Jeshi la Kujenga taifa (J.K.T) lakanusha Uvumi wa kutangazwa wa nafasi za Mafunzo 2016.

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,233
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), linapenda
kuutaarifu umma, kuzipuuza taarifa
potofu zinazosambazwa mitaani na
katika mitandao ya kijamii kuwa, JKT
limeanza kuandikisha vijana wa
kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa
Kujitolea kwa mwaka 2016.



Taarifa hizo siyo sahihi na wananchi
wanatakiwa kupuuza upotoshaji huo
wenye sura ya utapeli unaofanywa na
kikundi kidogo cha watu. Aidha, yeyote
anayedai kupewa fedha ili aweze
kumuingiza kijana katika Jeshi la
Kujenga Taifa aripotiwe mara moja
Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa.
Katika hili unahitajika ushirikiano wa
karibu sana ili kuweza kudhibiti
udanganyifu na utapeli unaofanywa na
watu wachache wanaojifanya wana
uwezo wa kuwaingiza vijana JKT, na
kudai watumiwe fedha kupitia mitandao
ya simu za mikononi kama vile Tigo
Pesa, M- Pesa, Airtel Money.




JKT linasisitiza kuwa, muda wa kuanza
mchakato wa kuchukua vijana wa
kujiunga na mafunzo ya JKT kwa
kujitolea utakapowadia, wananchi
watatangaziwa rasmi kupitia Mamlaka
za Serikali zinazohusika pamoja na
vyombo vya habari hapa nchini. Aidha
inazidi kukumbushwa kuwa nafasi za
vijana kujiunga na mafunzo ya JKT kwa
kujitolea hazipatikani kwa kununuliwa.


IMETOLEWA NA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO,
MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA, LEO TAREHE 08 JANUARI 2016
 
Back
Top Bottom