Jerry Muro ndiye DC pekee ambaye bado ana U-Sabaya USabaya?

Pamoja na aliyoyafanya Old Sabaya ambayo si mazuri ila amesalitiwa maana wapo wengi tu kwenye mfumo na Sabaya nikwasababu alikuwa mstari wa mbele......ila Sabaya akiamua kumwaga mboga unaweza kuta hakuna msafi hata mmoja
 
Mimi ni kada kindakindaki wa Chama cha mapinduzi lakini ningeomba katika andiko langu nichukuliwe kama mzalendo anayependa maadili ndani ya chama na serikali ya Mama yetu mpendwa. Kama DC Muro ana wapambe wake humu na itawagusa basi wacha iwaume lakini wajifunze.

Jerry Muro binafsi nimekua nikifuatilia kauli zake za kujiapia kupoteza watu wanaompinga yeye, kujiapia kutotangaza majina ya washindi wa uchaguzi, Yeye kama nani?wakati DC hatakiwi kukaribia milango ya vituo vya wapiga kura? Ndani ya CCM ni lini tutawamaliza kina Sabaya hawa ili chama hiki kiwe chama cha watu? DC anapata wapi ujasiri wa kuwaambia kinamama watabaki wajane? Yeye ataishi milele? Kwani mke wake hawezi kua mjane siku moja?

Ninamuomba Rais wangu kipenzi Samia Suluhu Hassan ambaye nimetokea kumwelewa sana kuliko Marais wote waliopita ukimtoa Mwl Nyerere, amtazame sana hatua kwa hatua ndugu Jerry Muro hata kwenye uadilifu wake juu ya usimamizi wa rasilimali za umma na utendaji wake kwa ujumla. Ni mtu ambaye mabega yako juu wakati wote, ndani ya chama hatutaki hii tabia na mwisho wake si mzuri.

Nimuombe tu DC Muro aache tabia hizi, serikali hii ni ya wananchi siyo yake. Wenye kutoa hukumu juu ya utekelezaji wa ilani ya chama ni Wananchi na siyo yeye. Asimwakilishe Rais wetu vibaya akalaumiwa.
alipewa u dc kwa influence ya makonda ,alikuwa anamwandika kwa kusifia sifa makonda.....akili zake zipo chini mnoooo
 
Wapi Makonda mtoto pendwa wa Mwendawazimu jiwe
Alikua anajiona Kama daslamu kaijenga yeye yule mshamba wa Kolomije,
Naomba mamlaka zimulike Kuna Kila dalili ubadhilifu alifanya,
Haiwezekani ndani ya muda mfupi amiliki Mali nyingi vile na experience ya kawaida hii kitu haiwezekani asilani Kwa mtumishi wa umma

Note Sina chuki na wivu Kwa mtu yeyote alifanikiwa,Wala Sina roho mbaya ya kumkandia jamaa kisa tajiri

Ila hapa tunataka tuweke mambo Sawa Ili vijana tukipewa dhamana tusiwe na tamaa za mafanikio ya haraka njia inayopelekea kufanya hujuma nyingi Sana Ili kujinufaisha matumbo yetu badala ya kujenga Nchi Kwa uaminifu ndipo mambo mengine yaje Kwa majaaliwa!
Halafu nisikie tena mtu anasimama hadharani na kusema eti mkuu wa Wilaya ndie Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya. Nitamuona kama mtu ambaye hajavaa nguo kutokana na haya yaliyotendwa na Sabaya, genge lake pamoja kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya
 
Sijawahi kumsikia akijisifu toka mwendazake aondoke, wewe utakuwa unakutana nae kwenye mambo yenu huko ndio anakutishia.
Wee, huyu Jerry aliingia kibabe nyumbani Kwa wakili merinyo bila kufata utaratibu, na akaumia maabavu na kuwaweka ndani( lockup) watoto wawili wa mh. Merinyo mbao nao ni mawakili. Haya yote aliyafanya baada ya hayati JPM kufariki.
 
Hivi kuna mtu alivuna na kupiga (Akitetewa na baba yake) kama Bashite awamu ya 5? Acheni unafiki nyinyi, mshahara wa mil 5 unawezaje kununua gari la zaidi ya mil 300, na hakununua gari moja!! Awamu hii ndiyo haina upigaji sasa, Kiongozi mkuu hana doa hata 1 la upigaji
Kafidishie gepu miaka 6 ya kibano cha ngosha ilikuwa si poa
 
Wee, huyu Jerry aliingia kibabe nyumbani Kwa wakili merinyo bila kufata utaratibu, na akaumia maabavu na kuwaweka ndani( lockup) watoto wawili wa mh. Merinyo mbao nao ni mawakili. Haya yote aliyafanya baada ya hayati JPM kufariki.
Duh, shutuma nzto..walimuacha salama kweli watafsir sheria hao?
 
Back
Top Bottom