Jenista Mhagama: Naamini kabisa tunao uwezo wa kuondoka na kufika kule tunapofikia

Erick Richard R-Madrid

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
399
282
1d7c7a3f888c666bd56a3d12cb0b10e2.jpg

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama amesema kwamba waajiri nchini wanashindwa kuajiri nchini kutokana na nguvu Kazi kutokuwa na ujuzi unaotakiwa katika soko la ajira hapa nchini yetu ya Tanzania.

Ameongeza kwa kusema kwa utafiti uliofanya hapa nchini mwaka 2014 unaonyesha watanzania ambao wapo katika soko la ajira wenye ujuzi wa hali ya juu ni asilimia 3.6 tu (3.6%).



Pia watanzania wenye ujuzi wa kati no asilimia 16 tu (16%) kati ya nguvu kazi yote tuliyonayo hapa nchini, pia watanzania wenye ujuzi wa hali ya chini kabisa ni asilimia 79.9 (79.9%).

Amesema ni wakati wa watu na taasisi kuhama kutoka katika maandishi na makaratasi na kila mtu aamue kubadilika na kujiona ni part ya uchumi katika chachu ya mabadiliko nchini Tanzania.

"Tunaweza kuondoka na kufikia kule tunapotaka kufikia" Jenista Mhagama
 
Back
Top Bottom