Jerry Silaa kupelekwa Bungeni na Karandinga ya Polisi, mashtaka yake kuongezeka hadi kuwa matatu

Jerry Silaa ambaye ni mheshimiwa mbunge wa ukonga kwa tiketi ya CCM, leo saa 4 asubuhi anatazamiwa kuletwa mbele ya kamati ya maadili ya bunge akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Aidha, mashtaka ya Jerry Silaa sasa yatakuwa matatu

1. Kusema uongo

2. Kuvunja heshima ya Bunge

3. Kudharau wito wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge

Ngoja tuone.

Updates;

Angepigwa fimbo kali kaliii kama 5 hv za makalio angekuwa na adabu huyu, amelidharau sana bunge..
 
Anza na mshahara wa Rais huo hata mia haukatwi na huku anajiita mzalendo
Tena yeye ndiye alitakiwa awe mzalendo number moja. Mshahara wake mkubwa huku matumizi aliyonayo ni madogo. Sehemu kubwa ya mahitaji yake tunamhudumia sisi halafu bado kidogo tunachobakiwa nacho baada ya kukatwa, tunaenda kufyekwa tena kwenye VAT na TOZO mbalimbali.

Yaani kila kona ni pesa inaporwa tu. Ukinunua fuel kwenye gari, panga.
Ukija kwenye parking ya gari hiyo hiyo, panga. Kiujumla pesa zinakwenda kuwahudumia wao huko.

Ukiangalia gari ya serikali inaachwa silence muda mrefu bila kuzimwa na kiyoyozi juu, wakati kiongozi yuko jukwaani, ni pesa yako inaungua. Hapo ukijumlisha msururu mkubwa wa magari kwenye huo msafara.

Wangetusaidia watanzania kwa kupunguza baadhi ya kodi na kubana matumizi huko serikalini.
 
Aisee cheki hiyo pic

IMG-20210827-WA0000.jpg
 
Kuhojiwa na Kamati hakuhitaji kwenda na mwanasheria, kwasababu hii sio mahakama ni just a quasi judicial body na ilipaswa kuishia kwa wabunge tuu. Hii ya Bunge kuwahoji watu nje ya Bunge kama mimi nilivyo itwa ni kinyume cha justice system yetu!.
Bunge limejiinua mno hadi masikio kutaka kushinda kichwa!.
P
Mkuu Pascal Mayalla Salam kwako. Kwa ulichoandika hapa, hao wakuu sana wanaweza kukuita tena.
Ahsante
 
Sasa akikatwa itaingia mfuko gani?
Ataachaje pesa anayolipwa kisheria?
Kitendo cha kupaza sauti tayari ameonesha nia njema
Mwalimu alijipunguzia 20% ya mshahara wake uliokuwepo kisheria bila kuibadili hiyo sheria..

Nimesema i'm not going to buy these derogatory dramas kama ameona mshahara haukatwi kodi aoneshe kwa mfano akipokea pungufu ndio wengine wafuate sio anasema kodi haikatwi then anatia mfukoni kitita kile kile..to me that is absolutely nonsense!
 
Tena yeye ndiye alitakiwa awe mzalendo number moja. Mshahara wake mkubwa huku matumizi aliyonayo ni madogo. Sehemu kubwa ya mahitaji yake tunamhudumia sisi halafu bado kidogo tunachobakiwa nacho baada ya kukatwa, tunaenda kufyekwa tena kwenye VAT na TOZO mbalimbali.

Yaani kila kona ni pesa inaporwa tu. Ukinunua fuel kwenye gari, panga.
Ukija kwenye parking ya gari hiyo hiyo, panga. Kiujumla pesa zinakwenda kuwahudumia wao huko.

Ukiangalia gari ya serikali inaachwa silence muda mrefu bila kuzimwa na kiyoyozi juu, wakati kiongozi yuko jukwaani, ni pesa yako inaungua. Hapo ukijumlisha msururu mkubwa wa magari kwenye huo msafara.

Wangetusaidia watanzania kwa kupunguza baadhi ya kodi na kubana matumizi huko serikalini.
Tatizo ni matumizi mabaya ya fedha za umma
 
Safari hii Ndugai amekosa wapinzani wa kukamata amenza kukamata watu wake
Roho ya ubaguzi, ndivyo ilivyo. Mbaguzi, huanza na Wahepele.(watu sa nao jina mimi ka nyumba ni kwake ambao hawamhusu. Mfano, mashemeji, watoto wa ndugu zake.).
Akisha watesa na kuwafukuza lazima atendelea na ubaguzi mpaka kwa watoto aliowazaa mwenyewe. Akimalizana na hao atmbagua hata mke wake mwenyewe.
Tusubiri yanakuja mengi tu.
 
Kuna waswahili wakiwa na vyeo na vihela huwa wanadharau na kujiona mno.

