Jesca Kishoa kwa hili la kumkosoa Kafulila hadharani na kufuta picha zake kwenye mitandao yako ya kijamii, umekosea

nyamakonge

JF-Expert Member
May 28, 2013
363
130
Wanabodi nachukua fursa hii kuwatakia afya njema. Nami naomba nichukue fursa hii kutoa maoni yangu juu ya yale aliyoyazungumza Mh. Jesca Kishoa mbunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA na mke halali wa mwanasiasa David Kafulila.

Mapema katikati ya wiki hii David Kafulila ambaye alikua mwanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo alitangaza uamuzi wake wa kujitoa kwenye chama hicho akidai kimepoteza dira katika kupambana na ufisadi.

Kafulila awali alikuwa mbunge na kada wa NCCR Mageuzi kabla ya kujiunga CHADEMA. Kafulila na Jesca wamefunga ndoa na kubahatika kupata mtoto mmoja.

Kuhama kwa Kafulila ni moja ya haki yake ya kikatiba bila kuangaliza sababu alizozitaja. Kilichonifanya niandike ni hiki sasa mara baada ya Kafulila kuhama mke wake Bibi Jesca Kishoa aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kukosoa uamzi huo wa mme wake hadharani huku akienda mbali na kuponda sababu zilizomfanya ahame. Jesca hakuishia hapo amediriki kubadili account zake mitandao ya kijamii kwa kutoa picha zote za mme wake na kubadili jina ambapo awali alikua akijiita Jesca Kafulila.

Kama mzalendo na mpenda taifa hili nimejiuliza hatua hii ya mke wa Kafulila ni ya nini? Yaani sisi kama taifa tumefika sehemu mpaka mambo ya kisiasa yanatugawa hadi kwenye familia?

Hata kama Jesca hakuridhishwa na uamuzi wa mme wake alitakiwa amuunge mkono kwa uamzi wake ambao ni halali kikatiba na kumpa moyo wa kusonga mbele na kumtaka wapambane kwa hoja sasa. Lakini kitendo cha yeye kuitisha mkutano na wanahabari na kumkosoa mme wake kimemfanya aonekane bado sio mkomavu kisiasa.

Na kama hali ndio hii itafika wakati ili kuoa utakua unaulizwa chama cha kisiasa unachokikubali ni kipi ndio unaruhusiwa kuoa/kuolewa. Tusifike uko kama taifa tuanze kukataa hizi chuki zinazotaka kutugawa .

Wasalaaam
 
Mkuu umeeleza vizuri kabisa, mambo ya kisiasa hayapaswi kufungamanishwa na family kabisa......namna huyo mbunge wa viti maalum alivyokurupuka kukomenti juu ya mmewe kubadili chama (haki yake kikatiba) ameonesha aina ya wabunge hasa wa viti maalum tulionao.......hewa kwelkwel!
 
Kiuhalisia Bi Jesca Kishoa yupo sahihi tena ikiwezekana hata papuchi asimpe kabisaaa,kwanza alimvumilia sana hakuna kitu kinauma kama mtu wako kufananishwa na mnyama "TUMBILI" yule mama alivumilia sn ss unamvumilia tumbili wako then anakuja kununuliwa kindezi c ndio mambo ya kuja kuiuza familia nzima na mke wako?Mwanaume lazima uwe ngangari na usitetereke ss huyu tumbili kanunuliwa mke amfagilie ili iweje?
 
Mwanamke ndiye anayelisha familia kwa sababu Kafulila hana kazi ni jobless, na ajira ya mke ipo Chadema sasa hapa wala huitaji degree kugunduwa Kafulila ni mpumbavu wa kwanza maana wa mwisho ana nafuu.

Kwanza wanaume wa kumuoa huyo Jesca tupo tumejaa tunamuomba Tumbiri atowe talaka haraka ndio atajuwa kumbe hata muuza kahawa naye anaendesha chombo cha moto.
 
Yule Mwanamke ni mpuuzi sana kwa kitendo alichokifanya.... labda kama wamepanga na bwanaake kuwazuga Chadema.

Mwanamke alieapa Kanisani kuwa atakuwa na Mmewe kwa shida na raha hawezi kufanya ujinga kama ule.

Nina wasiwasi huyo Mwanamke alishakuwa na kidume nje, Kafulila anachapiwa bila kujua.
 
Back
Top Bottom