Jeshi la Polisi hivi mmejipima kweli au kujitafakari kutokana na wimbi la ajali barabarani?

musicarlito

Senior Member
Dec 29, 2020
176
289
Wasalaam

Kipindi kifupi cha nyuma, tulianza kusahau mambo ya ajali mbaya za barabarani kama mabasi yaliyokuwa yagharimu uhai na majeraha makubwa kama sio ulemavu kwa watanzania.

Kilifanyika nini sio rahisi kujua kiufundi lakini ni wazi kongole ziwaendee waliopewa kusimamia jukumu hilo yaani polisi kitengo cha usalama barabarani.

Mambo sio hivyo sasa, hali imekuwa mbaya, taarifa ya habari lazima na ajali iwemo, yaani ni kama nayo ni sehemu ya kipindi kama utabiri wa hali ya hewa...jana Njombe Coaster imegharimu maisha ya watu na majeraha,leo Singida...kesho hatujui.

Viongozi wenye dhamana wakati mwingine ni vyema kujipima kuona kama bado mnafaa kutumikia nafasi zenu hizi,labda wako watu wanaoweza kutusaidia kulikwepa hili

Hali imekuwa mbaya
 
Mkuu sijui kama uliiona clip inayoonesha lile coaster kugonga gari la mbele yake kisha kuhama upande wake na kwenda kugonga head on collision lile lori hio inahusian vipi na jeshi la polisi
Labda wawe wanawaendesha.
 
Wasalaam

Kipindi kifupi cha nyuma,tulianza kusahau mambo ya ajali mbaya za barabarani kama mabasi yaliyokuwa yagharimu uhai na majeraha makubwa kama sio ulemavu kwa watanzania

Kilifanyika nini sio rahisi kujua kiufundi lakini ni wazi kongole ziwaendee waliopewa kusimamia jukumu hilo yaani polisi kitengo cha usalama barabarani

Mambo sio hivyo sasa...hali imekua mbaya,taarifa ya habari lazima na ajali iwemo ,yaani ni kama nayo ni sehemu ya kipindi kama utabiri wa hali ya hewa...jana Njombe Coaster imegharimu maisha ya watu na majeraha,leo Singida...kesho hatujui...

Viongozi wenye dhamana wakati mwingine ni vyema kujipima kuona kama bado mnafaa kutumikia nafasi zenu hizi,labda wako watu wanaoweza kutusaidia kulikwepa hili

Hali imekua mbaya
Sasa mtu anayetakiwa kukemea kwa nguvu zote yupo kwenye tour ya royal.Huku wa kina Sirro hawana habari yeyote.Hakika Hali ni mbaya Sana.
 
Wasalaam

Kipindi kifupi cha nyuma,tulianza kusahau mambo ya ajali mbaya za barabarani kama mabasi yaliyokuwa yagharimu uhai na majeraha makubwa kama sio ulemavu kwa watanzania

Kilifanyika nini sio rahisi kujua kiufundi lakini ni wazi kongole ziwaendee waliopewa kusimamia jukumu hilo yaani polisi kitengo cha usalama barabarani

Mambo sio hivyo sasa...hali imekua mbaya,taarifa ya habari lazima na ajali iwemo ,yaani ni kama nayo ni sehemu ya kipindi kama utabiri wa hali ya hewa...jana Njombe Coaster imegharimu maisha ya watu na majeraha,leo Singida...kesho hatujui...

Viongozi wenye dhamana wakati mwingine ni vyema kujipima kuona kama bado mnafaa kutumikia nafasi zenu hizi,labda wako watu wanaoweza kutusaidia kulikwepa hili

Hali imekua mbaya
Usalama unanzia kwako mwenyewe

Ova
 
Mkuu sijui kama uliiona clip inayoonesha lile coaster kugonga gari la mbele yake kisha kuhama upande wake na kwenda kugonga head on collision lile lori hio inahusian vipi na jeshi la polisi
Asee kuna muda hapo tulisikia kuwa ajali ikitokea mkoa husika kamanda wa polisi angewajibika,askari walikua wengi barabarani na mizaha ilipungua ajali zikawa chache...huoni askari hawatimizi majukumu yao?
 
Wasalaam

Kipindi kifupi cha nyuma, tulianza kusahau mambo ya ajali mbaya za barabarani kama mabasi yaliyokuwa yagharimu uhai na majeraha makubwa kama sio ulemavu kwa watanzania.

Kilifanyika nini sio rahisi kujua kiufundi lakini ni wazi kongole ziwaendee waliopewa kusimamia jukumu hilo yaani polisi kitengo cha usalama barabarani.

Mambo sio hivyo sasa, hali imekuwa mbaya, taarifa ya habari lazima na ajali iwemo, yaani ni kama nayo ni sehemu ya kipindi kama utabiri wa hali ya hewa...jana Njombe Coaster imegharimu maisha ya watu na majeraha,leo Singida...kesho hatujui.

Viongozi wenye dhamana wakati mwingine ni vyema kujipima kuona kama bado mnafaa kutumikia nafasi zenu hizi,labda wako watu wanaoweza kutusaidia kulikwepa hili

Hali imekuwa mbaya
Matatizo yanaweza kuwa mengi yakichangiwa na sisi madereva wenyewe , miundo mbinu kama vile barabara mbovu, kutokuwa na taa za barabarani , magari mabovu n.k. Lakini wenzetu wa kikosi cha barabarani na wao kwa kisai fulani wanaweza kuwa nao ni chanzo kwa sababu kwa sasa wamekuwa wanafanya kazi kwa kuvizia yaani ni kama wanasubiria kosa ndiyo wafanye kazi ya kukuandikia badala ya kutengeneza mazingira ya kuelimisha au kukaa mahali waonekani ili mtu aogope fanya makosa.Utakuta anatoka kichakani kama chui anawinda kuwahi simamisha gari sasa unajiuliza ukisimama na mwendo ulionao haoni kama unaweza sababisha ajali? Unakuta wakati mwingine gari hasa mabasi sijui ni marafiki zao wanafanya makosa lakini wala hawahangaiki wao ni kupambana na kirukuu na gari ndogo.Hebu tuangalie breakdown zilivyo na ubovu lakini hawazikamati kwa nini? Ajali ya Njombe kweli ni dereva wa Coaster ndiyo chanzo cha ajali alitaka pita magari mengine bila kutazama vizuri mbele.
 
Back
Top Bottom