Elections 2010 Jennister Mhagama wa Peramiho kaikosea nini CCM?

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Jennister mhagama alifanya vizuri katika nafasi ya uenyekiti ndani ya bunge lililopita na aliendesha vikao vya bunge kwa mafanikio kuliko hata Job Ndugai na pengine kuliko hata Anne Makinda.

Mhagama alikuwa mtu wa kwanza kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya unaibu spika nami niliamini angepata nafasi hiyo bila wasiwasi. Ghafla nikasikia zengwe la jina lake kutaka kuondolewa, mara nikasikia ameondoa jina lake kwa kile kilichosikika kua ni kuleta uwiano wa kijinsia ambao hata hivyo umekuwa ukitafsiriwa ndivyo sivyo. Baada ya kuondoa jina lake nilitegemea angepewa uwaziri au unaibu waziri lakini cha ajabu nimeshuhudia sophia simba akipewa uwaziri wakati Jennister Mhagama akiambulia patupu.

Swali ninalojiuliza ni kwamba JE JENNISTER MHAGAMA SIO MWANAMTANDAO?

I SUBMIT...
 
Huyu mheshimiwa hakuwa mwanamtandao mwaka 2005 ila anastahili nafasi kwenye serikali ya JK kwani ameonesha ni mtu mwenye uwezo na ni mchapakazi mzuri. Bila shaka atakapofanya reshuffle anaweza kumkumbuka.
 
Never on this government. Huyu alitaka kuivua nguo serikali ya chama chake Bungeni. Na ndicho kinachoendelea!
 
uteuzi haukuzingatia sana uwezo vinginevyo akina hawa, sophia,george,makongoro wasingekuwemo. kuna factor zaidi ya uwezo. jenista ana uwezo mkubwa kuwazidi hao wote.
 
Bado ana nafasi ya kuchangia akiwa Mbunge si lazima wakati apewe uwaziri. Naamini kati ya wabunge 260 na zaidi waliopo wapo wenye uwezo mkubwa wa kuwa watendaji katika uwaziri pia lakini tukumbuke tunahitaji wabunge wazuri wajimboni wanaoweza kuhoji matumizi yasiyoeleweka, ya zima moto, na kinjaa njaa katika halmashauri zetu nyingi hapa Tanzania yeye atapiga mzigo huko.
 
SamirNasri kabla hujahoji kuhusu Jenista ulikuwa na CV yake au umefurahishwa na sura yake. Hao uliowataja wanaweza kuwa na utendaji wa mashaka hapa na pale lakini elimu yao imeenda shule. Mwalimu Grade A jamani naye tumjadili humu? Mimi nafikiri hata yeye mwenyewe anajua ndo maana hajalalamika.
 
Labda walimMUSORI kama yule mama wa umoja wa wanawake wa chadema! hivi ndio vyama vyetu vya kiafrika......
 
Sio mwanamtandao,kama mnakumbuka alivyombana Hawa Ghasia, kuhusu kupandishwa vyeo watumishi wa halmashauri
 
Kweli ana uwezo mkubwa wa kuendesha vikao. hilo la zengwe naweka zipu mdomoni
 
SamirNasri kabla hujahoji kuhusu Jenista ulikuwa na CV yake au umefurahishwa na sura yake. Hao uliowataja wanaweza kuwa na utendaji wa mashaka hapa na pale lakini elimu yao imeenda shule. Mwalimu Grade A jamani naye tumjadili humu? Mimi nafikiri hata yeye mwenyewe anajua ndo maana hajalalamika.

Kwa nini tusimjadili kama watu wameishasema ana uwezo? Kweli unathamini makaratasi kuliko ufanisi? Kwa mtaji huo hatufiki kokote na tutazidi kuwatetemekea hao maPh.D bomu!

Amandla.....
 
Mbopo na wenzako wenye mtazamo kama wako nikufahamishe kuwa elimu kwa maana ya chetu na utendaji ni vitu viwili tofauti. Unasema si vyema kumjadili Jenista kutokana na kuwa na elimu ndogo. Najua tatizo hapa ni kuwa unauelewa mdogo sana hasa kuhusu maswala ya uongozi.

Nikufamishe kuwa uongozi hauhitaji mtu kuwa na profession fulani au kifikia kiwango fulani cha elimu ili awe kiongozi mzuri. Mifano ni mingi sana ukianzia na Bunge la 9 Jenista kama mwenyekiti alifanya vizuri sana kuliko wenyeviti wenzake wawili pengine hata kumzidi Anne Makinda.

Kwanini Jenista hakupata uongozi nionavyo mimi ni kwamba ameonekana kuwa mkweli na labda professional zaidi. Mtu wa aina hiyo CCM hawamtaki asilani rejea swala la sita.
 
SamirNasri kabla hujahoji kuhusu Jenista ulikuwa na CV yake au umefurahishwa na sura yake. Hao uliowataja wanaweza kuwa na utendaji wa mashaka hapa na pale lakini elimu yao imeenda shule. Mwalimu Grade A jamani naye tumjadili humu? Mimi nafikiri hata yeye mwenyewe anajua ndo maana hajalalamika.

wewe una elimu gani, pengine tukianza classification tutakutenga kwa elimu yako nmkuu, hata kama una PhD!!!! umeongea kitu cha ajabu sana ambacho kwa haraka unaonyesha jinsi elimu yako isivyokusaidia duh!
 
SamirNasri kabla hujahoji kuhusu Jenista ulikuwa na CV yake au umefurahishwa na sura yake. Hao uliowataja wanaweza kuwa na utendaji wa mashaka hapa na pale lakini elimu yao imeenda shule. Mwalimu Grade A jamani naye tumjadili humu? Mimi nafikiri hata yeye mwenyewe anajua ndo maana hajalalamika.
0 out of 1 members found this post helpful. Thank you for rating this post!
Amen!
 
Back
Top Bottom