Jeshi la Polisi kuchunguza kifo cha mfanyakazi wa ubalozi wa India

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Dar es Salaam, Polisi wanachunguza kifo cha mfanyakazi mwandamizi wa Ubalozi wa India nchini ambaye amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya 10, katika jengo moja lililopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam juzi usiku.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Ilala, Salim Rashid amesema mfanyakazi huyo ambaye ni raia wa India, alikuwa akifahamika kwa jina la Trilok Chopra (50).

“Bado tunaendelea kuchunguza sababu za yeye kufanya hivyo, lakini tunachochunguza ni kutaka kujua kama ni mauaji au alijirusha yeye mwenyewe,” amesema Rashid.

Marehemu ameacha mke na watoto wanne.
 
Back
Top Bottom