Jeshi la Mgambo; kwa sheria ipi wanaongozwa?

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,530
NImeona hii picha ninayoambatanisha hapa chini, nikajiuliza, ni mamlaka gani na sheria zipi ambazo zinawapa mgambo nguvu kama polisi?

7572.JPG

[SIZE=-2]Mgambo wa Manispaa ya Ilala, wakimpeleka Kituo Kidogo cha Polisi Kisutu, Dar es Salaam, mkazi wa Jiji ambaye walimkamata kwa kukasirishwa na kitendo cha kumsaidia mchuuzi aliyekuwa akinyang'anywa toroli lililokuwa limesheheni machungwa aliyokuwa akiuza katikati ya Jiji jana. (Picha na Richard Mwaikenda) [/SIZE]
 
Mgambo ni hatari kwa usalama wa nchi

Makala

Rai
13.03.2008
na siyovelwa hussein


ZAMANI tulikuwa tukihadithiwa, nadhani yalikuwa ni masihara, kwamba Tanzania haikuwahi kushambuliwa na majeshi ya makaburu wa Afrika Kusini kwa sababu ya Jeshi letu la Mgambo.

Kwamba makaburu walikuwa wakikerwa sana na jinsi Tanzania ilivyokuwa ikiwasaidia wapigania uhuru wa nchi mbalimbali za kusini mwa Afrika, kama Msumbiji, Angola, Namibia pamoja na vyama vya wapigania uhuru vya ndani ya Afrika Kusini kwenyewe kama ANC na PAC.

Ikasemwa kwamba kama ilivyokuwa ikiyashambulia makambi ya wapigania uhuru katika nchi mbalimbali, ilikuwa ikijua wazi kwamba Tanzania ndio kuna kambi na ofisi nyingi zaidi na hivyo kila siku dhamira yao ilikuwa kuharibu mtandao huo wa wapigania uhuru katika Tanzania. Hata hivyo, kikwazo kikubwa kwao inasemwa kilikuwa shaka juu ya nguvu, nidhamu na ujasiri wa Jeshi la Mgambo ambalo kwao lilikuwa kitisho kikuu.

Sababu yake ni kwamba eti kwa maendeleo yao ya teknolojia ya kijeshi walishaweza kuziona (kuzi target) kambi na vituo vyote vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wakaviona vituo vyote vya polisi, magereza na kila chombo cha dola kilichopo Tanzania.

Kikwazo kikawa maskani ya Jeshi la Mgambo. Kwa woga wao wakaamini kwamba pengine kambi za mgambo zimejengwa kwa teknolojia ya hali ya juu kiasi kwamba haziwezi kupatikana katika viona mbali vyao.

Kichekesho zaidi kikaletwa na woga waliojitia juu ya nidhamu na ujasiri wa jeshi hilo . Pamoja na kutoona maskani zao kilichowatisha zaidi kilikuwa ni jinsi walivyoweza kufanya kazi kwa ufanisi katika mazingira magumu na ya hatari. Enzi zile jeshi la mgambo lilikuwa chombo kilichotupwa zaidi kuliko vyote vya Serikali.

Kaburu akashangaa inawezekanaje askari huyu anayetegemea kirungu pekee huku hata sare zake zikiwa zimeraruka ovyo anaweza kuwa na ari ya kupambana katika changamoto ambazo kwa vyovyote zilihitaji askari anayepata motisha wa kutosha?

Hili likamkwaza Kaburu kiasi, pamoja na kujua kwa undani kabisa kwamba Tanzania inaratibu hujuma na mapambano dhidi ya utawala wao, walibaki kimya wakitafuta jinsi ya kulielewa vya kutosha Jeshi la Mgambo la Tanzania.

Kwa bahati mpaka mabadiliko ya kisiasa yanatokea Afrika Kusini bado walikuwa hawajalielewa jeshi hilo na hivyo kuifanya Tanzania iwe nchi pekee iliyokuwa ikijishughulisha na ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika ambayo haikuwahi kupata msukosuko wa moja kwa moja wa maguvu ya makaburu wa Afrika Kusini.

Kama kilikuwa kichekesho basi kiliishia hapo, lakini sasa imekuja dhana nyingine ambayo inahitaji umakini mkubwa kutoka katika Serikali yetu ili kudhibiti utendaji wa Jeshi la Mgambo.

Kama hapo nyuma walifanya kazi ya ziada kuihakikishia Tanzania usalama angalau kutokana na woga wa makaburu, sasa lina hatari kubwa ya kutubomolea usalama wetu kwa jinsi utendaji wa askari wake unavyokuwa adha kwa wananchi.

Haiwezekani kusema kwamba Serikali ya Tanzania inaanza kuonyesha woga kwa Jeshi la Mgambo kama ilivyokuwa Serikali ya Makaburu wa Afrika Kusini, lakini nina hakika Serikali inaona jinsi utendaji wa askari wa jeshi hilo unavyokiuka haki za binadamu na hata sheria za nchi, hasa mijini, lakini hakuna tamko linalotoka kukemea wala kuelekeza utendaji sahihi.

Matokeo yake hatari ya kuwashawishi wananchi kujilinda au kufanya visasi inazidi kuongezeka kadiri wanavyodhani Serikali Kuu kupitia vyombo vyake vya dola imeshindwa kuwalinda.

Matukio mengi ya hivi karibuni ambapo wananchi wameamua kupambana angalau kwa mawe na askari wa mgambo ambao mtindo mkuu wa utendaji wao ni nguvu na ubabe, ni kielelezo tosha cha jinsi uingiliaji kati wa Serikali unavyohitajika mapema.

Hata hivyo, inashangaza kwamba kila uchao mambo yale yale ya wananchi kupigwa, kuporwa mali zao, na kunyanyaswa na wanamgambo yanaendelea kurudiwa katika kila kona ya nchi huku Serikali ikionekana wazi kukaa kimya au kuunga mkono kimyakimya utendaji huo wa mabavu dhidi ya wananchi.

Mgambo ni jeshi halali japo si chombo cha dola. Haliundwi na rais kama yalivyo majeshi mengine isipokuwa linaundwa na sheria ndogo ndogo ambazo zinazipa mamlaka halmashauri za miji au wilaya kujiundia vyombo vyao vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kusimamia shughuli ambazo zipo chini ya mamlaka yao. Hata hivyo, mamlaka hayo kamwe hayawezi kuzidi au kukiuka yale ya vyombo vya dola ambavyo vinasimamia na kudhibiti masuala ya kitaifa, ikiwamo haki za kikatiba za wananchi.

Historia isiyo rasmi ya dunia nzima inaonyesha kwamba mizozo yote iliyozikabili sehemu mbalimbali za dunia ilizuka kutokana na watawala kutumia vyombo vya ulinzi na usalama visivyo rasmi, kuwanyamazisha wananchi.

Sitaki kuyafananisha jeshi la mgambo la Tanzania na yale tunayoyasikia kila siku duniani kote yakisababisha machafuko katika nchi mbalimbali lakini lazima niseme kwamba kama majukumu mazito ya kusimamia haki za raia yataendelea kuachwa katika mikono ya majeshi haya ambayo hayana mafunzo ya kutosha ya kukabiliana na changamoto za kiraia, hapana shaka siku moja mambo hayatakuwa tofauti na yale yanayotokea kwingineko duniani.

Katika Tanzania majeshi ya mgambo yanamilikiwa na halmashauri za miji au wilaya.

Halmashauri ndizo zenye mamlaka ya kusimamia shughuli zote za utendaji na maendeleo katika miji au wilaya hizo.

Kwa jinsi hii ni lazima halmashauri hizi zitakuwa na sheria zake ndogo ndogo ambazo ili zipate utii wa kutosha lazima zisimamiwe na vyombo kama Jeshi la Mgambo. Hata hivyo, ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi hili karibu katika kila sehemu ya nchi unatosha kulionyesha kama jeshi jingine jipya lenye mamlaka kuliko yale ya dola ambayo mitandao yake ipo katika kila pembe ya nchi.

