Jeshi la Polisi Dar, limewaua majambazi watatu na kukamata silaha mbili aina ya Shotgun Pump Action na Bastola aina ya Browning

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewaua majambazi watatu na kukamata silaha mbili aina ya Short Gun Pump Action na Bastola aina ya Browning.

Mnamo tarehe 26.07.2020 majira ya saa mbili usiku Jeshi la Polisi Kanda Maalum lilipata taarifa kuwa huko maeneo ya Mbagala Chamanzi kuna gari lenye namba T 855 ATE aina ya Nissan X-Trail likiwa na watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa katika harakati za kufanya uhalifu.

Baada ya kupata taarifa hizo kikosi kazi cha kupambana na ujambazi kiliweka mtego katika eneo hilo na baada majambazi hao kuhisi wanafuatiliwa na Polisi ghafla walianza kupiga risasi hovyo kwa hofu na ndipo askari wakaamua kujibu mapigo kwa kulishambulia gari la majambazi hao na kufanikiwa kuwaua papo hapo majambazi watatu na jambazi mmoja akafanikiwa kukimbia.

1596109145626.png

Askari walifanya upekuzi ndani ya gari la majambazi hao na kumkuta jambazi mmoja akiwa amevalia mavazi ya Jeshi la Polisi aina ya kombati za kijani (JUNGLE GREEN) na kofia aina ya bareti nyeusi ya Jeshi la Polisi, redio Call, Pingu, namba za gari T 832 DCW ambazo ndiyo namba halisi za usajili wa gari hilo na silaha mbili aina ya Short gun Pump Action ikiwa na risasi nne ndani ya magazine iliyofutwa namba na Bastola aina ya Browning iliyofutwa namba ikiwa na risasi nne ndani ya Magazine

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa majambazi hao walifanya matukio ya uhalifu Mkoa wa Pwani Wilaya ya Mkuranga maeneo ya Vikindu na Kisemvule ambapo mnamo tarehe 25/07/2020 majira ya saa mbili usiku majambazi hao walimteka na kumpora mfanyabiashara wa UWAKALA wa Benki na Mitandao ya simu aliyefahamika kwa jina la SALEHE MASOUD kiasi cha Tsh 19,600,000/= .

POLISI KANDA MAALUM KUIMARISHA ULINZI SIKUKUU YA EID EL-HAJJI.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi na usalama katika kipindi cha sikukuu ya Eid El-Hajji inayotarajiwa kuadhimishwa tarehe 31/07/2020.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawaasa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kusherehekea sikukuu kwa amani na utulivu na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa sheria kwani tumejipanga kuimarisha doria maeneo yote muhimu zikiwemo nyumba za Ibada, fukwe za bahari na tunawatadharisha watembea kwa miguu na madereva wa vyombo vya moto kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani.

Aidha Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawaomba Wananchi wa Dar es Salaam kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu kwani jukumu la kuzuia uhalifu ni la kila Mtanzania.

SACP- LAZARO B. MAMBOSASA,

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM,

DAR ES SALAAM.

30/07/2020.
 
Tunaomba picha za ubavuni za gari, haiwezekani gari ishambuliwe kwa risasi halafu ibaki mpya kiasi hicho!

Majambazi hayo yalianza kurusha risasi hovyo ilihali yalikuwa yanajua kabisa yana risasi chache, risasi 4 ndani ya 12bore pump action na 4 ndani ya pistol halafu yachezee risasi hovyo?

Hilo jambazi moja lilikimbia vipi mashambulizi yakiwa yanaendelea kwenye gari
 
Mkuu Gari liko central unaweza kwenda kulikagua
Kwa ufanisi zaidi

Ova
 
Aisee! Gari haina hata tundu moja la risasi!!
Umeona picha ya pande zote za gari?

Je, umepata uhakika kama hawakuteremka kwenye gari ndipo wakaanza kurushiana risasi?

Swali lako bado la msingi sana linahitaji majibu toka kwa wahusika.
 
Tunaomba picha za ubavuni za gari, haiwezekani gari ishambuliwe kwa risasi halafu ibaki mpya kiasi hicho!

Majambazi hayo yalianza kurusha risasi hovyo ilihali yalikuwa yanajua kabisa yana risasi chache, risasi 4 ndani ya 12bore pump action na 4 ndani ya pistol halafu yachezee risasi hovyo?

Hilo jambazi moja lilikimbia vipi mashambulizi yakiwa yanaendelea kwenye gari
Ha ha ha hawa watengenezaji wa hizi movie sijui hawajiulizagi haya maswali..
 
Tunaomba picha za ubavuni za gari, haiwezekani gari ishambuliwe kwa risasi halafu ibaki mpya kiasi hicho!

