Jeshi la polisi kitengo cha barabarani ni kero sana

Mangungu

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
2,392
3,017
Salam.

Nipo safarini Tanga ,nimefika nimefika Tanga nakamatwa na Polisi kitengo cha barabarani kua gari inadaiwa deni kubwa zaidi ya Tshs 95,000 kwa makosa ya barabarani,yaliyotokea moja Kigamboni tarehe 25/8/2019 saa 11 alfajiri, huu mda nilikua nimelala kwangu, Kinzudi mtaa wa majengo, na kosa la pili kurasini tarehe 29/8/2019 saa 2 asubuhi huu mda wala sikuwa maeneo ya sabasaba,kwenye karatasi ya fine number za gari ni zangu,lakini liseni ya dereva sio yangu ni jina la mwanamke ambaye sio ndugu yangu wala mke wangu.. Na nyumbani kwangu kwenye kuweza endesha gari ni mke wangu tu.. Tarehe ya kwanza gari lilikua nyumbani,na tarehe ya pili gari nilikua nalo mimi..

Na wakati nabishana nao,wakasema hii tabia ya polisi kuwapa fine watu wengine inafanyika sana tena sana tu.. Sasa ngoja wafatilie..

Basi katika mabishano ya hapa na pale,wakasema ngoja wamutafute mwenye liseni,wakafanya kazi yao,wakampata dada yupo kigamboni,mme wake ni polisi... Dada yule akipigwa fine anamwambia bwana wake,wanaandika liseni ya mwanamke wake lakini number ya gari wanaweka.ya kwangu.. Na hii nilishawahi lipa fine kwa kosa kama hili huko nyuma.. Sasa this time nikaamua kukomaa nao
Baada ya uchunguzi wao wakapata jibu,kua nafanyiwa uhuni na mtu wa polisi na mke wake... Yaan wananipiga fine mimi kwa liseni ya mwanamke..

Sasa ninashauri polisi kitengo cha barabarani waache huu upuuzi,wanalipaka matope jeshi la polisi kwa upuuzi wa watu wachache...
 
Pole sana mkuu, ni moja ya changamoto kubwa hasa kwa madereva... Usipokuwa makini utalipa fine ambayo haikuhusu kabisa .
 
Back
Top Bottom