Kwa bahati mbaya, wakati vyombo vingine vya dola huwa ni kimbilio la wanaotafuta haki miongoni mwa wananchi, Jeshi la Mgambo limegeuka kuwa silaha tu za halmashauri hata pale inapothibitika kwamba makosa yako upande wa halmashauri hizo.

Miaka ya nyuma tuliona aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusufu Makamba akiamuru askari kadhaa wa mgambo wakamatwe na kuchukuliwa hatua baada ya kumnyanyasa mwananchi mmoja wa Sinza. Angalau hii ilikuwa hatua ya kutia moyo kwa vile kila aliyeliona tukio lile asingeweza kulitofautisha na unyama uliofanywa na Interahamwe wa Rwanda au Janjaweed wa Sudan. Cha kushangaza na kujiuliza ni kwamba, hatua kama zile zimeishia wapi? Tumeona watu wakipigwa na kuvuliwa nguo hadharani pale Mtaa wa Kongo, nani aliwachukulia hatua mgambo wale?

Kila siku wananchi wanaporwa mali zao mitaani na kuishia katika mifuko ya mgambo hawa huku wenyewe wakiishia kupigwa kama mbuzi, hivi Serikali inadhani mambo haya yataendelea kuvumiliwa mpaka lini?

Tukio la juzi pale Tabata Dampo jijini Dar es Salaam, linatosha kuwa kielelezo cha ubatili unaondeshwa na halmashauri hizi, huku zikilitumia jeshi la mgambo kufanikisha ubatili wao.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala inasema eneo lililobomolewa kwa nguvu kubwa ya mgambo ni la viwanda na wala si makazi.

Wanasema hukumu imetolewa mahakamani na wao walikuwa wakitekeleza amri hiyo ya Mahakama. Sielewi kwa nini amri hiyo isitekelezwe na polisi bali halmashauri hiyo ambayo nayo imejisema kuwa ilikuwa mshitakiwa katika kesi hiyo.

Hata hivyo, ambavyo wananchi tunajiuliza ni kwamba hata kama iwe ni kweli utekelezaji ule ulikuwa halali na eneo lile ni la viwanda, hivi kuna vituo vingapi vya mafuta katika halmashauri hiyo hiyo ya Ilala ambavyo vimejengwa katika makazi ya watu na mgambo hawatumiki kuvibomoa? Kuna maghala mangapi katika makazi ya watu ambayo hayabomolewi kule Kariakoo au kuna viwanda vingapi katika makazi ya watu ndani ya halmashauri hiyo hiyo ambavyo kamwe haviguswi na nguvu za Halmashauri?

Kwa maana hii, Halmashauri ya Ilala inatwambia kwamba haiwezi kusimamia sheria kwa kutumia mgambo wake mpaka pale inapopata amri ya Mahakama, japo zaidi inatuonyesha kwamba matumizi ya mgambo kila siku yatawakuta watu masikini pekee, huku matajiri wakilitumia jeshi hilo kama fimbo za kutekelezewa mahitaji yao.

Ni lazima Serikali ielewe kwamba halmashauri nyingi hapa nchini zimejaa ufisadi ambao mara zote umelindwa kwa kupitia sheria ndogo ndogo, ikiwamo Jeshi la Mgambo. Kuziachia kuendelea kumiliki majeshi yanayonyanyasa watu ili kuwezesha ufisadi wa halmashauri hizo kuna hatari kubwa mbele kwa vile siku moja watu hawatakubali kuburuzwa kama kondoo.

Ningeruhusiwa kushauri ningesema kwamba ni afadhali sasa kabla mambo hayajaharibika zaidi, jeshi hili la mgambo liwe chini ya usimamizi kamili wa Jeshi la Polisi na pindi yanapohitajika kutumika isiwe tu kwa kuitaarifu Polisi isipokuwa Polisi iwe na mamlaka kamili ya kuwaruhusu mgambo baada ya kujiridhisha na sababu za operesheni husika.

uhalisi@yahoo.co.uk
 
NImeona hii picha ninayoambatanisha hapa chini, nikajiuliza, ni mamlaka gani na sheria zipi ambazo zinawapa mgambo nguvu kama polisi?

