Jeshi la polisi jijini Mwanza lasaka cd/dvd za uchochezi

Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
11,655
14,492
Akizungumza na waandishi wa habari,kamanda wapolisi jijini mwanza amewataka wote wenye cd hizo kuzisalimisha polisi,cd hizo ni pamoja na yenye jina Inuka chinja ule,na ile yenye kichwa BAKWATA NI TAWI LA KANISA,na pia wamedai kumsaka sheikh Illunga na wengine wanaohusika na cd hizo kwa tuhuma za uchochezi.
MY TAKE»inavyoonekana serikali mara zote inaogopa kuwawajibisha watuhumiwa wa upande mmoja hata kama kuna kila sababu ya kufanya hivyo,ni muda mrefu sana kumekuwepo na malalamiko hasa juu ya mkanda huo wa sheikh illunga,lakini serikali imekuwa ikitia pamba masikioni ama walikuwa wakisubiri kiongozi mwingine wa upande wa pili ajibu mapigo ili waweze kujiweka mbali na lawama au maandamano,kama ilivyokuwa kwa redio imani ambayo nayo ililaumiwa sana kwa uchochezi,lakini serikali hii sikivu iliendelea kupiga usingizi hadi pale radio neema ilipoinua sauti ndipo serikali ikaona kuwa ni wakati muafaka wa kuitolea uvivu kwa kuiunganisha na radio imaan,hivyo hii inatia shaka kuwa kama illunga asingepata mwenza,basi angeendelea tu kumwaga uchochezi wake bila tabu,hii ni aibu kwa serikali kuogopa wavunja sheria wake.
 
Kama huna cha kuposti sio lazima uposti,ni busara kunyamaza kuliko kuongea utumbo.Au unatumiwa nini.
 
Huko ndiko kuna watu wanaojaribu kurujesha amani kwa vitendo suala la uchochezi ni baya sana kuliko maandamano uchochezi ni process maandamano ni matokeo ya uchochezi. Utakuta polisi wanazuia maandamano bila kujua kiini cha maandamano. Tunamtaka Afande Kova aunganishe nguvu aungane na Kamanda Ernest Mango naye aanze msako wa CD DVD za uchochezi hapa Dar es Salaam.

Asante Kamanda Ernest Mango.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom