Mbunge Jerry Silaa aangua kilio bungeni baada ya kumaliza kuchangia mjadala

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mbunge wa Ukonga kupitia CCM, Jerry Silaa akilia baada ya kumaliza kuchangia mjadala wa kupitisha makadikio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Jijini Dodoma leo.

Silaa amemwaga machozi akieleza kuwa Kampuni ya Syno Hydro iliyopewa zabuni ya kujenga barabara ya mwendokasi kuanzia Kariakoo hadi Gongo la Mboto Jijini Dar es salaam imevurunda katika miradi mingine.

Mbunge wa Mbulu Vijijini kupitia CCM, Flatei Massay, yeye aliamua kuruka Sarakasi ikiwa ni njia ya kuonyesha hisia zake kwa kero ya kutokuwa na barabara ya lami jimboni kwake. Jerry Silaa aangua kilio. Flatei Sarakasi. Kulikoni kwa hawa wabunge?

Screenshot_20220523-133638~2.jpg
 
Wanafiki tu hao!

Mimi mwananchi wa kawaida ninaenunua material za ujenzi kwa bei kubwa huku mtaani silii ila huyo bwege marupurupu na mikopo kibao akisema ghorofa iote leo inaota anajifanya kulia.

Labda alisoma text kutoka kwa mkewe akimtishia kumuacha but kusema amelia kwa sababu ya wananchi huo ni uongo.
 
Jerry mara nyingi huwa yuko upande wa wananchi mkuu.

Na ndiyo maana hata kipindi malalamiko ya wananchi kudai wabunge wapunguziwe mishahara na posho wabunge wote walikataa isipokuwa yeye ambaye aliunga mkono matokeo yake akaishia kupigwa ban kuhudhuria baadhi ya vikao vya bunge.

Sasa sijui ulitaka amjengee kila mwananchi nyumba ili uamini kuwa angalau kuna muda huwa yuko upande wa wananchi.

Wabongo bhana msipopiganiwa haki zenu mnasema viongozi mafisadi mkipiganiwa haki zenu bado mnasema viongozi wanafiki na ndiyo maana viongozi wengi wameona wajiangalie wao na familia zao tu maana wabongo hamna jema.

Lazima mjue siyo viongozi wote wapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi wapo ambao wana uchungu na wananchi.
 
Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa akilia baada ya kumaliza kuchangia mjadala wa kupitisha makadikio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Jijini Dodoma leo.

Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay yeye aliamua kuruka Sarakasi, Jerry Silaa aangua kilio..Kulikoni kwa hawa wabunge?View attachment 2235484
waigizaji tu hao!!msiwaamini hata kidogo
 
Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa akilia baada ya kumaliza kuchangia mjadala wa kupitisha makadikio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Jijini Dodoma leo.

Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay yeye aliamua kuruka Sarakasi, Jerry Silaa aangua kilio..Kulikoni kwa hawa wabunge?View attachment 2235484
Bungeni siku hizi ni mahali pa kuonesha pia kipaji cha usanii!! Hili ni jukwaa la bure na lina watazamaji wengi!! Pinda pia alilia!! "wapigwe tu"
 
Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa akilia baada ya kumaliza kuchangia mjadala wa kupitisha makadikio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Jijini Dodoma leo.

Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay yeye aliamua kuruka Sarakasi, Jerry Silaa aangua kilio..Kulikoni kwa hawa wabunge?View attachment 2235484
Hawa Wambulu/ Wairaqw wanatufanya mazuzu
 
Back
Top Bottom