Jeshi la Polisi chini ya IGP Sirro kuogopa kuwahoji wahalifu wa CCM, je wamepoteza weledi?

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,364
2,000
Heshima kwenu wakuu,

Kwanza niwapongeze TAKUKURU na taasisi ya Kupambana na dawa za kulevya kwa kuweza kutenda kazi zao bila kujali chama cha mtu wala cheo chake.

Japo TAKUKURU wamekuwa wakipokea Maagizo kutoka juu, lakini wanaonesha japo nia ya kifanya kazi wasipoingiliwa. Mfano Wapokea waliokuwa wanahusika na kununua Madiwani, Nasssri alipeleka ushahidi lakini ukaharibiwa. Tunaelewa.

Taasisi ya kupambana na dawa za kulevya hadi sasa sina la kuwalaumu kwani wanafanya kazi nzuri kabisa.

Ila jeshi la Polisi wameshindwa kujipambanua kwenye ukada wa chama tawala. Hii ni changamoto kwao..

Mfano: Kuna Mbunge wa CCM anaitwa Dr. Godwin Mollel wa Jimbo la Siha, alisema mbele ya Umma kwamba ana Video za watu waliomshambulia kwa risasi Tundu Lissu. Aliyasema hayo 8/2/2019, lakini hadi leo 15/2/2019 Polisi wameshindwa kwenda kuuchukua huo ushahidi. Japo hata kumhoji tu wameshindwa.


Case closed: Mbunge Mollel adai ana ushahidi wa Chadema kuhusika issue ya Lissu - JamiiForums

Hapo ndo wasiwasi wangu ulipo.

Kuna kada wa CCM alimtishia kumuua Ben Saanane na Ben Saanane akapotea kweli. Ila alikuwa kashatoa namba ya simu ya wanaomtishia kituo cha Polisi, lakini hadi leo hakina aliyehojiwa..
Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali - JamiiForums

Kuna waliomuua Mwenyekiti wa CHADEMA Geita Alfonce Mawazo, pamoja kwamba wanajulikana lakini hakuna aliyekamatwa.

Kinachoniuma zaidi, Tundu Lissu, Ben Saanane na Alphonce Mawazo ni Wanachama wenzangu wa JamiiForums.

Kwa hali hii Polisi wataaminikaje?

Je, CCM wanayoyafanya, wafuasi wa vyama vingine wanashindwa kuyafanya?

Polisi inabidi wajitafakari kwa hili..

Polisi wanabambikia watu kesi, wengi wanaobambikiwa kesi ni vyama vya Upinzani. Hili nakumbuka hata rais alishawaonya.

Jaji Kiongozi:Askari Polisi wanabambika raia kesi - JamiiForums
Ninayo mengi ya kuongea.. Ila nawaogopa Polisi sababu wana bunduki. Lakini wangekuwa wanakubali kuweka bunduki chini tukabishana kwa hoja, wangekimbia kwa aibu.
TANZIA: Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro - JamiiForums
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
1,885
2,000
Siku utakayoshuhudia kuwa nafasi hii ya IGP watarajiwa wanaomba na kufanyia interview ,ndio wakati wa wewe kuja na hoja murua kama hii,but for now endelea kusubiri na kuisoma namba.
 

Essien jr

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
585
1,000
Kwa hiyo mifano yako mitatu ndio umeshaconclude Jeshi la polisi halifanyi kazi??
Kwa uzeee wako kazi zinazofanywa na polisi Ni zipi km kulinda na kufanya uchunguzii juu ya matukio yanayohatarisha aman ya nchi hawaziwezii. Unazani kazi zao Ni kuiba masanduku ya kula?, kuvamia na kuua kina Akwirina???
 

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,736
2,000
Jeshi la polisi limepoteza mwelekeo, mi nishajikatia tamaa toka jamaa alipotuonyesha sisitivii za mobile phone, ni kajua limeingiliwa na usanii. Sasa hivi nikimuona Mambosasa anaongea najua hiyo ishu ni magumashi. Kwa mfano utakumbuka ishu ya akwilina yeye ndo alikuwa kinara wa uongo eti risasi inaenda inapinda kona inaingia kwenye basi inapiga mtu. Issue ya Mo ni Mambosasa huyu huyu alilimaliza kwa usanii. Kwa ujumla linakatisha tamaa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom