Jesca Kishoa: Tusikubali kurudia makosa uwekezaji gesi asilia

the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
652
441
Mh Jesca Kishoa (Mb, )

Moja ya vitu ambavyo taifa lolote lile lingependa kujivunia kuwa navyo ni RASILIMALI. Msisitizo wangu mara zote umekuwa ukizingatia jinsi taifa litakavyonufaika vema na rasilimali zetu muhimu.

Moja ya mjadala mkubwa unaoendelea kwa sasa nchini ni juu ya Mkataba kati ya Serikali na campuni ya BAKER BOTTS .

Labda ni vema nianze kwa uchache kufafanua ukubwa wa investment hii ili tuone ni kwa namna gani ni muhimu kuwepo na nguvu na umakini mkubwa katika kuliamua na kulijadili swala hili.

UKUBWA WA MRADI
Ukubwa wa mradi wa Gesi Asilia huko mkoani Lindi ni dola billion 30 . Hii jumla ya chumi (GDP) za nchi nne;
Rwanda (10.5) , Burundi (3.1) , Msumbiji (14.3) na Somalia (5.4) , zote kwa pamoja.

Lakini pia ni sawa karibu na uchumi wote wa Uganda (32). Au kwa maana nyingine mradi huu mmoja tu ni takribani 50% ya uchumi (GDP) ya Tanzania.

Kwa ufupi uwekezaji huu wa mradi huu ndio mkubwa East Africa Nzima hakuna. Hivyo kwa vyovyote vile unahitaji kufanywa kwa ufanisi mkubwa kuanzia hatua za awali ambazo ni majadiliano. Napongeza hatua ya kuongeza nguvu ya washauri kwenye majadiliano haya. Sio ajabu ! Hili ni jambo la kawaida kabisa kufanywa na nchi mbalimbali duniani.

UWEZO WA KAMPUNI
Serikali kupitia TPDC imesaini mkataba na kampuni ya BAKER BOTTS ili iwe mshauri elekezi kati ya serikali na makampuni ya Equinox, Shell, ExxonMobil, Pavilion Energy, na Ophir Energy, wawekezaji kwenye mradi huo. Binafsi sina shaka na uwezo (CAPACITY) ya kampuni hiyo, nimeona kuwa ina uzoefu wa zaidi ya miaka 190 kwenye taaluma ya sheria na nishati na hasa gesi asilia, ikiwa imesimamia mikataba ya transactions kama huu wa kwetu kwenye miradi zaidi ya 120 ya gesi asilia kwa zaidi ya nchi 30 , ununuzi na ujenzi wa matenki 70 ya gesi asilia, ujenzi na ununuzi wa meli kubwa la kusafirisha gesi, kusimamia zaidi ya wanachama 200 wa sekta ya nishati duniani kwa ajili ya makubaliano ya gesi (LNG Master Sales Agreement), na ina wanasheria wapatao 725 wanaotambulika duniani. Tunategemea uzoefu uwe wa tija kwetu.

HOJA YA UWAZI NA WATAALAMU

Pamoja na ukubwa wao huo kampuni hii, hoja yangu hapa ni nchi yetu kupitia watu wetu kwenye sekta ya nishati kuendelea kujifunza kuhusu aina ya TAALUMA muhimu tunazozikosa nchini na zinaweza kuwa gharama kuzipata pale tunapozihitaji kwa sababu tu ya kutokuandaa watu wetu ili waendane na soko au mahitaji ya dunia. Ifike mahali maswala kama haya tuweze kuyasimamia wenyewe pasipo kutegemea nguvu kutoka nje.

Kwa miaka kadhaa, sekta ya nishati hapa nchini imekuwa kinara wa kuiingiza nchi kwenye skendo, gharama na upigwaji wa mara kwa mara kupitia mikataba mibovu na isiyowekwa wazi. Achilia mbali hizo skendo zilizoitikisa nchi, zikiwemo ESCROW ,
EPA , na RICHMOND. Mwaka 2018 nikiwa bungeni niibua hoja ya ubovu wa mkataba baina ya serikali na Kampuni ya SONGAS kwenye mradi wenye thamani ya Euro million 392 . Nilishauri serikali kupitia upya mkataba huo ulioliweka taifa kwenye hasara ya Tsh trillion 1.3 kufikia 2018 na ilikadiriwa kuwa mpaka mwisho wa mkataba huu (2024), Tanzania itakuwa imepoteza Tsh Trillion 2 au zaidi, kwa sababu ya kukosa umakini katika vipindi vya mwanzo vya majadiliano (negotiations). Nilionesha maeneo matatu ya ubovu wa mkataba ule; viwango vya uwekezaji (serikali 73% na SONGAS 27%), mgawanyo wa umiliki (serikali 46% na SONGAS 54%), na fidia za uwekezaji (capacity charge) serikali imekuwa ikiilipa SONGAS dola million 5 kila mwezi kimakosa mpaka leo.

Uzoefu wa taifa letu kupitia kwenye misukosuko ya kiuchumi kutokana na utiaji sahihi mikataba mibovu, ni sababu tosha kwa kila mwananchi anayependa nchi yake, kuwa sehemu ya kukataa kujirudia kwa changamoto hizi, kwani uwezo wa kuzuia ili yasitokee tena tunao.

Ninashauri 👇🏽;
1 . Pamoja na serikali kuamua kutumia makampuni tanzu na bora yenye uwezo mkubwa katika gesi, MIKATABA yote IWEKWE WAZI na ipelekwe bungeni ili ijadiliwe na kukubaliwa kabla ya kusainiwa na serikali kama ambavyo sheria ya uwazi sekta ya uziduaji inavyotaka. Hii inaonesha maana halisi ya bunge kuisimamia serikali na kutunga sheria.

2 . Nchi iwekeze kwenye NEGOTIATION skills. Kwa kuwa serikali ina mipango ya muda mrefu, ni vema iwapeleke watu wetu kwenye vyuo vya nchi zenye uwezo wa masuala ya diplomasia ya uchumi, majadiliano na usimamizi wa rasilimali kimakakati ili wasaidie taifa kwenye miradi ya kimkakati

3 . Local Content : Utekelezaji wa mradi huu uwe wa tija kwa watanzania (wazawa) kuanzia kwenye manunuzi, ajira na kuboresha maisha ya watu wetu, ikiwa ni pamoja na kuunganisha uwepo na mradi na faida zake kwenye sekta nyingine zinazotegemeana.

IMG-20220129-WA0006.jpg
 
anayekwenda kujadili bungeni ni nani?, aina ya wabunge tulionao ni watu wanaoweza kujadili na kudadavua hizo technical contracts kiuweledi kwa manufaa ya Taifa? ( tuanze from the basics kwa wabunge kuwa na angalau degree moja na kuendelea na exposure kwenye kazi yeyote kwa uzoefu hata miaka 4)..

Hatuhitaji kuwekeza kwenye negotiation skills, tunahitaji kuwa na mfumo bora wa elimu unaozalisha watu kweli wenye uwezo na maarifa ya kutosha kichwani...tuwe na mipango madhubuti juu ya graduates wetu wanapomaliza kwa kuwaattach kama internship kwenye makampuni makubwa ya kimataifa yanayofanya kazi hapa wapate exposure, tunahitaji kutrain watu wetu kwenye kada mbalimbali nje ya mipaka ya Tanzania hasa kwenye nchi zilizopiga hatua kwenye oil and gas na mining industry..

Local content ni upumbavu mtupu maana ipo na aisimamiwi ipasavyo zaidi ya mabwanyenye wenye mamlaka kutumia kigezo cha local contents kupenyeza makampuni yao na ndugu zao kila penye kazi zenye ulaji, mabwanyenye kutumia nyadhifa kuwasaidia matajiri kwa kupewa rushwa na kupenyeza makampuni.....

Hayo yote ni rahisi sana kila mtu individual akiacha UNAFIKI NA UBINAFSI...
 
Nadharia nzuri sana.
Swali muhimu; Hiyo gesi itakayohusika kwenye huo mradi TPDC/serikali inaimiliki kwa % ngapi?
Visima, viwanda vya kuchakata na mabomba ya kusafiririsha gesi yanamilikiwa na serikali kwa 100%?
 
Yule waziri wa kilimo wa sasa alikuwa anaongea sana na kuishauri serikali itumie njia au nini ili kufanikiwa, hatimaye late JPM akaona huyu anaongea sana ngoja nimpe nafasi kwa hicho anachokiongelea akifanyie kazi.

Huyu kijana mwenzenu (nishati) ni mbunge alikuwa na uwezo hata kabla ya kuteuliwa kuongea kwa uchungu kama bashe but nadhani na yawezekana anajua angeongea isingekuwa close deal kwa Magufuli ndiyo maana ameamua kufanya mikataba ya siri ila wenye nchi tunaonyeshwa wakiwa wanasaini basi.

Wanapoandaa deals wanaangalia jinsi ya kupiga kwa kuwashirikisha mabeberu huku ikitumika njia ya ushauli ambao tuna kumbukumbu zama zile za kina rostam na genge lake.

Huyu sijui joyce mb, yawezekana anaona bunge ni mbali so anaamua kuandika jf but bado bungeni ndipo sehemu sahihi ya kufunguka kuonyesha mna uchungu na nchi yenu, vinginevyo mnatuhadaa tu hapa.
 
Hii nchi tulichezewa tuna chezewa na tutaendelea kuchezewa..kama hatutaweka katiba mpya..na kusimamia sheria za nchi ipasanvyo zaidi hata ya china..kwa kuwawajibisha ipasavyo wanasiasa hasa wa ngazi za juu bila huruma kama wakifanya ufisadi au uhujumu uchumi wa nchi.

Hii nchi inahalibiwa na wanasiasa wenye ulafi..wizi walioendekeza maslahi yao mbele..na tuna wajua na kila siku wapo..serikalini na ndani ya chama..hao ndio tatizo la maendeleo kwa nchi yoyote duniani.

Ukiona nchi viongozi wake wajuu wanajiwekea kinga ya kutoshitakiwa..jua hapo hakua viongozi wazalendo bali wapigaji.

Mikataba iwekwe wazi..bungeni wananchi waifahamu..hivi hua mnaficha nini..mbona kuja kuomba kodi na tozo hua mnakuja open hamjifichi?

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
anayekwenda kujadili bungeni ni nani?, aina ya wabunge tulionao ni watu wanaoweza kujadili na kudadavua hizo technical contracts kiuweledi kwa manufaa ya Taifa? ( tuanze from the basics kwa wabunge kuwa na angalau degree moja na kuendelea na exposure kwenye kazi yeyote kwa uzoefu hata miaka 4)..

Hatuhitaji kuwekeza kwenye negotiation skills, tunahitaji kuwa na mfumo bora wa elimu unaozalisha watu kweli wenye uwezo na maarifa ya kutosha kichwani...tuwe na mipango madhubuti juu ya graduates wetu wanapomaliza kwa kuwaattach kama internship kwenye makampuni makubwa ya kimataifa yanayofanya kazi hapa wapate exposure, tunahitaji kutrain watu wetu kwenye kada mbalimbali nje ya mipaka ya Tanzania hasa kwenye nchi zilizopiga hatua kwenye oil and gas na mining industry..

Local content ni upumbavu mtupu maana ipo na aisimamiwi ipasavyo zaidi ya mabwanyenye wenye mamlaka kutumia kigezo cha local contents kupenyeza makampuni yao na ndugu zao kila penye kazi zenye ulaji, mabwanyenye kutumia nyadhifa kuwasaidia matajiri kwa kupewa rushwa na kupenyeza makampuni.....

Hayo yote ni rahisi sana kila mtu individual akiacha UNAFIKI NA UBINAFSI...
Mkuu kweli kuna mengi ya kufanya,elimu haiendani na matakwa ya taifa letu.Ni mmoja ya sababu za msingi makampuni ya nchi za kigeni yanapendelea kuwaajiri raia wa Kenya,Ghana,Zimbabwe,Uganda, South Africa, kwa sababu ya mfumo bora wa elimu.
Hata mikataba ikiwa haina dosari katika muundo wake itatekelezwa na watu gani upande wa Tanzania, umewaandaa kiasi gani?

Jambo la pili uroho wa kula bila kunawa.
Uroho wa watu wachache unawapa concessions nyingi wawekezaji bila kujali maslahi ya taifa.
Kampuni kongwe kama SHELL yenye uzoefu wa kuchinja nchi changa kwenye mikataba ya mafuta na gesi,itakuwa jambo la ajabu sana kama Tanzania itaibuka Mtakatifu.

Kwenye shughuli ya uchimbaji wa mafuta tokea mwanzo wake hakuna Mtakatifu ni ujanja kuwahi.Unakuta mtu alianzia ngazi ya chini akafanya kazi kwenye ring ,akapanda hadi ngazi ya OIM huyo ni Offshore Installation Manager ni Engineer mbobezi harafu labda anajiongeza anasomea sheria na marketing ya mafuta na gesi.Unakuja kukutana nae katika Negotiation table ya watu sampuli hiyo wapo 6 tena wenye uzoefu na nchi za Afrika katika uchimbaji wa gesi na mafuta na upande mwingine wasomi wetu tuliowabumba kutoka katika vyuo vyetu,unategemea nini kitatokea?

Tukiwa wawazi na kukubali kuondoa mapungufu yetu kama taifa,tutaibiwa miaka 20.Lakini tukifanya much know na huku tunaficha weakness zetu kwa visingizio lukuki tutapigwa miaka 50 hadi 100
 
Back
Top Bottom