Jeshi Binafsi La Marekani Latuhumiwa Kufanya Mauaji ili Kuangamiza Waislamu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
Wanajeshi wa jeshi binafsi la Blackwater Wednesday, August 12, 2009 9:19 AM
Bosi wa jeshi binafsi la ulinzi la Marekani linaloitwa Blackwater linalolinda amani nchini Iraq ambaye yeye mwenyewe inasemekana anajiona ni masiha aliyetumwa kuwaangamiza waislamu na kuutokomeza uislamu duniani anafanyiwa uchunguzi kufuatia tuhuma za mauaji ya raia wengi sana wa Iraq wasio na hatia.
Mwasisi wa kampuni hiyo inayoitwa Blackwater, Erik Prince kwa mujibu wa wafanyakazi wake wa zamani anajiona ni masiha kristo aliyetumwa kuja kutokomeza uislamu na waislamu duniani.

Kampuni hiyo ya jeshi binafsi la ulinzi la Marekani ni miongoni mwa makampuni matatu binafsi ya ulinzi yaliyokodishwa na Marekani kulinda amani nchini Iraq.

Blackwater iliingia mkataba na Marekani iwasaidie wanajeshi wa Marekani nchini Iraq kulinda amani, lakini matokeo yake wanajeshi wa Blackwater ambao muda wote hutembea na silaha nzito wanaogopwa zaidi na raia wa Iraq kuliko wanajeshi wa Marekani.

Wakati hatua za kisheria dhidi ya mwasisi huyo wa Blackwater zikiwa zimeanza nchini Marekani, ndugu wa wahanga wa mauji yaliyofanywa na Blackwater nchini Iraq wamesema wako tayari kutoa ushahidi mahakamani.

Farid Walid ambaye ni mmoja wa watu waliojeruhiwa kwa risasi miaka miwili iliyopita wakati wa mauaji ya raia wa Iraq 17 yalipofanyika, aliliambia gazeti la The Times la Uingereza, "Kila Mtu Hapa anajua jinsi Blackwater wanavyofanya mauaji ya watu wasio na hatia bila hata kufikiria".

Katika mauaji hayo, maafisa wa serikali ya Iraq waliwatuhumu wanajeshi wa Blackwater kutumia mabomu na kupiga risasi hovyo kuifanya barabara iwe nyeupe baada ya kukwama kwenye foleni ya magari barabarani.

Prince yeye binafsi anatuhumiwa kuingiza silaha kwa siri nchini Iraq kwa kutumia ndege yake binafsi na kuwaruhusu wanajeshi wa kampuni hiyo kutumia risasi zinazolipuka ambazo zimepigwa marufuku ili kuwaua wananchi wengi zaidi wa Iraq.

Kwa mujibu wa viapo vya wafanyakazi wake wawili wa zamani vilivyowakilishwa kwenye mahakama ya Virginia, Marekani siku ya jumatatu, mwasisi wa kampuni hiyo pia anatuhumiwa kuwaua au kuwatuma watu wawaue wafanyakazi wake waliokuwa wakishirikiana na maafisa wa Marekani katika kuchunguza vifo vya raia wa Iraq.

Wafanyakazi hao walisema kwamba Blackwater ilikuwa ikifanya mauaji ya kukusudia bila sababu ya msingi na walijihusisha na biashara ya silaha.

Wafanyakazi hao wawili walitoa viapo vyao na maelezo yao huku wakipewa majina ya bandia John Doe No 1 and John Doe No 2, kwakuwa walisema wanahofia maisha yao iwapo watagundulika wametoa ushahidi.

Katika mojawapo ya maelezo ya John Doe 2, ambaye alifanya kazi kama muajiriwa wa Blackwater kwa miaka minne alisema "Bwana Prince anajiona mwenyewe kama masiha wa kristo aliyetumwa kuwaangamiza waislamu na uislamu duniani" na kampuni yake "inaunga mkono na kusaidia katika jambo hilo kwa kuyaharibu maisha ya raia wa Iraq".

Wafanyakazi hao walisema kuwa Prince na viongozi wake wa juu waliharibu ushahidi wa video, email na nyaraka mbali mbali pamoja na kuficha tabia yao ya kufanya mauaji mbele ya wizara ya ulinzi ya Marekani.

Viapo hivyo ni mojawapo ya hatua za wanasheria wa Marekani wanaowawakilisha raia 60 wa Iraq ambao wanaishtaki kampuni ya Blackwater kwa mauaji iliyofanya.

Wafanyakazi hao pia walisema kuwa wanajeshi wa Blackwater walikuwa wakipewa madawa ya kuwabadilisha mawazo pamoja na madawa ya kuongeza nguvu ya steroids na pia walikuwa wakiwatumia makahaba watoto wa Iraq tofauti na jukumu lao la kuwalinda na kuwasaidia kuwa na maisha bora.

Mwanzoni mwa mgogoro wa Iraq, wanajeshi wanne wa Blackwater walivamiwa na kuuliwa na kisha miili yao kuchomwa moto na baadae kuning'inizwa kwenye daraja, hayo yalikuwa mauji ya kikatili yaliyowahi kufanyika nchini Iraq.

Jukumu la Blackwater nchini Iraq ni kusindikiza misafara ya wanadiplomasia mbali mbali pamoja na kulinda maeneo wakati wanajeshi wa Marekani wanapolala.

Hutumia helikopta na huingia kwenye mapambano ya kijeshi wakilisaidia jeshi la Marekani.

Blackwater ndio kampuni kubwa kuliko zote katika kampuni tatu za ulinzi zilizoingia mkataba na wizara ya ulinzi ya Marekani kulinda amani nchini Iraq.

Hata waziri mkuu wa Iraq, Nouri al-Maliki, alishawahi kutamka mara kadhaa akiitaka kampuni hiyo ya ulinzi ya Blackwater, ifukuzwe nchini Iraq lakini kampuni hiyo yenye makazi yake North Carolina, Marekani iliendelea kukaa nchini humo hadi mkataba wake ulipoisha mwezi mei mwaka huu.

Hatimaye wanajeshi wa Blackwater wataondoka nchini Iraq mwezi septemba.
GONGA HAPA KWA PICHA ZA BLACKWATER WAKIWA KAZINI > http://www.nifahamishe.com/photos_news.aspx?topic=165&&NewsId=713
 
Lilishindwa jashi la tembo wataweza hao.

Hakika haki haiwezi kabida kushindwa ba batili.
 
Bush kuna wakati alisema anapeleka Crusaders in Iraq. Hiyo ni moja sababu iliyochangia hao Blackwater kufanya mauaji ya kinyama dhidi ya Iraq people.
 
Moja ya theory ya Realism ni kuimpose their cultures to another country. NeoConservertisim wanaamini kwamba MidEast inabidi ifuate US culture in order to love US. Hii theory waliitumia wakati wa World War 11. Ambapo US walitunga katiba ya Japan na baadae Japan walianza kufuata US cultures. Realist wanaona dini ndiyo tatizo kubwa ambalo lipo MidEast. Moja ya strategy yao sasa hivi ni kuondoa Madrasa (Muslim School) kote MidEast.
 
Nop si kweli nia ya kampuni hiyo kuuangamiza uislamu,hii ni kampuni binafsi ambayo ilichukua tenda ya kuwalinda wanadipromasia wanaofanya kazi ubalozini iraq,ni kweli wamesababisha maafa kibao nadhani sasa wamebadili jina baada ya kupata kasha ya kuua watu wasio na makosa ;labda uniambie walipewa tenda bila kuwa na washindani hapo sawa.
 
oldnews1.jpg
 
Blackwater Worldwide are in iraq to do america's dirty jobs without the fear of prosecution.In iraq today kids after learning the words pappa and mom,next comes the word blackwater.you would rather meet american marines in the streets of baghdad then meet blackwater guards-these guys are trigger happy
 
Back
Top Bottom