Jerry Muro: Zitto Kabwe ana tatizo zito kichwani


AUGUSTINO CHIWINGA

AUGUSTINO CHIWINGA

Verified Member
Joined
Apr 23, 2017
Messages
167
Likes
521
Points
180
AUGUSTINO CHIWINGA

AUGUSTINO CHIWINGA

Verified Member
Joined Apr 23, 2017
167 521 180
ZITO ANA TATIZO ZITO KICHWANI

Na Jerry C. Muro
Dar es Salaam, Tanzania
28/10/2017

Kwako Zito Kabwe, naandika sio kama nakuchukia, Hapana naandika kwa kuwa nataka kukukumbusha jambo, kama ambavyo na wewe unatumia Nguvu kubwa Kuwakumbusha wananchi Kuhusu Takwimu na hali ngumu ya Uchumi, na mimi nimeona niandike kidogo kukukumbusha kuwa, Kwanza Hivi ACT-Wazalendo bado ipo? Umetoa taarifa ya Kamati kuu kwa waandishi wa Habari kuhusu Kusinyaa kwa Uchumi wa Nchi, Nimefurahi kuona mara baada ya wewe kuzungumza na Vyombo vya Habari ukijigamba kuwa hiyo Uliyosoma ni Taarifa ya Kamati kuu nikapigiwa simu na Mjumbe Mmoja wa ACT Wazalendo ambae yuko kwenye Kamati kuu akaniambia Naomba kunukuu " Ndugu Muro, hiyo taarifa ya Zito sio ya kamati kuu alishaandika akawatumia baadhi ya Wajumbe wasome pasipo kuruhusu hoja nyingine za wajumbe wengine zijumuishwe"

# basi na mimi kutokana na Ushahidi huo, nikajiridhisha kwa kiasi KIKUBWA Ndugu Zito nae ameamua "KUPIKA " taarifa ya Kamati kuu, anyway kwangu mimi MWIBA UNAPOINGILIA, ndipo hapo hapo MWIBA UNAPOTOKEA.

"ZITO HUNA LEGITIMACY TENA KISIASA, HIVYO HATA UNACHOKIANDIKA KINAKOSA LEGITIMACY PIA"

Najua wengi mtauliza naandika kama Nani,na namjibu Zito Kama Nani? Ila niwakumbushe tu Viongozi wa Serikali wapo ila wanaendelea na kazi za Ujenzi wa Taifa katika kuwatumikia wananchi na Sio "MABWANYENYE" niwatoe hofu naandika kama Kijana Mzalendo na Rafiki wa Zito Kabwe, mimi hapa nafanya tu kusafisha njia na kuwasaidia katika hatua za awali za kumjua Zito, ambae baadhi ya Rafiki zake kutoka Vyama vya Upinzani wanasema Huenda "AKILI" zake zimeanza kurejea, ila Naomba niseme Huenda ikawa Kweli ila zimerejea katika Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli ambae HAJARIBIWAGI.

[HASHTAG]#Zito[/HASHTAG] nadhani Unajua Mgogoro wako na viongozi wenzako wa Upinzani ulikuwa ni "UNDUMILAKUWILI" wako Mchana uko Chadema kisha usiku unakwenda kulala kwingine kwa maslahi na Tamaa zako, chadema walikubaini "WAKAKUSHUGHULIKIA " bahati nzuri uliwahi kuchomoko ukaepuka yale yaliyomkuta mzee wetu yule aliekuwa makamu mwenyekiti wenu zamani kwa sasa ni Marehemu.

[HASHTAG]#Zito[/HASHTAG] ukishakuwa na Tabia hii ya "UNDUMILAKUWILI" inakuwa kama Kilevi tu, Popote utakapokuwa hata kama nyumbani kwako au jimboni kwako, au kwenye Chama au mitaani lazima utaambatana na Tabia hii Naomba nikukumbushe kuweka Rekodi Sawa.

1. Ukiwa chadema ulikuwa "NDUMILAKUWILI" ulikuwa unapiga double double mchana chadema, usiku uko mitaa ya Lumumba WAKAKUTIMUA, nasubiria Tundu Lissu apone aje atukumbushe walivyo kutimua.

2. Ukaenda kule kwingine japo hukuingia ulianza kubeep , nako ukawa "NDUMILAKUWILI" wakastuka mapema wakagoka kukupa Chumba cha kulala wala korido ya kujiegesha.

