Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,188
- 4,100
Jeshi la polisi kanda maaluum ya Dar es salaam linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kuhusu Ugonjwa unaoenezwa na virusi vya korona.
Watuhumiwa hao ni Boniphac Elias Mwita umri miaka 29 mkazi wa Tabata na Rosemary Elias Mwita mke wa mshtakiwa wa kwanza umri ni miaka 41 nae ni mkazi wa Tabata.
Jeshi la polisi linasema kuwa mnamo tarehe 20/03/2020 majira ya saa saba mchana watuhumiwa hao wakiwa kwenye daladala yenye namba za usajili namba T.119 DKS wakitokea Tabata kuelekea hospitali ya Taifa Muhimbili walisambaza taarifa za uongo kuhusiana na habari za ugonjwa wa COVID19 maarufu kama korona.
Watuhumiwa hao walianza kukejeli huku wakitania kuwa serikali inapotosha wananchi kuwa kuna virusi vya korona na pia serikali haina fedha kwa ajili ya kulisha wanafunzi ndio maana shule na vyuo zimefungwa kwa kisingizio cha kuwepo kwa ugonjwa wa korona na kwamba serikali inafanya hivi kwa kwa ajili ya kuomba msaada wa fedha kutoka mataifa mbalimbali.
Jambo hili kulingana na hali halisi iliyopo nchini liliwakera abiria wengine na kuamua kuwaweka chini ya ulinzi watuhumiwa hao na kumwelekeza dereva apeleke gari kituoni, walipofika kituoni walikamatwa upya na ndipo wanapoendelea kushikilia mpaka hivi sasa. Ambapo jarada limeshaandaliwa na upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika na watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
Jeshi la polisi linatoa rai na onyo kwa watanzania wengine ambao wanaleta mzaha na kejeli kwa ugonjwa huu ambao kimsingi unaangamiza watu duniani na Tanzania ikiwa ni sehemu ya dunia hiyo, lazima kila mmoja aendelee kupokea maagizo kutoka kwa viongozi na serikali. Maana si jambo la kuchukilia mzaha kwa kuwa ugonjwa huu unaendelea kuchua maisha ya watu, hivyo watu waendelee kufuata maelekezo ili tuweze kuepuka balaa hili.