Jerry Muro analiaribu soka la Tanzania, wahusika mtazameni kwa umakini.

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,667
1,566
Huyu jamaa amekuwa anaongea saña wakati mwingine anaongea maneno ambayo si ya kiuana michezo.
Hivi karibuni ametokea kuiropokea TFF kuwa waliwafanyia makusudi katika maandalizi ya mechi yao dhidi ya Mo Bejaia iliyofanyika Algeria eti kwamba TFF ilificha vifaa ambavyo CAF walitoa kwa ajili ya mechi hiyo.
Leo ameibuka na kuilaumu tena TFF na Azam media kuwa wanawahujumu katika kuelekea mechi yao dhidi ya mazembe.
Kuna kipindi alionesha hadharani mbele ya vyombo vya habari kumnyanyapaa msemaji wa simba kutokana na hali yake (Albinism).
My take:
Huyu si mwanamichezo, wanaohusika naye hebu wamtazame kwa jicho lingine. Ipo siku atasababisha mgogoro ambao utalighalimu soka la Tanzania.
Ninaomba moderators uzi wangu huu uwekwe katika kumbukumbu,
 
Jenny Mro anasema Yanga mechi hii ni yetu na uwanja ni wetu, kwa hiyo tutakaa mahali popote uwanjani na kuwapangia wengine mahali tunapotaka. Sasa najiuliza, tangu lini Yanga wamekuwa wamiliki wa uwanja zaidi ya ule wa Kaunda?
 
Yan leo nimemsikiliza Jeri Muro ndio nikajua kweli Yanga waliingia chaka. Mm sio mshabiki wa simba ila Yanga wawe makin na huyu jamaa
 
Tatizo siyo JERRY MURO...tatizo ni wapenzi wa soka na watanzania kwa ujumla ambao hupenda kusikiliza masuala ya aina hiyo, wapenzi wengi wa soka wanapenda mipasho...kwa hiyo huyu dogo yeye anaangalia watu wanataka kusikia nini...Mimi nakuthibitishia kuwa JERRY MURO hivi sasa ni maarufu mno kutokana na kauli zake...Nenda kwenye vijiwe mbalimbali uone namna JERRY MURO 'anavyoenziwa'...utasikia watu wanasema umesikia JERRY MURO alivyowaumbua?? Wengine utawasikia wanasema ngoja niwahi kipindi cha michezo nikamsikilize JERRY MURO....Sasa whether JERRY MURO anaharibu soka ya Tanzania hilo linahitaji mjadala, lakini after a second thought, tangu lini soka la Tanzania likawa bora?
 
nimemsikia mara mbili akiongea kwanza aliongelea swala la kessy akiwaomba Simba wamruhusu lakini wakati huo huo akiwapiga simba mkwara atawashusha daraja msimu ujao wasipotoa barua hajui kwa maneno yake ni vigumu viongozi wa simba kumruhusu pia ameongelea swala la mashabiki wa yanga kukaa upande wowotehajui fujo yoyote ikitokea yanga wataadhibiwa ikiwezekana kuondolewa mashindanoni wote mnaomshabikia ndio mtakuwa wa kwanza kumlaumu pale yatakapotokea madhara
 
Yanga inabidi kuwa makini swala mashabiki kukaa upande wowote hii ni kuleta fujo isiyo lazima viongozi mjalibu kuwashauli mashabiki
 
Yanga inabidi kuwa makini swala mashabiki kukaa upande wowote hii ni kuleta fujo isiyo lazima viongozi mjalibu kuwashauli mashabiki
Mechi ni Yanga vs Mazembe, nani wa kuleta fujo? Simba muache ujinga wa kukariri kwamba kila mechi mna haki ya sehemu ya kukaa. Ninyi wang'oa viti wakubwa ndio vinara wa vurugu. Yanga wanajaribu kutuma mbinu za kimichezo tu, ili wa matopeni na akioli zao matope ni shida kwelikweli
 
Yan leo nimemsikiliza Jeri Muro ndio nikajua kweli Yanga waliingia chaka. Mm sio mshabiki wa simba ila Yanga wawe makin na huyu jamaa
Kwanini usiseme wewe sio mshabiki wa Mbeya City au stand united? Why umekimbilia kusema wewe sio shabiki wa simba?
 
Jenny Mro anasema Yanga mechi hii ni yetu na uwanja ni wetu, kwa hiyo tutakaa mahali popote uwanjani na kuwapangia wengine mahali tunapotaka. Sasa najiuliza, tangu lini Yanga wamekuwa wamiliki wa uwanja zaidi ya ule wa Kaunda?

Kaunda si Uwanja wa Yanga,Lile eneo OEVU na NEMC wanavuta kasi tu pale siku mtakuta pameporomoshwa
 
Mtoa mada unasema moderators wautunze uzi huu kwa ajili ya kumbukumbu, nikwambie tu umechelewa sana. Unabii kuhusu anguko la huyu mtu lilishatolewa zamani, na kama kawaida watu wakapuuza na wengine kuchukulia poa. Ila taratibu watu wataelewa tu na kwa bahati mbaya mashsbiki wake watakuwa ndio wa mwisho kumwelewa wakati itakuwa too late!
 
Back
Top Bottom