Jengo la ushirika "tfc ltd" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jengo la ushirika "tfc ltd"

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by KASRI, May 5, 2009.

 1. K

  KASRI Member

  #1
  May 5, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Niliamua kufuatilia mwenyewe ndani ya jengo hilo kujua hasa kuna nini kinaendelea. Bahati mbaya kufika hapo nikaelezwa kuwa wahusika wapo ghorofa ya 9 ndani ya jengo hilo, nikaingia ndani ya lifti. Lahawla!!!! lifti inaendeshwa huku ikishtua shtua sijui kama ni nzima. Sikuthubutu kuuliza maana tulikuwa watu kama 14 kwa wakati mmoja wote wanaonekana ni wenyeji maana wanamtania mwendesha lifti kwa jina.
  Ghafla wote wakashuka ghorofa ya 4 kuuliza nikaelezwa ni kwa Msajili wa makampuni BRELA.
  Ghorofa ya 8 nikakuta bango kubwa EXPORT PROCESSING ZONES AUTHORITY "EPZA"
  Ghorofa ya 9 TFC LTD (wamiliki wa jengo). Nilisita kushuka maana sikuwa na maelezo yakutoa kwa wakati huo. Dereva/mwendesha lifti nikamuuliza Wizara ya Viwanda ilipo akajibu wamehama, zimamoto akaniambia ghorofa ya kwanza. .....NILICHOKA!

  Nategemea kujulishwa zaidi na wana JF maana jengo baada ya kuungua zaidi ya mwaka sasa linaonekana kama limesuswa.
  Vipi wawekezaji wamegoma?
  Mwenyejengo hasa ni nani?
  Wanampango gani?
  Kuna kesi yoyote iliyopo mahakamani?

  Sehemu jengo lilipo ni pazuri sana kuwekeza hasa maofisi, hoteli nk.
   
Loading...