Jengo la Tume ya uchaguzi nchini Nigeria limeteketea kwa moto

Shigganza

Senior Member
May 24, 2018
160
500
Jengo la Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria, limeteketea moto zikiwa ni takribani siku sita kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu.


DyqmUa3U8AExMJh-600x300.jpegKwa mujibu wa msemaji wa tume hiyo, jengo hilo ambalo lipo katika Jimbo la Plateau liliteketea jana na kuunguza vitu vyote muhimu katika uchaguzi huo yakiwamo makasha na karatasi za kupigia kura.
Msemaji huyo alisema njama hizo ni kutaka kukwamisha shughuli hiyo ya upigaji kura, lakini akakaririwa na gazeti la This Day akisema bado ni mapema kuwatuhumu wahusika.
Uchaguzi huo mkuu unatarajiwa kufanyika Jumamosi hii Februari 16, 2019.


Katika hatua nyingine, Mshirika mkuu wa Rais Muhammadu Buhari katika uchaguzi huo, Nasir El-Rufai amewatishia raia wa kigeni akisema yeyote ambaye atajaribu kuingilia mchakato huo atarejeshwa nyumbani kwao akiwa ndani ya mfuko wa kuhifadhia maiti.


Nasir El-Rufai, ambaye ni Gavana wa Jimbo la Kaduna, alitoka kauli hiyo juzi katika mahojiano na Kituo cha Televisheni ya Taifa, ilipoanzishwa mada kuhusu jukumu la jumuiya za kimataifa katika uchaguzi huo.
 

Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
19,275
2,000
Kazi ipo,Buhari kashikwa pabaya. Hataki kuachia madaraka kama tarehe zilivyopangwa. Anataka kuendelea kuwa Rais kwa miezi kadhaa.
 

doup

JF-Expert Member
Feb 26, 2009
2,171
2,000
Afrika sijui nani katuloga. Hiyo ninhasara kubwa kwa taifa. Yaani watu kuteketeza pesa za walipa kodi kwa maslai yao hawaoni tabu
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
28,599
2,000
Africa bila unafiki haiendelei,haya ndio maneno Buhari alisema wkt wanamuondoa rais wa Gambia.

Buhari said, “We had to go through those actions because it was the only option for Nigeria and ECOWAS.

“We thank God for the role He allowed us to play in the Gambia. We believe in multi-party democracy. In Africa, it is absolutely necessary but for the system to work and one to come out of it clean, there is need for patience.

‘‘Patience on the part of leaders is also necessary in view of ethnic and religious diversities that prevail. Leaders must be patient, hardworking and resourceful.”
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,497
2,000
Siku zote anaevuruga 'Draft' ni Yule anaehisi anashindwa

Huenda Hata Wapinzani wanaweza kuchoma Moto Jengo la Tume kwa Kuwa watu wengi watahisi Ni Serikal

2020 Tume ya Uchgauzi waimarishiwe Ulinzi kwa Kuwa Huenda Vibaraka wa Mabeberu wakachoma Moto jengo kusingizia Serikal

1983 Nchi Moja wapo ya America Kusini Mpinzani wao aliekuwa Kwenye Peek alipigwa Risasi akafa watu wakalipuka kwa Maandamano wakaangusha Mamlaka iliyokuwepo Na Mke wa Yule Mpinzani akatawazwa Kuwa Rais nae akaitisha Uchunguzi huru kujua chanzo Cha Kifo Cha Mumewe

Ikaja kugundulika Ni mchezo wa Maadui waliotaka kuangusha Serikal kwa kuwatia hasira Wananchi

Hapa Nchin kwetu Mchezo Kama huo ulijaribiwa 2011 Kwenye Mgomo wa Madaktari japo haukufanikiwa kwa Kuwa Watu walistuka Na Jk kwa ujasiri wa Kijeshi alionao alikataa Wazo la kuifuta TGNP iliyokuwa imeratibu uasi ule
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom