Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)

Sir Carter

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
632
1,396
Habari zenu wana JF...

Ninaomba kuuliza iwapo kama kuna mtu anataarifa yeyote kuhusu nafasi za kujitolea za Jeshi la Kujenga Taifa maana nimesikia zimetoka lakini sijapata uhakika na taarifa nimeuliza humu iwapo kama kuna mtu anajua anifahamishe na mimi...
 
Ushachelewa Mbona watu wameshaenda muda sana. Jaribu mwakani. Kama una degree jaribu polisi peleka barua wizara ya mambo ya ndani nilisikia wanapokea baru a ila sijajua kuhusu dead line yao
 
Awamu nyingine walioingia mwaka jana mwezi wa12 ndio imemaliza mafunzo wiki iliyopita na wiki hii walioenda ni wale wa form6...
Awamu hii wakujitolea ndio sijapata taarifa kamili nimepata tetesi tu kama wameshatangaza ingawa haiko official...
 
Hakukua na tangazo Mjomba unaambiwa upeleke barua ya kuwa recruited ktk mafunzo basi. Maafisa hawanaga matangazo. Subiri zile za wote kama hizi zimeshapita
Hakuna kitu hicho usidanganye watu

Kwa sasa huwezi kwenda kozi ya uafisa bila kupitia ukuruti (kozi mama).

Ukitoka kozi unasugua benchi kwanza kabla ya kwenda kozi ya uafisa.
 
Mkuu tusibishane mimi sio polisi nilipewa hiyo taarifa na watu wa karibu. Kama nimepotosha na wewe unaufahamu ukweli basi sawa.
 
James Comey, acha kudanganya watu , Mzee wangu niyupo huko makao ni Brg.. Naday today napata updates .

Bado hazijatoka ila kwamwaka kuna uwezekano wakutotoka . muweni wavumilivu.
 
Mkuu tusibishane mimi sio polisi nilipewa hiyo taarifa na watu wa karibu. Kama nimepotosha na wewe unaufahamu ukweli basi sawa.
Taratibu nazifahamu.
Kwa sasa ni ngumu kujiunga na jeshi lolote bila kupitia jkt.
Hakuna kozi ya uafisa bila kupiga kozi ya awali.
 
Kwa hiyo mkuu hadi madaktari wanapitia JKT?

Last time watu wa afya walikua wanaapply makao pale then wanaenda pre cadet Ruvu kwa muda mfupi halafu ndio bogi linaenda TMA

Utaratibu umebadilika lini?
 
Habari zenu wana JF...

Ninaomba kuuliza iwapo kama kuna mtu anataarifa yeyote kuhusu nafasi za kujitolea za Jeshi la Kujenga Taifa maana nimesikia zimetoka lakini sijapata uhakika na taarifa nimeuliza humu iwapo kama kuna mtu anajua anifahamishe na mimi...

Kweli Watanzania bado tuna safari ndefu ya katika kubadilika hasa Kifikra na Kiupeo. Yaani kila mara hawa hawa JKT na hata JWTZ huwa wanatoa ufafanuzi juu ya Mafunzo yao na huwa wanatuambia kila mara kuwa tuachane na kutafuta taarifa kwingineko kote bali tuhakikishe kila mara tunatembelea mitandao yao ambayo iko verified kabisa kuweza kujiridhisha zaidi.

Hivi kama umeweza kuja kuuliza huku umeshindwa nini kuingia tu katika Kurasa zao hasa JKT uweze kupata taarifa za Kuaminika?

Cc: MAWAZO UJENZI
 
Kwa hiyo mkuu hadi madaktari wanapitia JKT?

Last time watu wa afya walikua wanaapply makao pale then wanaenda pre cadet Ruvu kwa muda mfupi halafu ndio bogi linaenda TMA

Utaratibu umebadilika lini?
Madaktari ni special case, ila kwa kada nyingi zilizosalia ni lazima uonje mziki wa jkt.

Pia naamini iko siku hata madaktari watatakiwa kupitia jkt full course maana jeshi kwa sasa limeanza kusomesha wataalam wake hasa wale wanamaliza form six (kombi za sayansi).
 
Waache wenge wasubiri jkt itangaze nafasi
Na changamoto inakuja kuna OP 3 ziko kwenye makambi ya malezi lolote linaweza kuwa uvumilivu unahitajika watatoa hizo nafasi
 
Kweli Watanzania bado tuna safari ndefu ya katika kubadilika hasa Kifikra na Kiupeo. Yaani kila mara hawa hawa JKT na hata JWTZ huwa wanatoa ufafanuzi juu ya Mafunzo yao na huwa wanatuambia kila mara kuwa tuachane na kutafuta taarifa kwingineko kote bali tuhakikishe kila mara tunatembelea mitandao yao ambayo iko verified kabisa kuweza kujiridhisha zaidi.

Hivi kama umeweza kuja kuuliza huku umeshindwa nini kuingia tu katika Kurasa zao hasa JKT uweze kupata taarifa za Kuaminika?

Cc: MAWAZO UJENZI
CDF Kalitolewa ufafanuzi juzi tu hili suala, sasa nashindwa kuelewa vijana wanakuaje???
 
Kweli Watanzania bado tuna safari ndefu ya katika kubadilika hasa Kifikra na Kiupeo. Yaani kila mara hawa hawa JKT na hata JWTZ huwa wanatoa ufafanuzi juu ya Mafunzo yao na huwa wanatuambia kila mara kuwa tuachane na kutafuta taarifa kwingineko kote bali tuhakikishe kila mara tunatembelea mitandao yao ambayo iko verified kabisa kuweza kujiridhisha zaidi.

Hivi kama umeweza kuja kuuliza huku umeshindwa nini kuingia tu katika Kurasa zao hasa JKT uweze kupata taarifa za Kuaminika?

Cc: MAWAZO UJENZI
Nashukuru kwa taarifa nilikua sina habari hii ya wao JKT na JWTZ kutoa ufafanuzi kuhusu kupata taarifa pembeni maana mimi nilipata taarifa pembeni nikasema nijaribu kuuliza huku huenda kuna watu wana taarifa zaidi lakini umenijuza kwahilo.

Ahsante...
 
Vijana hawa ndiyo walewale tangazo la NBS lilitoka.la kazi nafasi 450+ wao wakaja na thread za.kitoto za kuuliza ofisi, mara wanalipa shilingi ngapi, mara hawataenda vijijini.

Yaani, vijana wa leo ni majanga ila ao hao wanalala kwenye Instagram na FB, lakini kuperuzi kwenye tovuti za jeshi, jkt na kwengineko hawataki kabisa.
 
Back
Top Bottom