Jenista Mhagama atolea Ufafanuzi Mgogoro wa CUF, maandamano na kazi za Msajili wa Vyama

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,688
2,000
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU YALIYOJILI WAKATI WAZIRI MHAGAMA AKIJIBU HOJA ZINAZOIHUSU OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA, 10 APRIL 2018

Waziri wa Nchi, (Sera, Bunge, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama amezitolea ufafanuzi hoja za kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria pamoja na hoja zilizotolewa na wabunge wakati wakichangia majadiliano ya utekelezaji wa bajeti 2017/2018 na makadirio ya bajeti ya mwaka 2018/2019 ya Ofisi ya Waziri Mkuu na mafungu ya taasisi zinazosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwemo Ofisi ya Msajii wa Vyama vya Siasa nchini kama ifuatavyo;

Msajili wa Vyama vya Siasa amepongezwa kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akifanya siku zote wakati akiratibu na kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria namba 5 ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992.

Mheshimiwa Mhagama amesema kuwa Msajili wa Vyama vya siasa hawezi kuingilia mgogoro uliopo katika Chama cha Wananchi CUF kwa sababu mgogoro huo upo mahakamani.

Endapo CUF itaona vyema kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuingilia kati mgogoro huo, ifuate taratibu za mahakama za kuondoa kesi inayohusu mgogoro huo mahakamani vinginevyo Msajili hawezi kuingia mgogoro huo
Hoja nyingine iliyofafanuliwa ni suala la maandamano ambapo Serikali imesema kuwa suala hilo linaratibiwa na vyombo vya usalama wa nchi na Jeshi la Polisi.

Vyama vyote vya siasa vimetakiwa kuhakikisha maandamano yanayofanyika yanazingatia Sheria za nchi.
Aidha Mhe. Mhagama ameuhakikishia umma wa watanzania kuwa Serikali iliamua kwa dhati kuingia katika siasa ya mfumo wa vyama vingi miaka 26 iliyopita na amemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa kuhakikisha anakichukulia hatua za kisheria chama chochote cha siasa ambacho kitafanya shughuli zake kwa kutofuata sheria za nchi.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Dodoma
 

Rugaiyulula

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,378
2,000
Tuliamua kwa dhati kuwa na siasa za vyama vingi miaka 26 iliyopita. Lakini kwa sasa hivi tumeamua kwa dhati shughuli za siasa za vyama vingi hadi 2020. Hello Hon Mhagama please differentiate between the two!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Heci

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
1,843
2,000
[HASHTAG]#26042018[/HASHTAG] Dead or live, we are ready
 

3llyEmma

JF-Expert Member
Oct 23, 2017
5,268
2,000
Hv wale wabunge wa CUF walioshinda kesi mahakamani vp walisharudi bungeni.
 

Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,660
2,000
Mwamuzi au mpatanishi mzuri ni yule asiyeonekana kuwa na upande. Msajili wa vyama ameshajiondolea sifa hii na ni vigumu yeye kuwa mpatanishi bora katika tatizo hili la CUF.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom