Jesca Kishoa awasirisha kwa Tundu Lisu taarifa ya unyang'anyi wa viwanja Singida

KALEM B

Member
Dec 31, 2012
51
0
Mwanadada machachali wa chama cha democrasia na maendeleo bi Jesca kishoa maarufu kama (Iron Lad) jana tarehe 12.12.2013 amekamilisha na kukabizi taarifa ya uchunguzi wa unyang'anyi wa viwanja unaofanywa na mkurugenzi wa manispaa ya singida katika taarifa hiyo iliyoambatanishwa na miktasari ya vikao vilivyokaliwa na waanga wa tukio hilo imemtaja mwenyekiti wa ccm mkoa wa Singida kuhusika na uharamia huo ambapo wajumbe wamedai m/kiti huyo bwana Mgana msindai akishirikiana na mkurugenzi wa manispaa bwana Joseph mchina waliwahadaa wananchi na kuwataka wahame wakidai ni eneo la wazi na baadae wakamuuzia bwana Akwii mfanyabiashara wa mkoani hapa mwenyekiti wa ccm amekua na tabia ya kuingilia majukumu yasio yake kila wakati ususani kwenye mambo haya ya viwanja,itakumbukwa kua yeye ndiye alisababisha Singida kuwe na stand bubu nyingi baada yakuwaruhusu wenye mabasi kitendo ambocho mbali na kuweka mji katika mazingira machafu lakini pia inapoteza mapato ya manispaa kwa magari kutokufika stand kuu na badara yake mapato kwenda ccm kwa stand bubu kua nyuma ya ofisi zao
 

Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,447
2,000
CCm inanuka rushwa na dhuluma kila kona ya nchi
Utendaji wa nchi hii imefikia kikomo watendaji hawajitambui kwa kweli
Wabunge wana lalamika, mawaziri wanalalamika, na hata Rais analalamika
Juzi wabunge walisema wenyewe wananchi sasa inabidi tuamue wenyewe kuona ni yupi anayefaa kutuongoza
Hospital matatizo, wakina mama na watoto wanalala chini hadi leo,
mashuleni ndo usiombe kuna shule ukienda hata darasani unaogopa kuingia
Ukienda sokoni utawakuta wakina mama wanakimbia huku na kule eti wanakimbizwa na watoza ushuru
mama huyu kapeleka ndizi ya 2000 anatakiwa kulipa 500 alafu wakati huo huo hakuna kinachoendelea
Maendeleo ni duni, toa hiyo 500 alafu upate hata uduma dispensary nothing
narudia tena serekali hii imefikia kikomo haistahili hata kidogo kuendelea kuwa madarakani
 

MAPUMA MIYOGA

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
3,774
2,000
Kuna magamba bado yataona hii taarifa sio sahihi na ni kutafuta umaarufu, ila ukweli ndio huu maana naijua SGD.
 

Bulesi

JF-Expert Member
May 14, 2008
8,647
2,000
Nani asiyejua ufisadi wa Mgana Msindai tangu enzi hizo akiwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya serikali za mitaaa; huyu mzee ni jangili wa kutupa na kumpa uenyekiti wa Mkoa ,ccm imejipaka najisi!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom