johnsonmgaya
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 2,818
- 3,729
Jengo la Water front pembezoni mwa bandari ya Dar inawaka moto muda huu ikumbukwe ni mara ya pili hili jengo kupatwa na ajali hii.
Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani jijini Dar es Salaam limefunga kwa muda barabara ya Sokoine kufuatia jengo la Water Front kuwaka moto. Wamefanya ili kuongeza ufanisi katika juhudi za uokoaji zinazoendelea.
======
UPDATES;
======
Moto umezuka katika baadhi ya maeneo ya Jengo la NSSF Water Front lililopo Jijini DSM, ambapo zipo Ofisi za Waziri wa Viwanda na biashara na kusababisha mtu mmoja kupoteza fahamu na kukimbizwa hospitali.
Mwandishi wa TBC alifika eneo la tukio na kuzungumza na Waziri wa viwanda na biashara CHARSE MWIJAGE ambaye ametoa wito kwa Ofisi mbali mbali kutoa Elimu kwa wafanyakazi wao ya namna ya kujiokoa pindi kunapotokea ajali kama hizo.
Chanzo cha moto huo kinaelezwa kuwa ni moto ulioanzia katika Bajaji iliyokuwa imeegezwa katika maeneo ya jengo hilo. Moto huo umetokea majira ya mchana na tayari umedhibitiwa na vikosi vya zimamoto na uokoaji.