GwaB
JF-Expert Member
- Mar 19, 2014
- 4,015
- 5,397
Kwa mara nyingine tena katika kipindi kifupi sana tumeshuhudia mauaji ya askali polisi wakiwa katika majukumu yao ya kulinda wananchi na mali zao. Kitendo kilichofanywa na hawa watu ambao hadi leo bado haijafahamika kama ni magaidi au majambazi tu hakipaswi kufumbiwa macho kwani wanaouawa ni ndugu zetu.
Naamini kabisa askali wetu wamepitia mafunzo kabla ya kuhitimu kuwa walinzi wa usalama,lakini tukumbuke pia kuwa adui nae amepitia mafunzo yale yale na pengine kupita yale yanayotolewa na majeshi yetu hivyo ni vizuri sana kuanzia sasa tukachukua tahadhari kwa kuwapa askali wetu vitendea kazi imara ambavyo vinawahakikishia usalama wao pale wanaposhambuliwa.
Kuvaa fulana za kuzuia risasi na kufanya patrol kwa magari ya wazi kama Defender na zile Toyota kwa kweli kabisa ni kuwaweka wale vijana kama target na hii haiwezi kuvumilika tena.
Serikali iamue kwa dhati sasa kununua magari ya deraya ambayo ndio hasa yanayotakiwa kutumika katika patrol na kuingia kwenye mapambano. Ieleweke wazi kuwa kuna watu wanaojua kutumia silaha vile vile kama polisi lakini hawako jeshini,watu hawa wakivurugwa kimaisha wakageukia kufanya uharifu matokeo yake ni haya ya kujikuta Polisi wetu wakiingia kwenye mtego kama huu tulioushuhudia wiki iliyopita. Tuongeze tahadhari na mungu aziweke roho za marehemu mahala pema peponi.
Magari ya aina hii sasa yanatakiwa kutumika na jeshi la Polisi, naamini hili linatekelezeka.