Jeshi la Polisi Jiji la Dodoma mjitathimini, mauaji kata ya Ihumwa na Mtumba yamezidi

tunene

Member
Mar 14, 2017
76
86
Ni muda mrefu sasa tangu mwaka Jana mpaka mpaka Sasa hivi.Hali ya amani sio shwari Kwa wakazi wa ihumwa , mtumba na mahoma.

Jinsia ya kike mabinti na akina mama ndio wahanga wakubwa wa mauaji haya. Jua likizama tu akina dada na mama zetu inawalazimu kubakia ndani kama wafungwa hata dukani au Kwa jirani wanaogopa kwenda. Ni kama vile Kuna kikundi Fulani Cha watu kinazunguka mitaani kinakamata wanawake wanabakwa ,kuuawa na kunyofolewa kizazi.

Wengine wakienda mashambani au kuokota Kuni huko huko wanabakwa na kuuawa na kutolewa kizazi.

Taarifa hizi za mauaji police mnazo lakini hatujaona juhudi zozote za kukomesha Hali hii.

Tunaomba Jeshi la Police Sasa liamuke lifatilie na kugundua nani wanahusika na matukio hayo ya kinyama
 
Back
Top Bottom