Jeshi la Magereza limewaonea wanafunzi maafisa Kiwira! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi la Magereza limewaonea wanafunzi maafisa Kiwira!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KazaMwendo, Nov 7, 2009.

 1. K

  KazaMwendo New Member

  #1
  Nov 7, 2009
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana kuona vijana wanapata ajira serikalini halafu bila kutendewa haki mnawafukuza kwa makosa yenu wenyewe.Jeshi la magereza walitangaza nafasi za kazi ambapo walitakiwa wasomi na wengineo.Tulijitokeza kufanya interview na baada ya wiki mbili majibu ya tuliofanikiwa yakatoka.Tukaweka kambi chuo cha maofisa UKONGA na kufanyiwa vipimo vyote mbavyo vinatakiwa.Ninaposema vyote namaanisha vyote.Baada ya hapo tukapewa majibu yetu na kujiandaa kwa ajili ya kwenda kiwira kwa mafunzo.Tukaenda mafunzoni tukiwa tunajua tumeajiriwa na serikali kwani walituhakikishia kuwa tayari rumepata ajira.Sasa ndugu zangu ajabu ni kwamba baada ya kuanza mafunzo kule kiwira kwa miezi miwili,wanakuja haohao waliotuambia tumeajiriwa,wanakuja na kuwafukuza wenzetu kwa kigezo cha matatizo ya afya.Ndugu zangu,hawa watu walitupima wote na kutupa majibu kulekule UKONGA kabla ya kwenda mafunzoni.sasa kama sio njama za kuwatoa wenzetu na kuwaweka watu wao ni nini? Kwanini hawakusema mapema?Kweli ni haki iliyotendeka hapa.? Kuwapeleka watu mafunzoni wamehangaika miezi 2 halafu mnawafukuza kwa makosa yenu nyie?? Wana JF hapo pako sawa? Mbaya zaidi wengine wametolewa kwa kisingizio cha kuwa wanaumwa macho,wakati walipimwa na kuridhika nao...Serikali inatupeleka wapi???
  Mkereketwa
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Such rotten that its irrepairable!...Zote hizo ni harufu za rushwa na ndugunization!...Ninaishi na Kamanda wa Zimamoto huku mikoani, ambaye alikuwa amemwombea mwanae nafasi ya Uaskari zimamoto, lakini jina lake halikutokea...Basi alimpigia simu Kamishna wa Zimamoto na kumwambia kila kitu, ambapo aliweka hazarani kwamba alikuwa ameombwa rushwa alishawatumia watahini hao kilo kibao za maharage na nyama huko Dar, na bado wamemkata mwanae...Bosi huyo aliahidi kuwafuatilia waendesha interview!..Huenda jamaa zako wanaathiriwa na mambo kama hayo ndugu!..lol!Kweli
   
 3. K

  KazaMwendo New Member

  #3
  Nov 7, 2009
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwakweli hili hatutalinyamazia,ni uonevu wa hali ya juu. Ajira kwa vijana ndio hizi,watu wanatafuta kwa nguvu zao halafu wengine wanakuja kuchukua kiulaini,kwakweli hii itafika mbali kama sio wenzetu warudishwe kwani wana sifa zote na mbaya zaidi tumehenya nao huku kwa miezi miwili..
   
 4. D

  Da Meya New Member

  #4
  Nov 7, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This is too much jamani,Serikali ya Tanzania ni ya kujuana. wenye nazo wanapata kirahisi lakini hatuwezi kukaa kimya,mimi mafunzo ya jeshi najua yanavyokuwa.imagine mtu ukae miezi miwili ukiwa na uhakika wa kazi halafu wanakufukuza?? Hapana,this has to go far. Ongeeni na waziri masha mumpe malalamiko yenu kama huyo Kamishna Mkuu kawazingua.
   
 5. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nani wakuanza kuongea na Masha hujui Masha na huyo Kamishna ni wa CCM tena wana mtandao, wewe unaafikiri huyo Kamishna aliupataje huo ukamishna? Jaribu kulalamika kama haujanyea ndoo!!!!
   
 6. D

  Da Meya New Member

  #6
  Nov 7, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Basi ndugu yangu washauri hao wenzio waende Haki za Binadamu,nina uhakika watawasaidia hata ikiwezekana warudishwe mafunzoni.Watanzania tutaoneana mpaka lini jamani? Halafu haohao mwaka 2010 tunawapa kura zetu wakati chinichini wanatufanyia unyama.Nimepata website ya Haki za binadamu,watafuteni watawasaidia http://www.chragg.go.tz.
  Nitakuwa nanyi.Najua machungu yao kwani na mimi nimepitia Jeshini,sio mchezo.Halafu eti ukae miezi miwili wakutoe???!!!
   
 7. K

  KazaMwendo New Member

  #7
  Dec 3, 2009
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hili jambo halijapatiwa ufumbuzi, kuna mwenye msaada?
   
 8. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwenye haki kwahitaji ujasiri, hivyo kinachotakiwa kufanyika kwa sasa ni hao vijana wajitolee watafute chombo cha habari ambacho wao wenyewe wanajiridhisha kwamba kitawafikishia taarifa kwa umma, nina hakika taasisi zetu nyingi zinafanya kazi kwa milipuko ya habari ni kwa njia hiyo tu habari ikitoka either gazetini au redioni ndipo itaanza kushughulikiwa kama kwamba ni habari mpya.

  Tahadhari: Wanapaswa kuwa na vielelezo vyote muhimu.
   
Loading...