijipa kazi ya kama hii ya kijichunguza kuhusiana na tuhuma za ocd wa Hai kufanya siasa kinyume cha maadili ya jeshi. Kajichunguza na kujipa report mwenyewe na kisha kumpa promotion mtuhumiwa kuwa rpc. Mzee sirro ninakukumbusha kwamba hii nchi ni ya Watanzania wote na wala si ya ccm kama unavyodhani wewe.
Sirro ameharibu sana profile yake na anakwenda kustaafu kwa aibu kuu. Hakuna legacy yoyote ya maana aliyoacha nyuma yake.
 
Jeshi la Polisi nchini limejipa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyotokea kwenye daraja la selander, ambapo mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Hamza, aliwafyatulia risasi askari wawili na mlinzi mmoja wa kampuni ya SGA na kuwaua wote na askari wengine kadhaa kujeruhiwa na hatimaye yeye mwenyewe kuuawa na askari waliokuwa wakilinda doria eneo hilo

Kuna hadithi nyingi zinazosemwa semwa kuhusu nia ya huyo kijana aliyewafyatulia risasi askari hao.

Kuna wengine wanadai kuwa huyo kijana alikuwa analipiza kisasi kwa askari hao, baada ya kumdhulumu dhahabu zake ambazo alikuwa akiziuza.

Hebu tujiulize hivi hawa hawa Polisi watatoa ripoti bila kuuficha ukweli, hata kama ripoti hiyo itasema chanzo cha mauaji hayo ni wao Polisi kufanya dhuluma hiyo ya kumpora dhahabu zake huyo kijana??

Hata ukiangalia mazingira ya mauaji hayo, kwa huyo kijana kuwa-target maaskari watupu na kuwaacha raia, inadhibitisha tetesi hizo.

Ni kwanini basi isiundwe Tume huru ya kuchunguza chanzo cha mauaji hayo, Tume hiyo ihusishe na wataalam wengine kwa mfano majaji wastaafu, wanasiasa maarufu toka kwenye vyama vya siasa, na kadhalika na kadhalika.

Ninavyoona Mimi, kuunda Tume ya uchunguzi, ya maaskari watupu, ni sawaswa na kesi ya nyani kumpa ngedere!

Ni dhahiri hapo hata hayo matokeo ya uchunguzi wa Tume hiyo unaweza kuyabashiri
Ni dhairi ilitakiwa Timu huru/isiyotia shaka ya kiuchunguzi.
 
Jeshi la polisi linatakiwa kubadilika sana na kuacha uovu wao.
Leo hii ni hatari polisi kujua nyumbani kwako una kitu cha thamani!
Hivi pamoja na malalamiko yote haya ya wananchi, Jeshi la Polisi linashindwa vipi kujivua jukumu hili walilojipa la kufanya uchunguzi kwa tukio hili la Hamza na kuiachia Tume huru itakayochungiza sakata hilo kwa uwazi na Haki??
 
Na kada kindakindaki wa chama chaw ala.. Halafu (.... Kipenyo)

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
Kwanini tunasita kusema : Muuwaji alikua kada kindakindaki wa chama cha CCM na mjumbe wa chama halmashauri ya ILALA?
20210826_014448.jpg
 
Back
Top Bottom