Jesca Kishoa Kafulila aibua ufisadi mwingine kampuni ya Shell

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
kutano uliopita niligusia hapa kuhusu kuvunjwa kwa sheria Finance Act 2012, kifungu cha 29, kinachosisitiza uhamishaji wa shares usifanyike bila malipo ya kodi ya ongezeko la mtaji( capital gain tax), lakini kampuni ya shell imekwepa kodi ya zaidi ya $500m, kiasi ambacho ni zaidi ya trilioni1. hiki ni kiasi kikubwa kinachoweza kujenga reli hiyo ya kisasa kutoka Dar mpaka Moro lakini kwasababu ya vigogo wasiogusika TRA, FCC na serikali kwa ujumla, nchi inapoteza fedha hizo. Huu ni ufisadi mkubwa na sintomwelewa JPM kwa kuachia mamlaka husika bila kuzichukulia hatua kwa kosa la kuruhusu umamishaji wa sheres kabla ya malipo ya kodi hiyo kufanyika kinyume cha sheria ya fedha ya 2012,kifungu cha 29.

[HASHTAG]#Nasema[/HASHTAG] haya kwasababu kampuni hii ya Shell ni very corrupt, juzi hapa imetajwa kwenye majarida makubwa duniani ikiwemo mtandao wa Global Witness kwa rushwa ya $1bn , zaidi ya shilingi trilioni2 huko Nigeria kwa vigogo wa serikali hiyo ili kufanikisha biashara zake. Nani ataamini kama ukiukwaji huu wa sheria hii hapa kwetu haujafanyika kwa nguvu ya rushwa?Utawala bora upo wapi hapa?

# Nataka majibu kuhusu ufisadi huu, maana mkutano wa Januari nilihoji kwenye Kamati ya walipokuja watu wa Fair Competition Commission(FCC), nikawahoji kwann ufisadi ulitokea, wakashindwa kujibu na kuahidi wangejibu kwa maandishi baadae leo tunaelekea nusu mwaka hawajajibu.

# Niliwandikia barua rasmi TRA kutaka maelezo ya ufisadi huu kwa mujibu wa sheria ya Haki, Kinga na Mamlaka ya Bunge ya mwaka 2002, kifungu10, kutaka wanipe taarifa ya kwanini jambo hili limetokea, leo ni mwezi zaidi umepita bila majibu. Na hata Nilipochangia bungeni Januari mwaka huu, Waziri wa Nishati alijibu akikiri tatizo bila kutoa majibu ya kwanini sheria hii imevunjwa. Nataka Serikali hii inieleze kwanini ufisadi huu umetokea na wahusika hawachukuliwi hatua?
 
Jeska Kishoa- Just for matter of curiosity, Je Kampuni ya Shell bado ina operations zake nchini Tanzania? Over recent past bithaa zake zikiwepo mafuta, lubricants, hazionekani sokoni? Unaweza kuelezea kidogo kuhusu hii capital gain tax ambayo umehusisha shell na share transfer inahusika na transaction ipi tujue? The fact kwamba FCC wamehusishwa hapo ina maana kuna acquisition inayohusisha kampuni hiyo- please be precise!
 
Jeska Kishoa- Just for matter of curiosity, Je Kampuni ya Shell bado ina operations zake nchini Tanzania? Over recent past bithaa zake zikiwepo mafuta, lubricants, hazionekani sokoni? Unaweza kuelezea kidogo kuhusu hii capital gain tax ambayo umehusisha shell na share transfer inahusika na transaction ipi tujue? The fact kwamba FCC wamehusishwa hapo ina maana kuna acquisition inayohusisha kampuni hiyo- please be precise!
Yes wana operation offshore oil drilling .. Ndio walinunua BG ..
 
Mleta hoja sijamuelewa kabisa. Taarifa nusunusu. Shell kauza shares kwenda kwa nani? Shell wameuza shares kiasi gani mpaka kodi tu iwe Usd500Million? Mwaga mtama hapa uwanjani .
 
Yaje majibu siyo maswala ya kijinga maana walamba viatu wameanza kuikwepesha hoja
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom