Jeshi la Iran linapaswa kuwa na uwezo utakaomfanya adui ashindwe kuvunja ngome imara ya Iran | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi la Iran linapaswa kuwa na uwezo utakaomfanya adui ashindwe kuvunja ngome imara ya Iran

Discussion in 'International Forum' started by KABAVAKO, Sep 19, 2012.

 1. KABAVAKO

  KABAVAKO JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa jeshi hilo kupata uwezo mkubwa wa kuzuia aina yoyote ya mashambulizi ya adui dhidi ya Iran ya Kiislamu. Ayatullah Ali Khamenei ambaye alikuwa akihutubia hadhara ya makamanda wa jeshi la Iran na watayarishaji wa maonyesho ya mafanikio ya jeshi hilo katika mji wa Noushahr huko kaskazini mwa Iran, ameelezea kuridhishwa kwake na maendeleo makubwa ya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu na kusisitiza kuwa jeshi hilo linapaswa kupata uwezo mkubwa ambao hautampa mtu yeyote nafasi ya kushambulia ngome imara ya nchi na taifa la Iran. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa kuambatanishwa elimu na vitendo ndio sababu muhimu zaidi ya kufikiwa malengo na kutekelezwa kazi kwa njia sahihi. Amelitaka jeshi la Iran kutilia maamani suala hilo muhimu. Ayatullah Ali Khamenei ameashiria sisitizo la mafundisho ya Uislamu kuhusu nafasi ya juu ya elimu na amali na udharura wa kuambatanishwa viwili hivyo na kusema: "Kama ilivyosisitizwa tangu miaka mingi iliyopita, vituo vya elimu na mafunzo katika vikosi vya jeshi vinapaswa kuwa na maendeleo na ustawi endelevu. Amiri Jeshi Mkuu amesema kuwa lengo la muda mrefu la majeshi ya Iran ni kuwa na jeshi imara na linaooana na malengo na thamani za Jamhuri ya Kiislamu. Ameongeza kuwa thamani na malengo ya utawala wa Kiislamu hapa nchini ni mapana na yanahusu jamii nzima ya binadamu na haijuzu kushambulia na kuvunja heshima na mamlaka ya nchi yoyote kwa ajili ya kutimiza malengo hayo. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amelitaka jeshi kutoa kipaumbele kwa sayansi na elimu ya kisasa, kudumisha utengenezaji wa zana za kijeshi, kuzidisha kasi ya harakati ya utengenezaji vipuri, kuboresha na kubuni vitu vipya katika medani ya sayansi, kutumia walimu hodari, kupanua zaidi ushirikiano na vituo vya elimu na sayansi na vyuo vikuu na kutilia maanani masuala ya kimaanawi na kiroho.
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  mbwa asiye na meno anabweka....wasubiri kichapo tu, kinakuja wala hakiko mbali. hata sadam ilikuwa hivyoivo, hata gadafi....nchi za hawa watoto wa mamamdogo huwa wanajiamini sanaa kumbe hawana lolote, mwisho wake wanaishia kujificha kwenye mifereji ya nnya.
   
 3. k

  kalikenye JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 1,616
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Unamaslahi gani na hicho kichapo unachokitabiri?
   
 4. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Wakati wa vita hivyo Hormuz itafungwa hivyo basi mafuta yatapaswa kutumia njia ndefu kuja kwetu huku na makampuni yetu ya zamani makina BP, ili kufidia hasara waliyopata. Hivyo faida atakayopata ni kutoka ubungo mpaka mbagala kwa miguu!! Alichosahau ni kuwa kama vita ya Libya tu imefikisha bei ya mafuta hapo je hiyo itakayogusa njia halisi?
   
Loading...