Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 653
- 1,058
Amini usiamini angekuwa ni Waziri Mwanaume pale asingedumu vile. Jenister Mhagama amedumu kwa sababu hakuwa na uwezo wa kutofautiana na Waziri Mkuu hata Rais kuhusu maslahi ya wafanyakazi.
Ni Waziri gani angekubali miaka mitano ya uongozi wake wafanyakazi wa nchi hii wasipate nyongeza ya mishahara? Ni Waziri gani huyo mwenyewe kujiamini akubali hilo?
Magu mjanja sana - alimweka Jenny pale makusudi kabisa! Ukweli Jenny ni Mwanasiasa makini kwa maana ya siasa kweli. Huwezi kuamini kama elimu yake ni Diploma tu ya Ualimu. Jenny ni mtekelezaji mzuri wa maelekezo ndiyo maana alidumu pale. Ni msomaji mzuri wa trends za watakayo wakuu! Hana reasoning yake binafsi - attitude yake ni kutetea hata lisilo jema.
Ni mara moja tu alijaribu kutetea uamuzi mzuri wa Serikali wa kuunganisha mifuko ya pensheni. alitoa maneno yake pale Ikulu lkn bado hayakuzaa kitu ingawa yaliokoa asitumbuliwe kwani tayari Mkulu alikuwa kishaamua kuiharibu sekta ya hifadhi ya jamii kwa sababu ya kuzitaka fedha za mifuko.
Dada na Mheshimiwa Waziri wa Nchi Jenny kama utasoma hii thread jua kuwa huna la kujivunia katika miaka yako mitano kwamba uliboresha hali za wafanyakazi. Wewe ni Waziri uliyeumiza wafanyakazi kuliko Mawaziri wote waliowahi kusimamia jukumu hilo katika nchi yetu. U
kirudishwa nafasi hiyo na ukaendelea hivyo hivyo basi mtakuwa mnaunda nchi ya kidikteta kwani wafanyakazi hawatakuwa na uhuru wa kusikilizwa kuhusu maslahi yao kwa miaka kumi.
Mwenyezi Mungu wetu ni mwema na ni kweli anakuona!