Jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria lahitaji bilioni 4/- | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria lahitaji bilioni 4/-

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 12, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria, unahitaji jumla ya Shilingi bilioni nne (sawa na dola milioni 3.7 za Marekani) kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ofisi na makazi ya kudumu ya balozi.
  Ubalozi huo tayari umepatiwa notisi ya kunyang’anywa eneo kwa kushindwa kuliendeleza.
  Hayo yalielezwa na Balozi Msuya Mangachi, mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipotembelea ubalozi huo uliopo jijini Abuja juzi kukagua eneo la kiwanja cha ofisi na kisha kuonana na watumishi wa ubalozi huo.
  Balozi Mangachi alisema serikali ya nchi hiyo imeipatia Serikali ya Tanzania eneo la kujenga ofisi za ubalozi lenye ukubwa wa mita za mraba 5,294 na eneo jingine la kujenga makazi ya balozi lenye ukubwa wa mita za mraba 2,500 na kwamba tangu mwaka 1995 halijaendelezwa kwa sababu ya kukosa fedha za ujenzi.
  Hata hivyo, Serikali ya Tanzania imeshatoa dola 80,000 za Marekani kwa ajili ya kujenga uzio ili eneo hilo lisichukuliwe.
  Pia alimweleza Waziri Mkuu kwamba maeneo ambayo Tanzania inaweza kunufaika kwa kushirikiana na nchi ya Nigeria ni sekta ya elimu, kilimo, ufugaji samaki wa mapambo, biashara, michezo hasa soka na utengenezaji wa filamu.
  Akitoa mfano, alisema Serikali ya Afrika Kusini imepata walimu wengi kutoka Nigeria wa masomo ya sayansi na Kiingereza lakini ni baada ya kuwafuata na kuwasaili nchini kwao (Nigeria) ili kubaini uhalisi wa vyuo walivyotoka na uhalali wa vyeti vyao.
  Akizungumzia kuhusu fursa za kibiashara na Wanigeria, Balozi Mangachi alisema kuna fursa kubwa ya biashara kwa sababu wakazi wake hawalimi kwa kiasi kikubwa na kila kitu wanaagiza kutoka nje ya nchi yao hasa baada ya kugundua wana biashara kubwa ya mafuta.
  “Pia kipato cha mtu wa kati ni kikubwa ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika,” aliongeza.
  Akijibu hoja hizo, Waziri Mkuu alisema kuna haja ya kuangalia uwezekano wa kupata walimu kutoka Nigeria kama ambavyo Afrika Kusini imenufaika kwa sababu Tanzania bado inakabiliwa na uhaba wa walimu hata katika vyuo vya kufundishia walimu hao.
  Kuhusu kilimo, Waziri Mkuu alisema bado Tanzania inakabiliwa na changamoto ya kuinua hadhi ya zao la muhogo ili uweze kupata soko zuri duniani.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ni hili imetokea kutangazwa lakini ukweli ni kuwa hiyo ni hali ya kawaida kwa uwakilishi wetu nje. Viwanja vimekuwa vikichukuliwa na wenyeji kila siku. Kama Taifa tumekosa commitment katika jambo hilo!
   
Loading...