Jeshi la Polisi Dar, limewaua majambazi watatu na kukamata silaha mbili aina ya Shotgun Pump Action na Bastola aina ya Browning

Tunaomba picha za ubavuni za gari, haiwezekani gari ishambuliwe kwa risasi halafu ibaki mpya kiasi hicho!

Majambazi hayo yalianza kurusha risasi hovyo ilihali yalikuwa yanajua kabisa yana risasi chache, risasi 4 ndani ya 12bore pump action na 4 ndani ya pistol halafu yachezee risasi hovyo?

Hilo jambazi moja lilikimbia vipi mashambulizi yakiwa yanaendelea kwenye gari
Lugha ya polisi boss..
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewaua majambazi watatu na kukamata silaha mbili aina ya Short Gun Pump Action na Bastola aina ya Browning.

Mnamo tarehe 26.07.2020 majira ya saa mbili usiku Jeshi la Polisi Kanda Maalum lilipata taarifa kuwa huko maeneo ya Mbagala Chamanzi kuna gari lenye namba T 855 ATE aina ya Nissan X-Trail likiwa na watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa katika harakati za kufanya uhalifu.

Baada ya kupata taarifa hizo kikosi kazi cha kupambana na ujambazi kiliweka mtego katika eneo hilo na baada majambazi hao kuhisi wanafuatiliwa na Polisi ghafla walianza kupiga risasi hovyo kwa hofu na ndipo askari wakaamua kujibu mapigo kwa kulishambulia gari la majambazi hao na kufanikiwa kuwaua papo hapo majambazi watatu na jambazi mmoja akafanikiwa kukimbia.

View attachment 1521443

Askari walifanya upekuzi ndani ya gari la majambazi hao na kumkuta jambazi mmoja akiwa amevalia mavazi ya Jeshi la Polisi aina ya kombati za kijani (JUNGLE GREEN) na kofia aina ya bareti nyeusi ya Jeshi la Polisi, redio Call, Pingu, namba za gari T 832 DCW ambazo ndiyo namba halisi za usajili wa gari hilo na silaha mbili aina ya Short gun Pump Action ikiwa na risasi nne ndani ya magazine iliyofutwa namba na Bastola aina ya Browning iliyofutwa namba ikiwa na risasi nne ndani ya Magazine

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa majambazi hao walifanya matukio ya uhalifu Mkoa wa Pwani Wilaya ya Mkuranga maeneo ya Vikindu na Kisemvule ambapo mnamo tarehe 25/07/2020 majira ya saa mbili usiku majambazi hao walimteka na kumpora mfanyabiashara wa UWAKALA wa Benki na Mitandao ya simu aliyefahamika kwa jina la SALEHE MASOUD kiasi cha Tsh 19,600,000/= .

POLISI KANDA MAALUM KUIMARISHA ULINZI SIKUKUU YA EID EL-HAJJI.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi na usalama katika kipindi cha sikukuu ya Eid El-Hajji inayotarajiwa kuadhimishwa tarehe 31/07/2020.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawaasa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kusherehekea sikukuu kwa amani na utulivu na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa sheria kwani tumejipanga kuimarisha doria maeneo yote muhimu zikiwemo nyumba za Ibada, fukwe za bahari na tunawatadharisha watembea kwa miguu na madereva wa vyombo vya moto kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani.

Aidha Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawaomba Wananchi wa Dar es Salaam kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu kwani jukumu la kuzuia uhalifu ni la kila Mtanzania.

SACP- LAZARO B. MAMBOSASA,

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM,

DAR ES SALAAM.

30/07/2020.

"Walikuwa wanapambana ndipo wakafanikiwa kuua majambazi watatu"

Futuhiiiiiii Ndio Ni FUtuhiii.
 
Tunaomba picha za ubavuni za gari, haiwezekani gari ishambuliwe kwa risasi halafu ibaki mpya kiasi hicho!

Majambazi hayo yalianza kurusha risasi hovyo ilihali yalikuwa yanajua kabisa yana risasi chache, risasi 4 ndani ya 12bore pump action na 4 ndani ya pistol halafu yachezee risasi hovyo?

Hilo jambazi moja lilikimbia vipi mashambulizi yakiwa yanaendelea kwenye gari
Inabidi Polisi wabadili style yao ya kuua majambazi huwa wanawakamata na kuwapeleka misituni na kuwaua kisha wanakuja kuleta FUTUHI zao.
 
Watanzania sio wajinga!
Kama wewe ni mkweli tuambie

1. kuwa hakuna mtu aliyeuawawa na polisi
2. Waliouawawa ni Wanaharakati wa Maendeleo na Wazalendo wa nchi

Nenda central akapate ushahidi uje kutujuza
La sivyo sisi watanzania wajinga wewe ni kiongozi wetu
 
Mkuu umewahi kuwaona wakirushiana live au huwa ni historia? acha watu wakamatwe wapelekwe mahakamani
Siku hao wakora wakufikie na kukutoa marinda ndio utapeleka ushahidi mahakamani na madaktari waingiza kuangalia ukweli wako. Kuwa mpole
 
Kazi nzuri hongera kwa jeshi la police Tanzania
Kazi nzuri kuua?Wangestahili hongera endapo wangewakamata wakiwa hai.Jambazi anastahili kuishi,kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria(Mahakama).
 
Tunaomba picha za ubavuni za gari, haiwezekani gari ishambuliwe kwa risasi halafu ibaki mpya kiasi hicho!

Majambazi hayo yalianza kurusha risasi hovyo ilihali yalikuwa yanajua kabisa yana risasi chache, risasi 4 ndani ya 12bore pump action na 4 ndani ya pistol halafu yachezee risasi hovyo?

Hilo jambazi moja lilikimbia vipi mashambulizi yakiwa yanaendelea kwenye gari
Nalo neno!
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewaua majambazi watatu na kukamata silaha mbili aina ya Short Gun Pump Action na Bastola aina ya Browning.

Mnamo tarehe 26.07.2020 majira ya saa mbili usiku Jeshi la Polisi Kanda Maalum lilipata taarifa kuwa huko maeneo ya Mbagala Chamanzi kuna gari lenye namba T 855 ATE aina ya Nissan X-Trail likiwa na watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa katika harakati za kufanya uhalifu.

Baada ya kupata taarifa hizo kikosi kazi cha kupambana na ujambazi kiliweka mtego katika eneo hilo na baada majambazi hao kuhisi wanafuatiliwa na Polisi ghafla walianza kupiga risasi hovyo kwa hofu na ndipo askari wakaamua kujibu mapigo kwa kulishambulia gari la majambazi hao na kufanikiwa kuwaua papo hapo majambazi watatu na jambazi mmoja akafanikiwa kukimbia.

View attachment 1521443

Askari walifanya upekuzi ndani ya gari la majambazi hao na kumkuta jambazi mmoja akiwa amevalia mavazi ya Jeshi la Polisi aina ya kombati za kijani (JUNGLE GREEN) na kofia aina ya bareti nyeusi ya Jeshi la Polisi, redio Call, Pingu, namba za gari T 832 DCW ambazo ndiyo namba halisi za usajili wa gari hilo na silaha mbili aina ya Short gun Pump Action ikiwa na risasi nne ndani ya magazine iliyofutwa namba na Bastola aina ya Browning iliyofutwa namba ikiwa na risasi nne ndani ya Magazine

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa majambazi hao walifanya matukio ya uhalifu Mkoa wa Pwani Wilaya ya Mkuranga maeneo ya Vikindu na Kisemvule ambapo mnamo tarehe 25/07/2020 majira ya saa mbili usiku majambazi hao walimteka na kumpora mfanyabiashara wa UWAKALA wa Benki na Mitandao ya simu aliyefahamika kwa jina la SALEHE MASOUD kiasi cha Tsh 19,600,000/= .

POLISI KANDA MAALUM KUIMARISHA ULINZI SIKUKUU YA EID EL-HAJJI.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi na usalama katika kipindi cha sikukuu ya Eid El-Hajji inayotarajiwa kuadhimishwa tarehe 31/07/2020.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawaasa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kusherehekea sikukuu kwa amani na utulivu na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa sheria kwani tumejipanga kuimarisha doria maeneo yote muhimu zikiwemo nyumba za Ibada, fukwe za bahari na tunawatadharisha watembea kwa miguu na madereva wa vyombo vya moto kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani.

Aidha Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawaomba Wananchi wa Dar es Salaam kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu kwani jukumu la kuzuia uhalifu ni la kila Mtanzania.

SACP- LAZARO B. MAMBOSASA,

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM,

DAR ES SALAAM.

30/07/2020.
Hayo maelezo ya polisi huwa ni ya ku copy na ku paste kwa kila mauaji wanayofanya
 
Back
Top Bottom