JERUSALEM: Fahamu kuhusu Ngazi isiyohamishika

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,684
8,833
FB_IMG_15753459283002795.jpg

NGAZI ISIYOHAMISHIKA.

Kwa wale waliobahatika kwenda kuhiji Jerusalem bila shaka watakuwa wanalifahamu kanisa kongwe la Sepulchre lililojengwa mnamo mwaka 326 likiaminika kuwa ndimo lilipokuwa kaburi la Yesu Kristo pamoja na eneo ambalo Yesu alisurubiwa. Ukitazama kwa makini katika moja ya madirisha ya kanisa hilo, utaona kuna ngazi. Ni ngazi iliyokuwepo hapo kwa zaidi ya miaka 250 kiasi cha kupewa jina la 'immovable Ladder' yaani ngazi isiyohamishika kwani imekaa hapo tangu mwaka 1757.

Sio kwamba imeshindikana kutoka, La hasha!!.ipo hapo kwa sababu maalumu, na huenda kuondolewa kwake kutaweza kuzusha hali ya machafuko ndani ya kanisa la Sepulchre au Jerusalem kwa ujumla kwasababu ngazi hiyo ipo hapo kwa sababu za kiimani na za kisiasa. Uwepo wa ngazi hiyo pale, ndio kuwepo wa amani na utulivu katika kanisa takatifu la Sepulchre ambalo limebeba 'historia ngumu lakini tamu' kiasi kwamba ili uweze kuielewa historia hiyo inabidi uanze kwanza kuielewa historia na matukio katika mji wa Jerusalem. Kabla hatujafika mbali, nikwambie tu kwamba kanisa hilo linamilikiwa na wakristo wa 'madhehebu zaidi ya matatu ingawa aliyekabidhiwa kushika funguo za kanisa hilo ni muislamu kutoka kwenye familia ya kiislamu.

Ndio!! Naona sasa unapata picha ya jinsi kanisa hilo lilivyo na historia ngumu. Na ugumu huo umesababishwa na historia ngumu ya mji wa Jerusalem, mji ambao kwa karne na karne umekuwa ukigombewa na madhehebu ya kidini huku kila dhehebu likijiona kuwa na haki na stahili ya kumiliki mji huo kwa imani kwamba hapo ndipo kulipofanyika matendo matakatifu ya mitume na manabii wao. Mfano;

'Wayahudi' huchukulia Jerusalem kama eneo ambalo Abraham alimtoa sadaka mwanae Isaka, eneo ambalo Daudi alianzisha mji, eneo ambalo mfalme Selemani, Zerubbabel na Herodi walijenga mahekalu na wanaamini kuwa bado kutajengwa upya hekalu lingine. Wakristo nao hupachukulia Jerusalem kama eneo ambalo bwana Yesu Kristo aliishi akifundisha, pia akafa na kufufuka hapo. Halikadharika waislamu nao hupachukulia Jerusalem kama mji wa tatu kwa utakatifu baada ya Mecca na Medina ambapo Mtume Muhammad alitua kusali akiwa katika safari yake ya Israa na pia hapa ndipo kwenye msikiti mtakatifu wa Alaqsa. Kwa kifupi niseme tu kwamba Jerusalem ni mji ulioteka hisia za waumini wa dini zote tajwa hapo juu, ndio mana migogoro ya kugombea umiliki wa maeneo ya Jerusalem umekuwa ni mkubwa kutokana na kila dini kupachukulia hapo kama mahala pake patakatifu.

Kwa muda mrefu sasa watu wa dini zote hizo wamekuwa wakiishi hapo Jerusalem licha ya mji huo kupitia vipindi tofauti tofauti vya kihistoria ikiwemo kuvamiwa na kuchukuliwa mateka na watu kutoka dola ya Ashuru 'Assyria' kabla ya kuvamiwa tena na wababeli, ujio wa wagiriki na waajemi, utawala wa dola ya Rumi, vita vya msalaba, utawala wa 'dola ya kiislamu ya Ottoman', kuanzishwa kwa taifa la Israel n.k.. Hayo na mengine mengi, yalichagiza kuwepo kwa mivutano hapo mjini Jerusalem nchini Israel/Palestina.

