Jeshi la Australia lanasa silaha Somalia

Don san tan

JF-Expert Member
May 23, 2015
562
433
Jeshi la wanamaji wa Australia
limekamata boti moja katika pwani ya
Oman ambayo haikujulikana inakotoka.
Ilisemekana ni boti la uvuvi lakini
walipofanya upekuzi,wakagundua
shehena kubwa ya silaha ambazo
wanashuku zilikuwa zinapelekwa Somalia.
Miongozni mwa silaha hizo ni magruneti
na bunduki zaidi ya 2,000 za AK 47
bunduki aina za rashasha mbali na
bunduki zenye nguvu.
Shehena hiyo ya silaha ilikuwa imefichwa
chini ya neti za uvuvi.
Majeshi ya wanamaji wa Australia ni
mojawapo ya majeshi ya kimataifa wenye
meli zinazoshika doria kwenye bahari kuu
na wanamamlaka ya kukamata silaha
zinazopelekwa Somalia.
Je boti hiyo ilikuwa ya akina nani hasa,
taarifa hizo hazijawekwa bayana hadi
sasa.
Licha ya marufuku ya Umoja wa mataifa
kuzuia kununua ama kuuzwa kwa silaha
nchini Somalia ,Umoja huo huwa
unairuhusu serikali ya taifa hilo
lililosakamwa na vit katika upembe mwa
Afrika kununua silaha ndogo ndogo kwa
nia ya kuisaidia kujihami dhidi ya
makabiliano na kundi la Al Shaabab na
kulinda usalama wa raia nchini.
 
Back
Top Bottom