Mama samia shugulikia hao wasaliti endapo watakutwa na hatia.
 
Kuhojiwa na Kamati hakuhitaji kwenda na mwanasheria, kwasababu hii sio mahakama ni just a quasi judicial body na ilipaswa kuishia kwa wabunge tuu. Hii ya Bunge kuwahoji watu nje ya Bunge kama mimi nilivyo itwa ni kinyume cha justice system yetu!.
Bunge limejiinua mno hadi masikio kutaka kushinda kichwa!.
P

Mayalla, subpoenas of witness testimonies of private citizens by a legislative branch aren’t unique to Tanzania!

About two centuries ago, the powers of U.S. Congress to issue subpoenas, including subpoenas of witness testimonies of private citizens, were challenged in court. The dispute was resolved in favor of Congress, with the Supreme Court saying that in order to write laws Congress also needs to be able to investigate.

This power to issue subpoenas, while broad, is not unlimited. The Supreme Court said Congress is not a law enforcement agency, and cannot investigate someone purely to expose wrongdoing or damaging information about them for political gain. A subpoena must potentially further some legitimate legislative purpose.
 
Mayalla, subpoenas of witness testimonies of private citizens aren’t unique to Tanzania!

About two centuries ago, the powers of U.S. Congress to issue subpoenas, including subpoenas of witness testimonies of private citizens, was challenged in court. The dispute was resolved in favor of Congress, with the Supreme Court saying that in order to write laws Congress also needs to be able to investigate.

This power to issue subpoenas, while broad, is not unlimited. The Supreme Court said Congress is not a law enforcement agency, and cannot investigate someone purely to expose wrongdoing or damaging information about them for political gain. A subpoena must potentially further some legitimate legislative purpose.
Mkuu Pulchra Animo, kwanza asante kwa hii. Hata Bunge letu linapokaa kama Kamati Teule kama ile Tume ya Mwakyembe kuichunguza Richmond inakaa kama quasi judicial body na ili issue subpoenas kwa lengo la kufanya uchunguzi na sio kuhukumu.

Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, kazi za Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ni ku deal na wabunge tuu na sio sisi tusio wabunge. Kazi za kamati hiyo ziko nne, na zinawahusu wabunge tuu, akiwemo Spika na Naibu wake. Haiwahusu watu wengine wowote nje ya Bunge hivyo kitendo cha Spika kupeleka peleka watu wasio wabunge kwenye Kamati hiyo ni masikio tuu kuzidi kichwa! kwa Bunge kujigeuza a kangaroo court. Kazi hizo zimeainishwa kama ifuatavyo:

1. Kuchunguza na kutoa mapendekezo kuhusu masuala yote ya haki, kinga na madaraka ya Bunge yatakayopelekwa na Spika;

2. Kushughulikia mambo yanayohusu maadili ya Wabunge yatakayopelekwa na Spika; na

3. Kushughulikia shauri linalomhusu Mbunge anayewakilisha Bunge kwenye chombo kingine cha uwakilishi au Mjumbe wa Bunge la Afrika Mashariki.

Mahali pekee ambapo mtu asiye mbunge anahusika na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ni pale tu mtu huyo atakapojisikia kuwa amepata athari HASI kutokana na kauli au maneno au shutuma zilizotolewa Bungeni kumhusu yeye binafsi. Na ikitokea hivyo anaweza kupeleka malalamiko pamoja na maelezo yake ya kujitetea kwa Spika. Na taratibu za kufanya hivyo zimeainishwa.

Mtu atahusika kwenye shughuli za kamati ikiwa atajisikia ameathiriwa na matamshi ya huko mjengoni. Lakini sijawahi kuona fasili yoyote inayosema Bunge likihisi limekoswa na raia basi limwite raia huyo kwenye kamati ya maadili na kumweka kiti moto.

Mayalla, a 9 can be seen (and read) as a nine or a six, depending on where one stands!

Kwa mtazamo wangu, kuna vitu ambavyo private citizens wanaweza kufanya au kusema vikawa ndani ya uwezo wa hiyo Kamati kuchunguza. Kwa mfano, tuhuma kwamba wabunge hawalipi kodi ni tuhuma ambayo moja kwa moja inagusa madaraka ya Bunge, kwasababu hiyo tuhuma inaaminisha Bunge limetumia vibaya legislative powers zake kwa kutunga sheria mbovu inayowasamehe wabunge kulipa kodi. So, getting to the bottom of this allegation is within the powers of this Committee, even if the alleging party (Jerry Slaa) weren’t an MP.
 
Tunasema kitu kile kile, Kamati ya Bunge ni kwa wabunge, hao ni wabunge, hivyo this is their right forum, kitendo cha kuniita mimi nisiye Mbunge, ni u kangaroos court.
P
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom