Jesca Kishoa aibua ufisadi mwingine wa shilingi Trilion 1.3 sakata la SONGAS

sasa kama mkataba ni wa 2004 alikuwa wapi kusema aje kusema sasa?
na kwa nini akimbilie bunge la awamu ya tano kuwa dhaifu? bunge la awamu ya nne limekaa na huu mkataba mbovu kwa nini haliitwi dhaifu?
Maswali yako yadhihirisha udau wa upande fulani, conflict of interest. Hakuna muda mahususi wa kuibua uhalifu. Hoja ya msingi ni ushahidi wa tuhuma. Tusikubali kila tuambiwalo bila udadisi. Lakini watoto, wajukuu ,vitukuu na vilembwe, vitashindwa hata kuenzi makaburi yetu kwa matatizo watakayo kuwa nayo kiuchumi kwa sisi kutohoji maswala ya msingi.
 
Dahh...

Hii ngoma itakuwa ni ya BENI hii na alishasema tuwaache wapumzike.
 
Sawa ufisadi huu ushuhulikiwe.Lakini hiyo isiwe sababu ya kutusahaulisha ile 1.5 trilion,na kishika uchumba chetu kutoka ACACIA

Ila hayo maelezo ya ziada ya kuhusu ndoa yake yanaleta ukakasi,sababu hayahusiani na hoja aliyoileta mezani

Alafu kuwa Mwanaharakati wa upinzani alafu mumeo yuko chama tawala ambacho ni cha kidhalimu nayo inaleta ukakasi vilevile.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wanaoana watu wa dini tofauti ,wanaishi haileti ukakasi, nini vyama tofauti vya siasa !?
 
Mwanasheria wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini (before split) na wasaidizi wake pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wawajibishwe.
Mwanasheria wa iliyokuwa wizara ya Nishati na madini ndio kwa sasa amekuwa waziri wa Nishati.. Shamba la bwana kheri, mbuzi wa bwana Kheri basi yote kheri.
 
Songas amewekeza 27% lakini ana hisa 54%
Serikali imewekeza 73% lakini ana hisa 46%
Hii inaonyesha akili za serikali na bunge letu.
Kwa hesabu kama hii tokea 2004 hadi leo ni wazi kuna viongozi wanaonufaika na kikotoo hiki.
Ifike wakati viongozi wastaafu wasiruhusiwe kushiriki kwenye mambo ya kuongoza au kutoa ushawishi wa kisiasa.
Ni wazi mikono yao ni michafu na mzigo kwa taifa.
 
Mwanasheria wa iliyokuwa wizara ya Nishati na madini ndio kwa sasa amekuwa waziri wa Nishati.. Shamba la bwana kheri, mbuzi wa bwana Kheri basi yote kheri.
Duuu basi hapo ndiyo salute kubwa Mkuu.
 
Sawa ufisadi huu ushuhulikiwe.Lakini hiyo isiwe sababu ya kutusahaulisha ile 1.5 trilion,na kishika uchumba chetu kutoka ACACIA

Ila hayo maelezo ya ziada ya kuhusu ndoa yake yanaleta ukakasi,sababu hayahusiani na hoja aliyoileta mezani

Alafu kuwa Mwanaharakati wa upinzani alafu mumeo yuko chama tawala ambacho ni cha kidhalimu nayo inaleta ukakasi vilevile.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo ya ziada alikuwa anajibu maswali ya waandishi wa habari ...............!!
 
sasa kama mkataba ni wa 2004 alikuwa wapi kusema aje kusema sasa?
na kwa nini akimbilie bunge la awamu ya tano kuwa dhaifu? bunge la awamu ya nne limekaa na huu mkataba mbovu kwa nini haliitwi dhaifu?

Huo ni wajibu wa serikali yoyote, tena uzuri zote zilikuwa za ccm. Serekali hii ndio inasema inapambana na ufisadi, sasa inabidi tuone kwa vitendo.
 
kishoa.jpg

Waziri Kivuli wa Nishati Jesca Kishoa amshauri Spika wa Bunge kumuita mbele ya kamati ya bunge ya maadili Mwanasheria mkuu wa Serikali kwa kulidanganya Bunge na kushindwa kufanyia kazi taarifa za Ufisadi unaendelea katika mikataba ya kampuni ya kuzalisha Umeme wa Gesi ya SONGAS badala ya kumuita CAG Profesa Assad kwa kusema maneno ya ukweli..
.
Kishoa anatoa Rai hiyo jijini Dodoma ambapo amesema Ufisadi huo Unaendelea umebainishwa katika Ripoti ya CAG ya mwaka 2009 na ya mwaka 2018 ambapo mwanasheria mkuu wa serikali aliahidi mbele ya Bunge kua atalifanyia kazi ambapo mpaka sasa hajalifanyia kazi huku Bunge likishindwa kumuwajibisha.
Katika Ripoti hizo za CAG zilionyesha Tanzania mepoteza zaidi ya shilingi Trilion 1.3 na mikataba hiyo ikiendelea itapoteza zaidi hivyo Waziri huyo Kivuli pia ameomba Rais Magufuli kutumia Mahakama za Kimataifa katika swala hilo kama kwake limekua gumu ili kuokoa fedha za Watanzania
 
  • Thanks
Reactions: Gut
Mahakama ya mafisadi iliishia wapi?
Hivi kutetea mafisadi ni uzalendo?
 
View attachment 994866
Waziri Kivuli wa Nishati Jesca Kishoa amshauri Spika wa Bunge kumuita mbele ya kamati ya bunge ya maadili Mwanasheria mkuu wa Serikali kwa kulidanganya Bunge na kushindwa kufanyia kazi taarifa za Ufisadi unaendelea katika mikataba ya kampuni ya kuzalisha Umeme wa Gesi ya SONGAS badala ya kumuita CAG Profesa Assad kwa kusema maneno ya ukweli..
.
Kishoa anatoa Rai hiyo jijini Dodoma ambapo amesema Ufisadi huo Unaendelea umebainishwa katika Ripoti ya CAG ya mwaka 2009 na ya mwaka 2018 ambapo mwanasheria mkuu wa serikali aliahidi mbele ya Bunge kua atalifanyia kazi ambapo mpaka sasa hajalifanyia kazi huku Bunge likishindwa kumuwajibisha.
Katika Ripoti hizo za CAG zilionyesha Tanzania mepoteza zaidi ya shilingi Trilion 1.3 na mikataba hiyo ikiendelea itapoteza zaidi hivyo Waziri huyo Kivuli pia ameomba Rais Magufuli kutumia Mahakama za Kimataifa katika swala hilo kama kwake limekua gumu ili kuokoa fedha za Watanzania

Sio bure, inaelekea kuwa kuna watu wakubwa/wazito sana ndani ya CCM wanaofaidika binafsi na ufisadi huu! Vinginevyo ungekuta hii ilisha vurumishwa kitambo sana!
 
sasa kama mkataba ni wa 2004 alikuwa wapi kusema aje kusema sasa?
na kwa nini akimbilie bunge la awamu ya tano kuwa dhaifu? bunge la awamu ya nne limekaa na huu mkataba mbovu kwa nini haliitwi dhaifu?

Udhaifu wa bunge uliotajwa haukuainisha kuwa ni bunge la awamu ya tatu , ya nne au ya tano. Hata hivyo hoja ni kuwepo kwa ufisadi
 
Back
Top Bottom