Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam lakamata silaha mbili aina ya bastola na kuwaua majambazi wawili

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,799
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUPATIKANA KWA SILAHA MBILI AINA YA BASTOLA NA KUUWAWA KWA MAJAMBAZI WAWILI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limefanikiwa kukamata silaha mbili aina ya bastola na kuwaua majambazi wawili katika matukio mawili tofauti.

Tukio la kwanza ,Mnamo tarehe 19.06.2020 majira ya saa mbili usiku huko maeneo ya Mbangala Zakhem Jeshi la Polisi Kanda Maalum lilifanikiwa kuzima tukio la ujambazi wa kutumia silaha uliokuwa umepangwa kufanyika katika maduka ya miamala ya fedha.

Majambazi hao wapatao watatu kabla ya kufanikisha azma yao ya ujambazi tayari Jeshi la Polisi lilikuwa limeisha pata taarifa kutoka kwa msiri wake na kuweka mtego katika eneo hilo na baada ya majambazi hao kubaini uwepo wa makachero katika eneo hilo walianza kufyatua risasi hovyo na ndipo askari walipoamua kujibu mashambulizi na kufanikiwa kumpiga risasi mgongoni jambazi mmoja na atimae kufariki dunia papo hapo na majambazi wengine wawili walifanikiwa kukimbia na kutoweka kusikojulikana.

Baada ya kupekuliwa jambazi huyo anayekadiliwa kuwa na miaka 35-40 alikutwa na bastola aina ya BROWNING yenye namba A 953749 na TZCAR 101379 ikiwa na risasi tano ndani ya kasha(Magazine)

Mwili wa marehemu umeifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na juhudi za kuwatafuta majambazi waliokimbia zinaendelea.

Tukio la pili,Mnamo tarehe 13.06.2020 majira ya saa nne usiku huko maeneo ya Shekilango karibu na bandari kavu kikosi kazi cha kupambana na ujambazi kikiwa kinawafatilia majambazi watatu waliokuwa kwenye pikipiki ghafla kilishambuliwa na majambazi hao na ndipo kilipoamua kujibu mapigo na kufanikiwa kumjeruhi kwa risasi jambazi mmoja na wengine wawili kukimbia.

Jambazi aliyejuruhiwa anakadiliwa kuwa na umri wa miaka 25-35 alifariki dunia akiwa njiani akikimbizwa hospitali na alipopekuliwa alikutwa na silaha bastola aina ya RIVOLVER iliyotengenezwa BRAZIL yenye namba J.006703 ikiwa na risasi nne ndani ya kasha (Magazine).

KUKAMATWA KWA MTANDAO WA WIZI WA MAGARI NA MAGARI YA WIZI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum linawashikilia watu watano kwa tuhuma za wizi wa magari hapa Jijini Dar es Salaam na kwenda kuyauza mikoani.

Watuhumiwa hao ni:-

1. Hatibu Mwinyi,35yrs,Mkazi wa Katoro Geita.

2. Onesfori Venance@Massawe, 28yrs, Mkazi wa Kimara.

3. Jabir Rajabu, 40yrs, Mkazi wa Nyamanoro Mwanza

4. Sanford Hezekia, 41yrs, Mkazi wa Nyakato Mhandu Mwanza.

5. Nasir Said, 44yrs, Mkazi wa Bushushu Shinyanga.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam katika kipindi cha kuanzia tarehe 28.05.2020 hadi 20.06.2020 lilifanya operesheni ya kuwasaka wahalifu wanaojihusisha na wizi wa magari na kufanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa hao waliokuwa wanaiba magari hapa DSM na kuyasafirisha hadi Mikoa ya Mwanza,Shinyanga na Geita kisha kuyauza.

Watuhumiwa hao walikamatwa na magari yafuatayo:-

1. T 425 DQE, TOYOTA KLUGER.

2. T 162 DBU, TOYOTA HARRIER.

3. T 423 CFF, TOYOTA NOAH

4. T 761 CVL, TOYOTA TOWN ACE na

5. T 999 DDF, TOYOTA IST.

Magari haya yote katika nyakati tofauti yaliibiwa hapa Jijini DSM na kupelekwa mikoa niliyoitaja.

Watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa mahakamani hivi karibuni kujibu tuhuma zao.

SACP-LAZARO B. MAMBOSASA,
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.
26/06/2020.
 
Polisi wangekuwa wanawavunja miguu tu ili waweze kuwahoji wapate mtandao wote ujambazi
 
hongera kamanda mambo sasa na timu yako nzima kwa kutuhakikishia usalama wakaazi wa jiji la DSM, hakika kwa sasa DSM sio tena kichaka cha ucjambazi/uhalifu,
wananchi wote wa jiji la DSM tutoe ushirikiano kwa jeshi letu ili tutokomeze uhalifu.
ushauri wangu kwa jeshi la polisi kwa kila wilaya za DSM,
1. tuhakikishe tunatokomeza vyanzo au magenge ya kihalifu ambayo ni vijiwe vya wavuta bangi, dawa za kulevya, magenge haya ya wahuni yapo ktk mitaa yetu ni magenge haya ndiyo huzalisha majanbazi wa badae, kila kituo cha polisi kina paswa kuyabaini magenge /vijiwe hivya na kuvitokomeza kabisa.
2. kipindi hiki tunacho elekea ktk uchaguzi mkuu ni vyema doria zikaimarishwa kila kona ya jiji, sio tu katikati ya mji bali hata pembezoni ambapo mipango huanzia.

3.viongozi wa serikali za mitaa washirikishwe ktk kufichua na kubaini magenge ya wahalifu ktk maeneo yao,

tukifanya hayo kwa ukamilifu na hakika tutakuwa tumengamiza mazalia ya uhalifu na hakika Dsm itakuwa shwari muda wote hakutakuwa hata na vibaka wa kuiba kandambili.
 
Mwananyamala kwa kopa kuna kituo cha polisi nyuma ya kituo cha polisi kuna wavuta bangi kama wote, safari ni ndefu sana
 
toa taarifa, ikishindikana hata makao makuu, tusijifunze kulalamika bila kuhangaika kwanza, jeshi la polisi la sasa linachukua hatua na kama wapo naami ni wachache tu ambao bado hawajajirekebisha.
tutoe taarifa
 
Hii haikubaliki kabisa. Majambazi nao ni watu wana haki kama binadamu wengine ya kuishi. Kwanini wasingewanyang'anya tu hizo silaha nakuwakamata bila kuwaua kwa kutumia mbinu walizofunzwa chuoni?

Tanzanian police does not value lives and this is fundamentally wrong and totally unacceptable!

Poleni wafiwa kwa kupoteza wapendwa wenu. Mjaliwe wepesi na faraja kipindi hiki kigumu na cha huzuni mnapitia.
 
1. Hatibu Mwinyi,35yrs,Mkazi wa Katoro Geita.

2. Onesfori Venance@Massawe, 28yrs, Mkazi wa Kimara.

3. Jabir Rajabu, 40yrs, Mkazi wa Nyamanoro Mwanza

4. Sanford Hezekia, 41yrs, Mkazi wa Nyakato Mhandu Mwanza.

5. Nasir Said, 44yrs, Mkazi wa Bushushu Shinyanga.
[/QUOTE]Dah naona majina yame balance. Hii inaleta faraja kuna uhiano. Kwasababu tumezoea majina ya ndugu zetu upande wa pili katika matukio kama haya.

Cc kahtaan @struggleman Bwanautam
 
Back
Top Bottom