7572.JPG

[SIZE=-2]Mgambo wa Manispaa ya Ilala, wakimpeleka Kituo Kidogo cha Polisi Kisutu, Dar es Salaam, mkazi wa Jiji ambaye walimkamata kwa kukasirishwa na kitendo cha kumsaidia mchuuzi aliyekuwa akinyang'anywa toroli lililokuwa limesheheni machungwa aliyokuwa akiuza katikati ya Jiji jana. (Picha na Richard Mwaikenda) [/SIZE]

Nachofahamu mimi, jeshi la mgambo linaongozwa na kuuanzishwa kwa sheria inayoitwa THE PEOPLE'S MILITIA ACT NO.9 ya mwaka 1989, kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka toka awamu hadi awamu ,pia wanaongozwa na sheria inayoitwa THE PEOPLE'S MILITIA(POWER OF ARREST) ACT,1975 na mwisho THE PEOPLE'S MILITIA(Compensation for injuries)ACT ya mwaka 1973.Sheria hizi ni za zamani sana na zinakuwa complemented na sheria nyingine kama vile za halmashauri na ile inayompa mamlaka mkuu wa wilaya.Na People's millitia imekuwa defined kama;

Peoples Militia'' means an organized group of the people of the
United Republic operating with the authority of and under the
aegis of the Government and which is receiving any military
training or participating in any military, quasi-military or law
enforcement exercise for the protection of the sovereignity of the
United Republic or for the protection of the people or the property
of the United Republic, but does not include the Police Force,
any arm or branch of the Defence Forces, the Prisons Service or
the National Service.

Naomba kuwasilisha.
 
Hata kama kuna sheriaimewekwa kuunda Mgambo, lakini utendaji kazi wao unaonyesha hauna nidhamu hata kidogo.

Jinsi wanavyofanya kazi kwa jazba, ubabe na kutokujali mali au uhai, inakuwa sawa na vile vikundi vya kiharamia janjawidi Sudan, wababe wa Sierra Leone, wenye mapanga Rwanda na Burundi na sehemu nyingine ambako kuna hawa "sungusungu" ambao hujichukulia hatua mkononi kutoa adhabu.
 
NImeona hii picha ninayoambatanisha hapa chini, nikajiuliza, ni mamlaka gani na sheria zipi ambazo zinawapa mgambo nguvu kama polisi?

7572.JPG

[SIZE=-2]Mgambo wa Manispaa ya Ilala, wakimpeleka Kituo Kidogo cha Polisi Kisutu, Dar es Salaam, mkazi wa Jiji ambaye walimkamata kwa kukasirishwa na kitendo cha kumsaidia mchuuzi aliyekuwa akinyang'anywa toroli lililokuwa limesheheni machungwa aliyokuwa akiuza katikati ya Jiji jana. (Picha na Richard Mwaikenda) [/SIZE]

Ni hii hapa
THE PEOPLE'S MILITIA(POWER OF ARREST) ACT,1975
ukihitaji nakala yake kwenye pdf nitakuwekea hapa,ili majadiliano yanoge.
 
Hata kama kuna sheriaimewekwa kuunda Mgambo,
lakini utendaji kazi wao unaonyesha hauna nidhamu hata kidogo
.

Jinsi wanavyofanya kazi kwa jazba,
ubabe na kutokujali mali au uhai, inakuwa sawa na vile vikundi vya kiharamia janjawidi Sudan, wababe wa Sierra Leone, wenye mapanga Rwanda na Burundi
na sehemu nyingine ambako kuna hawa "sungusungu" ambao hujichukulia hatua mkononi kutoa adhabu.

Sasa hayo ya kukiuka utaratibu sheria haijawaruhusu hata kidogo,huo ni ukiukaji maadili kama ambavyo polisi au mwanajeshi yeote yule anaweza kukiuka.Ila kwa sawli kuwa wanaongozwa na sheria zipi,hizo nilizokutajia ndio sheria zao kama ambavyo polisi wanaongozwa na PGO zao,CPA,Police force and auxiliaary ...Act nk
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom