Uchaguzi 2020 Jesca Kishoa Kafulila kuchukua fomu kugombea Ubunge CHADEMA Iramba ni kejeli na dharau kama si matusi kwa vijana wenzako

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,159
9,360
Awali NI kupongeze Sana,kwa kitendo chako Cha kijasiri kuwa licha ya changamoto na matatizo lukuki iliyopitia CHADEMA umebaki imara!

Ni lazima nikusifu kwa kuwa hats ndani ya familia yako changamoto hizi zilitamalaki. Hongera Sana!

Ni bahati mbaya sana huku ndani JF tunatumia majina bandia. Mimi Ni mshiriki was Siasa za Iramba Magharibi nyuma ya jukwaa. Nikiamini kuwa hakuna mbadala wa kichocheo kikubwa Cha Maendeleo zaidi ya Utawala Bora, kwa msisitizo Good Gorvanance.

Mdogo wangu Jesca, nimekupongeza kwa ujasiri wako kuwa bado upo CHADEMA naomba pia nikupongeze pia kuwa mwaka huu pia umeamua kugombea Ubunge Iramba Magharibi.

Kwangu Mimi pongezi hizi za pili ni muhimu zaidi kwa kuwa nimeshangazwa kuwa eti umerudi like ulipokutelekeza.

Kisiasa hili linawezekana kwa kuwa nyie wanasiasa Front Liners huwa mnajali zaidi : Unapata Nini, Wapi na Njia gani utatumia kupata hicho

Jesca unakumbuka Hali ya kiafya uliyokuwa nayo katikati ya Kampeni Mwaka 2015? Unakumbuka kuwa Kuna watu walikuwa wanakufanyia Kampeni kwa niaba yako kwa maana uliwalipa?

Jesca unafahamu pia kuwa kuna kundi lingine lilikuwa mbele yako likikupigania wewe na CHADEMA bila kujali kuwa unawalipa, mnafahamiana au la?

Watu Hawa walitoa muda, rasilimali zao kuhakikisha kuwa Unapata kura zile kwa jasho na damu. Unafahamu Siasa za kishamba na kipumbavu anazofanya Mwigulu kwa maana hiyo Vijana wengine walihatarisha maisha yao kukupigania?

Jesca unafahamu Kuna watumishi wa umma walikuwa wanatoroka kazini kutoka mikoa ya mbali kwenda kusaidia CHADEMA na wewe haujawahi hata kutaka uwafamu?

Je, baada ya jitihada hizo zote ambazo bila Shaka zilikupa Ubunge wa Vitu Maalum uliufanyia nini Iramba?

Uliweka misingi gani ambayo CHADEMA ingejivunia baadaye?

Hivi uliwahi hata kuhudhuria vikao vya Madiwani uwakilishe mawazo yako kule huku ukijenga Chama. Sina uhakike Kama ulienda hata kuapishwa.

Jesca umwahahi kutembelea mara ngapi matawi ya CHADEMA, umefanya nini kupitia Ubunge wako kuhakikisha unaimarisha Chama huku vijijini?

Kuna kundi la watu huwa lina amini kuwa wanasiasa siasa ni ujanja ujanja na usanii penginekwa kuwatumia wajinga ili wao, wanasiasa waendelee kula. Watu hawa wanaweza kutumia mfano wako kujenga hoja zao.

Kwa mapenzi niliyo nayo kwa Siasa mbadala naomba niishie hapa. Kwa misingi dhaifu uliyoweka unachofanya ni ku bet ili vyovyote itakavyo kuwa urudi tena kula kwa Viti Maalum.

Vijana na pengine wazee watakao kuwa mnakimbizana na kumpigia kelele Mwigulu na CCM Wana machungu mioyoni mwao Ila hawana jinsi wanajua wewe ni mnufaika wa Mbichi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamiii, una nukia waridi bila shaka na wao mpaka Oktoba nao watahisi hako ka waridi

All the Best Dada!
 
Hawa ambao upande mmoja tayari wameshajipaka rangi ya kijani (CCM), sio wa kuwaamini sana ndio wale watakaokuja kuanza kujiuzulu na kudai wanaunga mkono juhudi! Pia hata mazingira aliyokuwa nayo Kafulila (mumewe) mwaka 2015 si sawa na ya sasa, uwezekano ni mkubwa sana akasaliti upinzani katikati ya mhula! Hawa watu wa type hii ni bora CHADEMA ingewafagia wote!
 
Nawe mwambie mkeo achukue fomu,ni haki yake acha wapiga kura na chama chake kiamue
Kulia lia mitandaoni hakukusaidii
Kiongozi ukikuta Filsofa wanajadili Mambo kaa kimya sikiliza!
Unaonesha ujinga wako bila sababu..sisi ndio wapiga kura wa Iramba !
Na Jesca anaelewa NILICHOANDIKA!
 
Mume wake ni RAS sidhani kama atadumu CDM, CDM watafute mtu mwingine tofauti ya huyu muda wowote ataunga mkono juhudi.

Huyu atagombea hili amwachie Mwiguru Hilo Jimbo... Hatofanya kampeni ili ashinde atafanya usanii ili Mwiguru apite kiulaini...

Chadema wasikubali kumsimamisha huyo mgombea watafute mtu mwingine machachari...
 
Back
Top Bottom