Majambazi hayo yalianza kurusha risasi hovyo ilihali yalikuwa yanajua kabisa yana risasi chache, risasi 4 ndani ya 12bore pump action na 4 ndani ya pistol halafu yachezee risasi hovyo?

Hilo jambazi moja lilikimbia vipi mashambulizi yakiwa yanaendelea kwenye gari
kumbuka hizo ndizo walizokutwa nazo Mkuu
 
Watanzania sio wajinga!
 
kumbuka hizo ndizo walizokutwa nazo Mkuu
Kuna tukio lilitokea pia arusha, "arapisii" akiwa ni yule kada wa fisiem alohamishiwa chuoni moshi,tukaambiwa kulikuwa na stand off ya takribani masaa mawili au matatu wakirushiana risasi makaka jambazi na polis, lakin kwenye taarifa tukaambiwa eneo la tukio yaliokotwa maganda ya risasi yasiyozidi 12, sasa unajiuliza kwa muda wa masaa mawili au matatu hiyo stand off ndo zilirushwa risasi 12 tu kutoka kwa majambazi??

Huyo mambosasa ni empty head kabisa! Toka aseme risasi ilikata kona ikamuua akwilina huwa simtofautishi na pimbi
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewaua majambazi watatu na kukamata silaha mbili aina ya Short Gun Pump Action na Bastola aina ya Browning.

Mnamo tarehe 26.07.2020 majira ya saa mbili usiku Jeshi la Polisi Kanda Maalum lilipata taarifa kuwa huko maeneo ya Mbagala Chamanzi kuna gari lenye namba T 855 ATE aina ya Nissan X-Trail likiwa na watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa katika harakati za kufanya uhalifu.

Baada ya kupata taarifa hizo kikosi kazi cha kupambana na ujambazi kiliweka mtego katika eneo hilo na baada majambazi hao kuhisi wanafuatiliwa na Polisi ghafla walianza kupiga risasi hovyo kwa hofu na ndipo askari wakaamua kujibu mapigo kwa kulishambulia gari la majambazi hao na kufanikiwa kuwaua papo hapo majambazi watatu na jambazi mmoja akafanikiwa kukimbia.
View attachment 1521443
Askari walifanya upekuzi ndani ya gari la majambazi hao na kumkuta jambazi mmoja akiwa amevalia mavazi ya Jeshi la Polisi aina ya kombati za kijani (JUNGLE GREEN) na kofia aina ya bareti nyeusi ya Jeshi la Polisi, redio Call, Pingu, namba za gari T 832 DCW ambazo ndiyo namba halisi za usajili wa gari hilo na silaha mbili aina ya Short gun Pump Action ikiwa na risasi nne ndani ya magazine iliyofutwa namba na Bastola aina ya Browning iliyofutwa namba ikiwa na risasi nne ndani ya Magazine

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa majambazi hao walifanya matukio ya uhalifu Mkoa wa Pwani Wilaya ya Mkuranga maeneo ya Vikindu na Kisemvule ambapo mnamo tarehe 25/07/2020 majira ya saa mbili usiku majambazi hao walimteka na kumpora mfanyabiashara wa UWAKALA wa Benki na Mitandao ya simu aliyefahamika kwa jina la SALEHE MASOUD kiasi cha Tsh 19,600,000/= .

POLISI KANDA MAALUM KUIMARISHA ULINZI SIKUKUU YA EID EL-HAJJI.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi na usalama katika kipindi cha sikukuu ya Eid El-Hajji inayotarajiwa kuadhimishwa tarehe 31/07/2020.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawaasa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kusherehekea sikukuu kwa amani na utulivu na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa sheria kwani tumejipanga kuimarisha doria maeneo yote muhimu zikiwemo nyumba za Ibada, fukwe za bahari na tunawatadharisha watembea kwa miguu na madereva wa vyombo vya moto kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani.

Aidha Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawaomba Wananchi wa Dar es Salaam kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu kwani jukumu la kuzuia uhalifu ni la kila Mtanzania.

SACP- LAZARO B. MAMBOSASA,

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM,

DAR ES SALAAM.

30/07/2020.
Kwanini wasikamatwe wakafikishwa mahakamani?
 
Tunaomba picha za ubavuni za gari, haiwezekani gari ishambuliwe kwa risasi halafu ibaki mpya kiasi hicho!

Majambazi hayo yalianza kurusha risasi hovyo ilihali yalikuwa yanajua kabisa yana risasi chache, risasi 4 ndani ya 12bore pump action na 4 ndani ya pistol halafu yachezee risasi hovyo?

Hilo jambazi moja lilikimbia vipi mashambulizi yakiwa yanaendelea kwenye gari
Zinatakiwa ziwe risasi ngap ndio waanze kuchezea?
 
Back
Top Bottom