Moja kati ya maeneo ama majengo yenye mvutano mkubwa ni hilo ulionalo pichani. Hilo ndio 'kanisa takatifu la Sepulchre' au kwa kingereza tunaita Holy Church of Sepulchre. Historia ya kanisa hili imeanzia mwaka 326 wakati wa utawala wa mfalme Costantine wa dola ya Rumi ambaye aliamua kujenga kanisa hilo ikiwa ni baada ya kuitambua rasmi dini ya kikristo. Ifahamike kwamba, kabla ya kujengwa kanisa hilo, kulikuwepo na hekalu la kipagani lililojengwa na mfalme Hadrian wa dola ya Rumi kwa ajili ya kumtukuza 'Jupiter' mmoja wa miungu ya kirumi. Alipokuja Costantine aliamuru kubomolewa kwa hekalu hilo na kutangaza kuanza ujenzi wa kanisa 'Sepulchre' kwa ajili ya utukufu wa Yesu Kristo. Inaelezwa kwamba wakati wanafukua udongo kwa ajili ya ujenzi, wakaliona pango ambalo waliamini kuwa hapo ndipo lilipokuwa kaburi la Yesu.

Lakini kanisa hilo lilibomolewa mwaka 614 pale Jerusalem ilipovamiwa na dola ya Sassanid ingawa miaka 16 iliyofuata, mfalme Heraclius wa dola ya rumi alilikarabati upya kanisa hilo la Sepulchre.

Kuna kitu kinaitwa 'Religious Tolerance' yaani ustahimilivu hususani wa dini ya mwenzako. Mfano unapoona mtu wa dini moja, mathalani ya kihindu anaishi vizuri kwa amani na mtu wa dini ya kalasinga, hiyo ndio tolerance. Unapoona msikiti unajengwa kwenye jamii waishio wakristo na amani inatawala, hiyo ndio tolerance. Unapoona kiongozi wa serikali mkristo na anajumuika vizuri na waislamu, hiyo ndio tolerance. Miaka ya 638, Jerusalem ilitwaliwa na waislamu. Lakini aliyekuwa kiongozi wa kiislamu 'Khalifa Umar ibn Khattab' aliruhusu wakristo waendelee na ibada zao katika kanisa la sepulchre-kinyume na matarajio ya walio wengi ambao walidhani angeamuru kanisa kubomolewa. Huo ndio mfano wa uungwana na Religious Tolerance.

Na kuna stori inaeleza kwamba Askofu mmoja wa kanisa la Sepulchre alikuwa akimtembeza Umar kwenye maeneo ya kanisa la Sepulchre mara muda wa Khalifa kuswali ukafika. Askofu akaandaa pahala ndani ya kanisa ili Khalifa aweze kuswali. Ila Khalifa alikataa kuswali katika eneo la kanisa akisema kwamba endapo atafanya hivyo, wafuasi wake wangeweza kutafsiri vibaya kitendo hicho wakidhani kinalenga kugeuza kanisa kuwa msikiti, kitu kitakachozua mtafaruku. Badala yake, Khalifa alisogea hatua hache kutoka pale lilipo kanisa la Sepulchre na kisha kufanya swala katika eneo hilo ambalo miaka ya baadae palikuja kujengwa msikiti uitwao 'Masjid al Umar' kwa kumbukumbu yake.
Karne zikapita hadi ilipofika mwaka 1009 ambapo kiongozi (caliph) wa dola ya Fatimid katika kampeni yake ya kueneza uislamu, aliamuru kubomolewa kwa kanisa la Sepulchre ingawa baada ya mazungumzo na utawala wa dola ya Rumi mashariki (Byzantine), Caliph mpya aitwaye Ali az Zahir aliruhusu kujengwa tena kwa kanisa la Sepulchre ambapo ujenzi wake ulimalizika mnamo mwaka 1048 wakati wa utawala wa mfalme Constantine IX wa dola ya Rumi.

________
Naam, na hiyo ndiyo historia fupi sana ya kanisa tukufu la Sepulchre lililopo mjini Jerusalem. Katika sehemu ijayo utaona ni kwa namna gani kanisa hili linasimamiwa na madhehebu sita ya kikristo. Na ilikuaje hadi funguo za kanisa hilo hushikwa na muislamu. Pia tutaona ni kwanini ngazi ile haijahamishwa tangu mwaka 1757.
 
Hapo hapo kwenye uislam ulikuwa kabla hemu tuambie chanzo cha palestina ni nini sio yule mtoto wa mjakazi au sijaelewa
View attachment 1279988

Ni wanadamu walewale tu washenzi

Wanadamu wenye wivu hasira viburi roho mbaya,etc

Pamoja na kujaza chumvi sana hiyo historia,ni folklore tupu!
 
Usisahau kuni tag mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom