Jerry Muro hana kesi ya kujibu, aachiwa aende zake

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetupilia mbali shauri la Msemaji wa Yanga, Jerry Muro kusikilizwa.
Kamati hiyo imesema hoja zilizotolewa ili kumuita Muro zilikuwa na mapungufu na haikuona kama kuna sababu ya kumuita na kumhoji.
“Kweli kamati ya maadili imetupilia mbali, ninaona ni ushindi kwa Wanayanga na ninawasamehe wote walionitesa.
“Huu ni ushindi wa Wanayanga wote, lakini wito wangu kwa sasa ni sote kuungana, kwa Wanayanga na TFF kwa ajili ya maendeleo ya soka nchini,” alisema Muro katika ujumbe wake mfupi.

Lakini Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Wilson Ogunde alisema TFF inapewa nafasi ya kumpa Muro wito mwingine kama utaona anatakiwa kweli kuitwa kwenye kamati hiyo.

"Kama TFF inahitaji aitwe tena, basi tuwape nafasi ya kumuita tena kwa barua nyingine ukiachana na ile ambayo ilionekana kuwa na mapungufu," alisema Ogunde.

Jerry aliitwa kwenye kamati ya maadili baada ya TFF kupitia katibu wake mkuu, Mwesigwa Celestine kumtumia barua hiyo ya wito ingawa nayo ilikuwa na mpungufu rundo kwani haikueleza hata anatakiwa katika kamati ipi.
 
mwesigwa na malinzi ni mabwanyenye yanayofuja mali za TFF na kuvuruga maendeleo ya soka kwa tamaa zao za kipumbavu kabisa.
 
Aibu sana. Kama Jerry Muro hajui bendera ya taifa inavosimamishwa (yaani rangi ya bluu chini) anawashinda viongozi wa soka hapo TFF, hili ni janga kwa taifa.
 
Huelewek umeandika nn...kajifunze kuandika kwanza ndo urudi tena kuchangia
 
Angalau huyo Muro kakumbuka bendera ya Taifa. Je hao wasioikumbuka kabisa, wakiwemo viongozi wa TFF?
 
mwesigwa na malinzi ni mabwanyenye yanayofuja mali za TFF na kuvuruga maendeleo ya soka kwa tamaa zao za kipumbavu kabisa.
Ile kauli ya Muro ya maiti kun'gan'ia mwosha inajitokeza hapa. TFF iwajibike kwa kutia hasara ya kuitisha Kkao kisicho na sababu, Kikao Hewa! Au ndio kujihalalishia mipango ya Eid el Fitr baada ya ile ya viingilio Mazembe - Yanga kubuma?
 
Itakua ndo mipango yenyewe maana yale mabwanyenye kwa uroho na kupenda vya dezo ni hatari
 
Aibu sana. Kama Jerry Muro hajui bendera ya taifa inavosimamishwa (yaani rangi ya bluu chini) anawashinda viongozi wa soka hapo TFF, hili ni janga kwa taifa.

Sio muda utalalama kwanini Muro hajaiweka bendera kwenye mlingoti wake maana mnatafuta sababu,ushawaona wale wanaojifunika mfano Mbwana na Ulimwengu je wanafuata mpangilio wa rangi au kwa Muro ndio tatizo.
 
Huelewek umeandika nn...kajifunze kuandika kwanza ndo urudi tena kuchangia
Ameeleweka mbona ,,ww ndo hujelewa na tatizo wa co uandishi ila ukifikiria ki mwendo kasi utaona kama haeleweki,,ngoja nikusaidie kukuelewesha,,jamaa hapo kamaanisha kuwa hiyo bendera alioishika jery muro amekosea kuishika kwa mtiririko wa rang zake kama inavyotakiwa hapo ilitakiwa rangi ya bluu ndo iwe down na co iwe juu kama yy alivyoigeuza ,
 
Sio muda utalalama kwanini Muro hajaiweka bendera kwenye mlingoti wake maana mnatafuta sababu,ushawaona wale wanaojifunika mfano Mbwana na Ulimwengu je wanafuata mpangilio wa rangi au kwa Muro ndio tatizo.
Tatizo la wanasiasa wetu ni kutetea ujinga kwa mahaba tu waliyonayo. Bendera ya taifa inapaswa kupewa heshima mkuu, sio tambara la kupeperushwa hovyo hovyo. Bendera yetu ina muonekano wake si vema kuiweka juu chini. Sawa?
 
Ameeleweka mbona ,,ww ndo hujelewa na tatizo wa co uandishi ila ukifikiria ki mwendo kasi utaona kama haeleweki,,ngoja nikusaidie kukuelewesha,,jamaa hapo kamaanisha kuwa hiyo bendera alioishika jery muro amekosea kuishika kwa mtiririko wa rang zake kama inavyotakiwa hapo ilitakiwa rangi ya bluu ndo iwe down na co iwe juu kama yy alivyoigeuza ,
Mkuu, JF sio wote 'great thinkers'. Kitu kiko dhahiri kabisa yeye hakielewi! Ila posti za siasa tena uchwara ndo anazielewa.
 
Back
Top Bottom