Jeshi la polisi jirekebisheni, hivi ndivyo rushwa inavyopokelewa

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,186
9,288
Hebu jiulize kitu kimoja kwanini bus hata kama haipandishi wala kushusha abiria lakini lazima iingie stand ya maili moja?

Basi iko hivi,basi lazima iingie stand maili moja hata kama halishushi wala kupakia abiria,na linavyoingia tu lazima kutakua na askari analielekeza pa kusimama,na ukichunguza kwa makini kabisa mhudumu mmoja atashuka ataenda kwa wale juakali wa pale wanaouza maji na vitu vingine,huyu mfanyabiashara anakua karibu mno au nyuma ya askari hivyo yule mhudumu atatumbukiza 5000 kwenye kile kibox cha maji au soda au hata apples,na yule mfanyabiashara harakaharaka atasogea eneo lile.

Yule askari ataingia ndani atapiga mkwara mzito sana wa danganya toto kisha atashuka,hata kama bus linahitilafu fulani au tatizo flani atajitahidi kulifunika asilizungumzie kisha atashuka mhudumu ataingia ndani kisha bus linang'oa nanga na abiria wasijue kinachoendelea.

Hawa wafanyabiashara wa maili moja ndio watu wa kati wakupokea pesa kisha wanaondoka harakaharaka hadi bus liondoke. Pia vilevile kila daladala ya simu2000/kibaha inapoingia stand hiyo kuanzia saa nne asubuhi lazima utaona askari akiinyooshea mkono kwa maana ya kumwita mhudumu lakini ukichunguza kwa makini hii daladala haitasimama pale aliko askari wala askari hatoifata tena anaweza hata kujifanya yuko bize na mambo mengine kisha konda atakunja 3000tsh ataishika kwa kuibana nyuma ya ticketi kisha atarudi nyuma kule aliko askari ataenda kumpa ile pesa au akaja muuza maji akasema weka humu na ukiangalia kwa mbaaaali utaona yule askari anakuelekeza mpe huyo(yaani muuza maji)

Sasa ole wako ukatae kutoa hii pesa ndio utawajua wao kina nani Raha zaidi inakuja pale unapompata askari wa kike ukamlaghai na maneno matamu atakufungukia kila kitu,kwamba zile wanazikusanya na kumpelekea yule anaewapanga pale siku hiyo na aslimia fulani wanabaki nayo,wasipofanya hivyo hawatapangwa stand. Sasa swali la kujiuliza hawa askari wa tanzania hawalipwi mishahara kama askari wa kenya wanavyolipwa ?

Kama wanalipwa tamaa za nini?na wanaanzaje kwenda kukamata au kumwita fulani ni mhalifu bila kujiangalia wao kama ni wasafi au lah Kama wanalipwa na bado wanachukua hela za hawa wahudumu ambao wengi wao hawana mshahara hiyo ni dhambi kubwa.

TUSITAFUTANE JAMANI
 
Waacheni polisi wetu wanasaidia sana wananchi, hivi mnafikiri polisi wakikomaa sana maisha yataenda?
 
Hawa usipo watoa kidogo hata kama gari ni jipya,utatafutiwa kosa tu.
Utasikia mbona redio yako haishiki E-FM ilimradi tu uonekane unakosa.
 
Hebu jiulize kitu kimoja kwanini bus hata kama haipandishi wala kushusha abiria lakini lazima iingie stand ya maili moja?

Basi iko hivi,basi lazima iingie stand maili moja hata kama halishushi wala kupakia abiria,na linavyoingia tu lazima kutakua na askari analielekeza pa kusimama,na ukichunguza kwa makini kabisa mhudumu mmoja atashuka ataenda kwa wale juakali wa pale wanaouza maji na vitu vingine,huyu mfanyabiashara anakua karibu mno au nyuma ya askari hivyo yule mhudumu atatumbukiza 5000 kwenye kile kibox cha maji au soda au hata apples,na yule mfanyabiashara harakaharaka atasogea eneo lile.

Yule askari ataingia ndani atapiga mkwara mzito sana wa danganya toto kisha atashuka,hata kama bus linahitilafu fulani au tatizo flani atajitahidi kulifunika asilizungumzie kisha atashuka mhudumu ataingia ndani kisha bus linang'oa nanga na abiria wasijue kinachoendelea.

Hawa wafanyabiashara wa maili moja ndio watu wa kati wakupokea pesa kisha wanaondoka harakaharaka hadi bus liondoke. Pia vilevile kila daladala ya simu2000/kibaha inapoingia stand hiyo kuanzia saa nne asubuhi lazima utaona askari akiinyooshea mkono kwa maana ya kumwita mhudumu lakini ukichunguza kwa makini hii daladala haitasimama pale aliko askari wala askari hatoifata tena anaweza hata kujifanya yuko bize na mambo mengine kisha konda atakunja 3000tsh ataishika kwa kuibana nyuma ya ticketi kisha atarudi nyuma kule aliko askari ataenda kumpa ile pesa au akaja muuza maji akasema weka humu na ukiangalia kwa mbaaaali utaona yule askari anakuelekeza mpe huyo(yaani muuza maji)

Sasa ole wako ukatae kutoa hii pesa ndio utawajua wao kina nani Raha zaidi inakuja pale unapompata askari wa kike ukamlaghai na maneno matamu atakufungukia kila kitu,kwamba zile wanazikusanya na kumpelekea yule anaewapanga pale siku hiyo na aslimia fulani wanabaki nayo,wasipofanya hivyo hawatapangwa stand. Sasa swali la kujiuliza hawa askari wa tanzania hawalipwi mishahara kama askari wa kenya wanavyolipwa ?

Kama wanalipwa tamaa za nini?na wanaanzaje kwenda kukamata au kumwita fulani ni mhalifu bila kujiangalia wao kama ni wasafi au lah Kama wanalipwa na bado wanachukua hela za hawa wahudumu ambao wengi wao hawana mshahara hiyo ni dhambi kubwa.

TUSITAFUTANE JAMANI
Huku ni kusaidiana ndugu zanguni...... ni nani asiyeijua khali ni ngumu?
Mbona ma trillioni ya kodi yanakusanywa hatupewi report yamefanyia nini?
Huku ni kujiongeza...tuwe wazalendo wa kula kwa urefu wa kamba.
 
Mmoja alinikamata nilikuwa napeleka gar morogoro gar haikuwa na Kosa akaomba tu nimsaidie 5000 ni mzee wa makamo ya 50,yrs
 
unapouliza swali kama askari wa Tz hawalipwi mishahara kama wanavyolipwa wa Kenya, una maanisha askari wa Kenya hawaombi wala kupokea rushwa?
 
Ukweli traffic na askari wengine pale Kibaha ni Kero ya aina fulani ambayo haijapata dawa
 
Kuna siku nilipigwa tochi nikiwa na gari na huku polisi yupo juu ya pikipiki anaendesha duh! Niliamanika nilijuwa namiminiwa risasi ile nacheki vizuri kumbe ilikuwa tochi.
 
Back
Top Bottom