Jeshi la Polisi halina msaada ukiripoti kutishiwa maisha

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,463
40,963
Imesikika kauli eti ya kamanda wa Kanda Maalum ya Dar, ikimtaka Askofu Mwingira aripoti haraka makao makuu ya polisi kwa mahojiano juu ya kauli ya Askofu huyo kutamka kuwa mara kadhaa alinusurika kuuawa na watu wa Serikali.

Sijui wanaenda kumhoji ili wafanye nini. Na kama alinusurika kuuawa na watu wa Serikali, sijui polisi watafanya nini.

Tundu Lissu, kabla ya kushambuliwa kwa risasi, alikuwa ameripoti polisi mara 2 kuhusiana na watu walioonekana kuwa na dhamira mbaya, waliokuwa wakimfuatilia kila mahali. Baada ya Tundu Lissu kutoa taarifa hiyo kwa Jeshi la Polisi, kwani Polisi walifanya nini? Hata baada ya Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi, Polisi walifanya nini? Kuna watu wangapi wamepotezwa, wameuawa, taarifa zimetolewa Polisi, Jeshi la Polisi wamefanya nini?

Wananchi tunajua, ukiona mtu amepotea au ameuawa, umetoa taarifa Polisi, hakuna kinachofanyika, basi uovu huo umehusisha vyombo vya Serikali.

Kama Askofu, Mwingira alijua kabisa kuwa wanaomtafuta kumfanyia uovu ni watu wa Serikali, taarifa hizo angezipeleka wapi wakati uovu dhidi ya watu ambao ama Serikali au viongozi wa Serikali hawawataki, huhusisha jeshi hilo hilo la Polisi?

Hivi kutoweka kwa Lijenje, utaenda kuripoti kwa Kingai, Goodluck, Jumanne au Mahita?

Leo hii, kama nchi, tupo kwenye mazingira ya hovyo kabisa. Mtu akipotea, watu wanauliza kama aliyepotea ni wa chama gani, kama ni kiongozi wa chama cha upinzani, kama amewahi kumkosoa kiongozi wa Serikali au Serikali, na jibu likiwa ndiyo, watu huwa wamejihakikisha kwa zaidi ya 99% kuwa uovu huo utakuwa umefanywa na vyombo vya Serikali. Huo ndio ukweli wenyewe.
 
Maswali MAGUMU SANA kwa JESHI LETU
1.Nani alimteka MO
2.Nani alimpiga Risasi Tundu Lissu
3.Nani alimpiga Risasi na Kumuua Akwilina
4.Ben saa 8 yupo wapi
5.Azory yupo wapi
6. Miili iliyokutwa kwenye viroba ufukweni ilikuwa ya watu gani, waliuliwa na nani na uchunguzi umefikia wapi?
 
Maswali MAGUMU SANA kwa JESHI LETU
1.Nani alimteka MO
2.Nani alimpiga Risasi Tundu Lissu
3.Nani alimpiga Risasi na Kumuua Akwilina
4.Ben saa 8 yupo wapi
5.Azory yupo wapi
Wanashimdwa kuyajibu haya, wanamparamia Askofu Mwingira aliyeamua kuwaeleza watanzania yanayomsibu kuliko kwenda kimya kimya kuwaeleza polisi ambao anajua hawatafanya lolote maana ndio wahalifu wenyewe.
 
6. Miili iliyokutwa kwenye viroba ufukweni ilikuwa ya watu gani, waliuliwa na nani na uchunguzi umefikia wapi?
Tena miili ya kwenye viroba, Mwigulu pia anahusika. Tena alitoa kauli ya wazi eti ni miili ya wahamiaji haramu wa kisomali. Yawezekana alikuwepo wakati wakiuawa.
 
Back
Top Bottom