Jeshi la polisi Dar lawanasa raia wa Uganda na pembe za Ndovu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
SAM_1599-620x308.jpeg
SAM_1599-620x308.jpeg

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Saalam limewakamata watu wawili Raia wa Uganda wakiwa na pembe 660 za Ndovu pamoja na mashine ya kukatia pembe hizo.

Simon Siro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amewaeleza waandishi kuwa, watuhumiwa hao ni Juma Saidi (54) na Ally Sharif (26) wamekamatwa Kimara jijini Dar es Salaam.

Kutokana watuhumiwa hao na wengine mbalimbali kukamatwa wakiwa katika nyumba za kupanga Kamanda Siro amesema ili kuwepo kwa usalama, wamiliki wa nyumba za kupanga waendeleze zoezi la kuwa na picha za wapangaji wao.

“Nafikiri mnakumbuka niliwaambia ili tuwe salama watanzania, unayempangisha hakikisha kwamba unaweka picha yake hiyo itatusaidia kumtafuta na kumkamata pindi anapofanya tukio,”amesema.

Kamanda Siro amesema upelelezi bado unaendelea ili kubalini mtandao mzima wanaoshirikiana nao kufanya uhalifu wa kuua na kuchukua pembe za ndovu.

“Tutahakikisha wanatueleza mtandao wanaoutumia na kisha tutawafikisha mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili,”amesema.
 
View attachment 360801 View attachment 360801

Hivi ni kwanini serikali ya tanzania imekataa kuteketeza hizo pembe za ndovu zinazokamatwa?kuna nini nyuma ya pazia?
 
Back
Top Bottom