3. Ukawa Kiongozi kwenye kamati ya Bunge kule ukawa "NDUMILAKUWILI" mchana mkitembelea miradi, usiku unakwenda kwa Wakurugenzi wakuu wa hizo taasisi na kufanya yako nadhani Unajua au unataka tumrudishe Mheshimiwa sana "balozi" kule aliko aje tumuulize kuhusu fedha za hifadhi ya mfuko wa taasisi yake?

4. Zito umeanzisha chama chako cha ACT-Wazalendo, hapa ndio nimechoka kabisa, chama ni chako wewe mwenyewe ila bado umekuwa "NDUMILAKUWILI" hata wa chama chako mwenyewe? Ngoja iko siku kina Profesor Mkumbo, na mama Mghwira watasema tu naamini WATASEMAsiku.

5. Hii ya Mwisho ndio kali ya mwaka, umekuwa "NDUMILAKUWILI" hata kwa ndoa yako mwenyewe? Brother najua mnaruhusiwa Kuoa hata wake wanne, iweje ndoa ya kwanza Ufunge kwa Mbwembwe hivyo halafu Ndoa ya pili Ufunge kwa *KIFICHO* kama sio muendelezo wa Tabia yako ya "UNDUMILAKUWILI" this is too bad kwa maisha yako.

Ukisoma hoja zote hizo hapo juu, zimenifanya niseme "ZITO HUNA TENA LEGITIMACY"

Sasa tuendelee na uku kwingine,

[HASHTAG]#Ukimsikiliza[/HASHTAG] Zito Kabwe Leo alivyozungumza na vyombo vya Habari, utaona Hasira zake za wazi dhidi ya Serikali ya Mhe Magufuli, hii inaacha maswali mengi sana hivi huyu Zito ndie yule aliemwambia Mhe Magufuli kuwa anajenga uchumi mzuri na analeta maendeleo?

[HASHTAG]#Zito[/HASHTAG] Kabwe amekuwa Kiongozi wa Kamati Nyeti za Bunge, amekuwa kwenye siasa za vyama vingi tena upande wa upinzani kwa maisha yake yote, pia Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo hivi anajua hiki anachokiongea kuhusu Uchumi wa Taifa? Hivi Zito ana taasisi ya kufanya utafiti kuhusu uchumi wa Nchi kuliko World Bank, IMF au Bank Kuu BOTau taasisi ya taifa ya takwimu?

[HASHTAG]#Zito[/HASHTAG] usitumie mwanya wa Hali ya taifa ya KIUCHUMIkatika kupitia kipindi cha Mpito kinachofanywa na Serikali na haswa katika Serikali ya Awamu ya Tano inayojenga misingi ya Uchumi wa Viwanda kwa kuondoa fedha Haramu kwenye Mzunguko zilizokuwa zinatumiwa na Mafisadi.

[HASHTAG]#Zito[/HASHTAG] huenda umefanikiwa kucheza na Akili za Marafiki zangu wa Kigoma ila KAMWE hutafanikiwa kuchezea akili za Watanzania, hivi nikuulize Tangu umekuwa Mbunge wa Kigoma katika maeneo tofauti mpaka Leo una jambo gani ambalo unaweza kujivunia kuwa umelifanya kwa wana Kigoma tukasema state of the art kutoka Kigoma?
-au unajivunua kuiomba serikali kukarabati uwanja wa Ndege ambao unaweza kutumia wewe mwenyewe na matajiri wachache uku wapiga kura wako wakipambana na Vumbi la barabarani kwenye adventure na Saratoga? Mshukuru Magufuli unaempiga vita kwa maslahi ya MABWANYENYE kwa kuendelea kukujengea barabara zote zinazounganisha Mkoa uliozaliwa na mikoa mingine
-Magufuli huyu unapambana nae juzi juzi ndie amekupa mradi mkubwa wa maji kuwai kuonekana katika Historia ya maisha yako.

[HASHTAG]#Zito[/HASHTAG] usigeuze tasnia ya Siasa nchini ikaonekana ya Hovyo kwa "TAMAA"zako za kisiasa, najua utajitokeza kujibu huu waraka kisha na mimi nitatoa ninayojua Relax, au unadhani hatujui?

[HASHTAG]#Zito[/HASHTAG] nikipata muda nitawakumbusha watanzania ile ziara yako ya Masomo kule Ujerumani ilikuwa na kitu gani nyuma yake, nadhani sasa ni wakati wa kuweka kumbukumbu Sawa kwa watanzania.

Sasa nimeamini ile kauli ya Kiongozi Mmoja Mkuu wa Chama KIKUBWA cha Upinzani nchini alisema Naomba kunukuu

"MPUUZENI HUYO ZITO, MANA ZITO SIO NDEGE WALA MNYAMA, ZITO NI POPO MCHANA YUKO UKU, USIKU YUKO KULE "

[HASHTAG]#sote[/HASHTAG] tunatambua Tanzania ni miongoni mwa nchi Changa ambazo zinakuwa vizuri KIUCHUMI, na katika ukuaji huu Changamoto hazikosekani, na tunapaswa kutatua changamoto zetu wenyewe kwa Lugha tunayoelewana wenyewe.

#Ni wangu mimi kitendo cha Serikali kutoa Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu zaidi ya Shilingi Bilioni 140 zitakazowanufaisha zaidi ya wanafunzi 20,000 wa vyuo vikuu nchini, kwangu mimi nikiwa kijana lazima nimpongeze Mhe Rais Magufuli kwa kuwatazama vijana katika jicho la kipekee zaidi

Nimalize kwa kusema tu, Mheshimiwa *Rais, Dkt. John Pombe Magufuli alishasema yeye HAJARIBIWI, wewe angaika tu, mwisho wa siku Ukiona serikali haikupi attention basi na wewe unaweza" KUJITEKA MWENYEWE" ukakimbilia kule Mombasa, nchini Kenya.

Nawatakia week end njema.

Jerry C. Muro
*Dar es Salaam, Tanzania*
*28/10/2017*
 
T

tajirijasiri

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
2,754
Likes
3,262
Points
280
T

tajirijasiri

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
2,754 3,262 280
Jerry C. Murro unatafuta cheo. Soon utapata ukuu wa Wilaya. Strategy zako ni kutembea na Bashite na kuponda Upinzani kwa Hoja mfu.

Usisahau kumshukuru aliyekuuzia vyeti.

Bashite na Jerry, ndege wafananao manyoya huruka pamoja.
Laana ya milele iwaangazie, mfe mmekenua.
 
Jerry santonga

Jerry santonga

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2014
Messages
574
Likes
408
Points
80
Jerry santonga

Jerry santonga

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2014
574 408 80
Weka audio kusoma kunachosa mzee
 
kobilo

kobilo

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2014
Messages
719
Likes
1,260
Points
180
kobilo

kobilo

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2014
719 1,260 180
Huyu jamaa atapata uteuzi mda si mrefu, jitihada zake zitaonekana soon
 
P

Pohamba

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2015
Messages
18,768
Likes
31,487
Points
280
P

Pohamba

JF-Expert Member
Joined Jun 2, 2015
18,768 31,487 280
Zitto anatumia taarifa ya kupika Eti ya Kamati kuu ya ACT kushutumu takwimu za Serikali Eti za Kupikwa!

Kwanza alete report ya Kamati kuu ya ACT isiyopikwa ndio atapata legitimacy ya kuongelea hayo Madai yake!

Uhamiaji Wamkumbushe Zitto Kama walivyomkumbusha Bashe akaufyata!
 
SDG

SDG

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2017
Messages
7,531
Likes
7,760
Points
280
SDG

SDG

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2017
7,531 7,760 280
Jerry amemjibu Zitto kwa hoja alizotoa leo?
 
N

Nguzomia

Member
Joined
Sep 30, 2017
Messages
81
Likes
129
Points
40
N

Nguzomia

Member
Joined Sep 30, 2017
81 129 40
Sijui kama itafikia siku niteuliwe kwa vyeo vya kisiasa kama DC, RC, DAS & RAS. Maana unahitaji kujipendekeza kupita kiasi, heri uwe msomi tu mzuri labda siku moja utakumbukwa kama hawa maProf, lakini design za akina Murro ni kipaji kwa kweli. Maana inabidi ujipendekeze hata kwa miaka zaidi ya 5 ili siku moja uambulie kuteuluwa ambapo pia unakuwa hujui utadumu kwenye nafasi hiyo kwa muda gani bila kutumbuliwa. KUJIPENDEKEZA HASA KWA WANAUME NI KIPAJI. Yaani hata kama ni chuki hizo ameshindwa kuona component ya uchumi kwenye press ya Zitto anakuja na hoja vya vyama! WATANZANIA HATUSHIBISHWI NA VYAMA
 

Forum statistics

Threads 1,249,966
Members 481,167
Posts 29,716,096