Jeraha la kisiasa ( political casuality) la Prof. Kitila Mkumbo kwenye kuwania Ubunge

Mjenga Nchi

Member
Apr 21, 2020
6
19
Joto la harakati za kupata ubunge limezidi kupamba moto miongoni mwa watia nia wa chama tawala pamoja na vyama vya upinzani.
Ni sarakasi , vitimbi na mnyukano vinaendelea huko majimboni.

Hapa nataka nizungumzie jimbo la Iramba Magharibi ambalo lipo chini ya Dr Mwigulu kupitia chama Cha Mapinduzi. Baada ya Dr Mwigulu kupigwa chini kwenye uwaziri ilikuwa ni hoja kubwa ya Prof Kitila kunyemelea jimbo la Iramba kwa kuwaaminisha wananchi kwamba Rais kamchagua yeye na Mwigulu hafai tena kuwa mbunge kutokana na utendaji wake kuwa mdogo.

Hii ajenda ilimsaidia kumnadi na kama ingekuwa ni kuangalia tathmini ta ushindi wa ubunge basi alikuwa na kama asilimia 50 ya kupata ubunge. Lakini kitendo cha Mwigulu kuteuliwa tena kuwa Waziri wa Katiba na Sheria limekuwa pigo kwa Kitila zile asilimia 50 zimeisha na kubaki asilimia 5. Ile nguvu aliyokuwa anaitumia kwamba Rais hamtaki tena Mwigulu imejibiwa na uteuzi.

Hili suala ni sawasawa na la Kenya kuhusu Hand shake kati ya Rais Uhuru Kenyata na Odinga kuwa pigo kwa Ruto katika kinyanganyiro cha kumpata atakayechukua kiti cha Urais.

Sasahivi wananchi wa Iramba wao wanamshukuru Rais kwa kumaliza uchaguzi wa Iramba. Maana wanasema tayari Rais wanaye na Mbunge wanaye walichobakiza ni kupata madiwani tu.

Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni, Uchaguzi wa leo wa kata ya Mtoa kumpata katibu wa chama cha Mapinduzi katika kata hiyo umevuta hisia za watu wengi baada ya kuonekana kuna ukinzani wa pande mbili kati ya wagombea ambao wanajulikana kuwa ni timu Kitila na timu Mwigulu. Kata hiyo ndio nyumbani kwa Prof Kitila. Kilichotokea mgombea wa timu Mwigulu kaibuka mshindi kwa ushindi mkubwa wa kura 61 huku timu Kitila akiambulia kura 9.

Wananchi wamechukulia huo ushindi kama ndio ishara ya uchaguzi wa kwenye kura za maoni. Watu wanajiuliza je kama kitila kaweka mtu wake kwenye kata ya nyumbani akapigwa chini je itakuweje akishindana kwenye kata za nje ya kwao.

Uchaguzi wa Mtoa na kitendo cha Mwigulu kuteuliwa kuwa waziri limekuwa jeraha kwa Prof Kitila pamoja na wapambe wake.
Ushauri mkubwa ambao anastahili kupata ni kuendelea kumpa moyo. Huku timu Mwigulu wanazidi kutamba kwa kusema matokeo ya leo ndio tafsiri halisi ya kumfuata mamba kwenye kina kirefu cha maji.

Je Prof ataendelea na harakati za kuutaka ubunge?
Lakini kuna mdau mmoja amezidi kuwa na iman na Prof kwa kusema kuwa wana imani naye ataweza kuwaletea maji...
Wengine bado wanamshangaa Prof kwa kuendelea kuwa kinyume na maagizo ya viongozi wa juu kwa kuanza kufanya kampeni mapema kwa majimbo ambayo wabunge wake ni wa chama cha Mapinduzi.

Wako
MJENGA NCHI
 
Mwigulu kwenye siasa za ubunge ananguvu sana

Huyo kijana anaushawishi sana kisiasa

Huyo ni born politician, kitila angegombea jimbo lingine singida au Arusha kwani wanautamaduni unaofanana
 
Cjui hao wabunge wa ccm wananchi wanawachagua ili wakafanye nn maana naona wote hufanya kazi ya kumsifia rais na kutukana wapinzan huku wananchi wakiendelea kuteseka na kero zilezile tangu Uhuru......

Wote wawili naona ni mambwa tu...
 
Hakuna hata mmoja kati ya waliotoka upinzani watapata Ubunge kupitia tiket ya CCm mwaka huu. Oct 2020 uchaguzindani ya CCM ni kati ya CCM asilia Na CCM wahamiaji. Wahamiaji walionjeshwa tamu ya mishikaki wakati wa chaguzi ndogo na si baada ya hapo/ oct 2020.

Si Mwita wala Kitila atakayekatisha hata kura za maoni.
 
Kitila ni mfa maji anatafuta pakutokea mwigilu sio size yake ni namba ya juu sana
 
IMG-20200519-WA0014.jpg
 
Back
Top Bottom